Mashabiki wa Simba tujiandae kisaikolojia!

Mashabiki wa Simba tujiandae kisaikolojia!

Hawa Asec wa sasa hawana mpira wowote Simba akifungwa na hawa utakua ni uzembe mkubwa sana. Wanafungwa fungwa tu huko ligi ya kwao. Kwakifupi kwenye kundi la Simba akikaza anaongoza hilo kundi kuelekea robo fainali. Pamoja na ubovu wa Simba kwa sasa na kukosa kocha lakini sioni timu ya kuisumbua Simba kwenye kundi lao. Simba atakwenda robo fainali tena kwa kishindo kikuu
Asec wanaongoza league ya kwao,pili ni moja ya timu iliyojaa vijana wadogo. Sasa ule ugoigoi wenu mkipoteza mpira hamuwahi recover mpira mnatembea,mtapigwa nyingi. Msimu huu kwenye mechi zote ulizocheza cleansheet hazidi tatu,kila mechi unamuhusu magoli.

Hapo lazima muwe na utimamu wa mwili,ili muweze kushindana na timu iliyo sheheni vijana wadogo la sivyo,mmejitahidi sana droo.
 
Hawa Asec wa sasa hawana mpira wowote Simba akifungwa na hawa utakua ni uzembe mkubwa sana. Wanafungwa fungwa tu huko ligi ya kwao. Kwakifupi kwenye kundi la Simba akikaza anaongoza hilo kundi kuelekea robo fainali. Pamoja na ubovu wa sasa na kukosa kocha lakini sioni timu ya kuisumbua Simba kwenye kundi lao. Simba atakwenda robo fainali tena kwa kishindo kikuu
Aminaaaa....
 
Hatuwezi kupoteza hiyo mechi b... Huwa tuko tofauti sana kwenye mechi za CAF. Hii ni kawaida yetu kwa miaka yote. Ndiyo mechi yetu ya kurejesha kujiamini kwetu.

Oba
Kitu nakukubali huwa hujikatii tamaa. Mungu awasaidie msiaibike sana.
Goli chache zinatosha kwa kufungwa b…
 
Wanalunyasi,

Ni vizuri kuambiana ukweli wengine msije kufa kwa pressure game na Asec. Timu yetu mpaka sasa haina kocha mkuu wala kocha wa fitness.

Timu inafanya mazoezi na waalimu ambao kwa muda huu mfupi huku wakiwa wanajua wanashikilia bomba kwa muda mfupi ni ngumu kuwa motivated!

Tunahamasishwa kwenda uwanjani bila viongozi kuonesha nia na commitment mpya baada ya kipigo cha aibu dhidi ya watani. Kwenye press zao wanajitetea tu bila kukubali kuwajibika pia.

Matatizo ya Simba kiufundi msitegemee mabadiliko makubwa sana kwa muda huu mfupi. Juma Mgunda angeweza kutusaidia kwa program fupi lakini hawa waliopewa timu tujiandae.

Swala la kocha mkuu ni dharura, linapaswa lifanyiwe kazi kidharura. Kama funds zipo kupata kocha bora sio tatizo ila kama budget ni kikwazo lazima itatuchukua muda mrefu na kutugharimu.

Game na Asec haina dalili nzuri mpaka sasa. Viongozi wetu wachangamke na pia wawe na data base ya makocha wakubwa wenye vigezo ili kutafuta kocha isiwe kama anatokea sayari nyingine.
Ilikuwa kosa kubwa kumfukuza kocha na kutuhumu wachezaji bila ushahidi kwa kusikiliza kelele za washabiki oya oya. Nilionya kuwa japokuwa iliuma kufugwa goli tano lakini tukumbuke tuko kwenye ligi, tuangalia yajayo matokeo yake ndiyo haya. Nina uhakia asingefukuzwa kocha mchezo na Namungo tusingedondosha poin mbili ambazo ndiyo zimempa ubingwa utopolo.
 
Nawalaumu saaaaana wanachama wenzetu waliomchagua Mangungo kuwa mwenyekiti kwani huyu yupo hapo kuitumia Simba kama ngazi ya kupandia kupata ubunge. Kila mwanachama wa Simba ambaye alimpa kura Mangungo ajue anahusika na anguko la Simba.
 
Yani hakuna kipigo kitaniumiza kama kilichopita cha watani wa jadi, nilishindwa hadi kutoka nje ya geti.
Hata tufungwe ngapi kwa sasa sitoumia kwasababu ndicho ninachokitegemea kitokee maana Uongozi ni kama haupo na timu hamna.
 
Nawalaumu saaaaana wanachama wenzetu waliomchagua Mangungo kuwa mwenyekiti kwani huyu yupo hapo kuitumia Simba kama ngazi ya kupandia kupata ubunge. Kila mwanachama wa Simba ambaye alimpa kura Mangungo ajue anahusika na anguko la Simba.
Mangungu ana kosa gani?
 
Wanalunyasi,

Ni vizuri kuambiana ukweli wengine msije kufa kwa pressure game na Asec. Timu yetu mpaka sasa haina kocha mkuu wala kocha wa fitness.

Timu inafanya mazoezi na waalimu ambao kwa muda huu mfupi huku wakiwa wanajua wanashikilia bomba kwa muda mfupi ni ngumu kuwa motivated!

Tunahamasishwa kwenda uwanjani bila viongozi kuonesha nia na commitment mpya baada ya kipigo cha aibu dhidi ya watani. Kwenye press zao wanajitetea tu bila kukubali kuwajibika pia.

Matatizo ya Simba kiufundi msitegemee mabadiliko makubwa sana kwa muda huu mfupi. Juma Mgunda angeweza kutusaidia kwa program fupi lakini hawa waliopewa timu tujiandae.

Swala la kocha mkuu ni dharura, linapaswa lifanyiwe kazi kidharura. Kama funds zipo kupata kocha bora sio tatizo ila kama budget ni kikwazo lazima itatuchukua muda mrefu na kutugharimu.

Game na Asec haina dalili nzuri mpaka sasa. Viongozi wetu wachangamke na pia wawe na data base ya makocha wakubwa wenye vigezo ili kutafuta kocha isiwe kama anatokea sayari nyingine.
Heri umekuwa mkweli
Umewaambia ukweli wenzio.

Ni kipigo kingine hadi akili ziwakae sawa muache kufukuza makocha kwa mihemko kisa tu mmwfungwa na Yanga.
 
Back
Top Bottom