Mtanzanias
JF-Expert Member
- Jul 30, 2021
- 1,747
- 3,725
Leo hii analaumiwa Okrah, mechi iliyopita alilaumiwa Zoran, ya ngao akalaumiwa Inonga, sasa nyie kila mechi mtakuwa mnatafuta kichaka cha kufichia madhaifu yenu?
Mlikuwa mnasema Juma Mgunda atainyoosha Yanga kwakuwa alipata sare moja ya nusu fainali kule Arusha, nikawauliza kabla ya mechi wanipe rekodi za Mgunda mara ya mwisho kuifunga Yanga ilikuwa ni lini wakaja na stori za hii ni Simba siyo Coast Union, nikasema sawa.
Hiyo Simba mara ya mwisho kamfunga Yanga lini wakaangaliana kama walioshikwa ugoni, nikawaambia rekodi zote zinawakataa. Jeuri ya kumfunga Yanga kwa sasa haipo kwenu hata mkatafute kocha chini ya bahari hamuwezi kumfunga Yanga.
Huyo Mgunda kwenye mechi 6 alizokutana na Yanga kaambulia sare mbili, nyingine kabutuliwa ndiyo mlitegemea leo awape ushindi mbele ya Yanga?
Kama siyo kurusha lawama kwa Okrah mngefanya nini? Viongozi wenu hawajampa mkataba, walikuwa wanategeshea hii mechi waone kama atapata matokeo ndiyo wampe Ukocha Mkuu. Lakini naona ngoma imekuwa nzito, ameshindwa kuutafuna mfupa uliowashinda makocha wengi. Inabidi sasa atafutwe Kocha Mkuu na yeye awe msaidizi, matunguli ya Kitanga yamekwamia bagamoyo.
Sasa kichaka kimoja kilichobaki kufyekwa watu waishiwe hoja ni mechi za kimataifa, na chenyewe kitafyekwa karibuni na hapo mashabiki uchwara wataibua jipya la hatumtaki Mo badala ya Mgunda na Matola.