Mashabiki wa Simba tujiandae kisaikolojia!

Asec wanaongoza league ya kwao,pili ni moja ya timu iliyojaa vijana wadogo. Sasa ule ugoigoi wenu mkipoteza mpira hamuwahi recover mpira mnatembea,mtapigwa nyingi. Msimu huu kwenye mechi zote ulizocheza cleansheet hazidi tatu,kila mechi unamuhusu magoli.

Hapo lazima muwe na utimamu wa mwili,ili muweze kushindana na timu iliyo sheheni vijana wadogo la sivyo,mmejitahidi sana droo.
 
Aminaaaa....
 
Hatuwezi kupoteza hiyo mechi b... Huwa tuko tofauti sana kwenye mechi za CAF. Hii ni kawaida yetu kwa miaka yote. Ndiyo mechi yetu ya kurejesha kujiamini kwetu.

Oba
Kitu nakukubali huwa hujikatii tamaa. Mungu awasaidie msiaibike sana.
Goli chache zinatosha kwa kufungwa b…
 
Ilikuwa kosa kubwa kumfukuza kocha na kutuhumu wachezaji bila ushahidi kwa kusikiliza kelele za washabiki oya oya. Nilionya kuwa japokuwa iliuma kufugwa goli tano lakini tukumbuke tuko kwenye ligi, tuangalia yajayo matokeo yake ndiyo haya. Nina uhakia asingefukuzwa kocha mchezo na Namungo tusingedondosha poin mbili ambazo ndiyo zimempa ubingwa utopolo.
 
Nawalaumu saaaaana wanachama wenzetu waliomchagua Mangungo kuwa mwenyekiti kwani huyu yupo hapo kuitumia Simba kama ngazi ya kupandia kupata ubunge. Kila mwanachama wa Simba ambaye alimpa kura Mangungo ajue anahusika na anguko la Simba.
 
Yani hakuna kipigo kitaniumiza kama kilichopita cha watani wa jadi, nilishindwa hadi kutoka nje ya geti.
Hata tufungwe ngapi kwa sasa sitoumia kwasababu ndicho ninachokitegemea kitokee maana Uongozi ni kama haupo na timu hamna.
 
Nawalaumu saaaaana wanachama wenzetu waliomchagua Mangungo kuwa mwenyekiti kwani huyu yupo hapo kuitumia Simba kama ngazi ya kupandia kupata ubunge. Kila mwanachama wa Simba ambaye alimpa kura Mangungo ajue anahusika na anguko la Simba.
Mangungu ana kosa gani?
 
Heri umekuwa mkweli
Umewaambia ukweli wenzio.

Ni kipigo kingine hadi akili ziwakae sawa muache kufukuza makocha kwa mihemko kisa tu mmwfungwa na Yanga.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…