Mashabiki wa Simba wamebadilika sana

Mashabiki wa Simba wamebadilika sana

Albinoomweusi

JF-Expert Member
Joined
Oct 28, 2016
Posts
3,433
Reaction score
8,585
Anaandika @exaud_msaka_habari

Kuna kitu kikubwa sana kimebadilika kwenye mfumo wa Mashabiki wa Simba wa kuisapoti timu yao, nadhani sio mbaya na wengine wakajifunza kwao.

Jana nilibahatika kuona ile mechi na nilikaa na mashabiki wa Simba hata kabla hawajapata goli walikuwa wameshakubali kuwa jana haikiwa siku nzuri kazini.

Nimefuatilia Mahojiano yao nje ya uwanja baada ya mechi nimegundua wanaanza kuelewa maana ya Soka, wanaanza kuelewa ile kauli ya mpira una matokeo ya Kikatili.

Kwa baadhi ya Matukio ya uwanjani wengi tulitegemea kusikia lawama nyingi kwa watu mbalimbali.

Goli la Mugalu ambalo mwamuzi alisema ni Offside lazima mwamuzi angetoka na ulinzi wa Polisi pale, na leo tungeona Press ya kuuliza "SJUI TUJITOE".

Kushikwa mkono kwa Shomari Kapombe ndani ya Box na mwamuzi kutokuona nakwambia ingekuwa zamani leo kusingekalika huku.

Kwa idadi ya Magoli aliyokosa jana Mugalu nina uhakika leo mjadala ungekuwa aondoke au asiondoke, ila kitu cha kushangaza hakuna lawama.

Kuanza nje kwa Morrison na Chama na baadae wakaingia na kubadilisha mchezo basi leo Gomezi angekuwa amewekwa kiti cha moto akijadiliwa uwezo wake, ila naona wametulia ina maana wameelewa.

Jana baada ya mchezo kuna makala ilikuwa inatembea mitandaoni ya mashabiki wa Simba wakiwapongeza wachezaji wao na kuwapa moyo, jambo ambalo ni mpya sana kwenye soka la Tanzania ni nadra mno kuona.

Nadhani kubadilika kwa mashabiki wa Simba kunatokana na imani waliyonayo kwa wachezaji wao, kunatokana na kutokuwepo kwa makundi ndani ya timu, lakini pia kiwango cha uwanjani kilichoonekana.

Tunajifunza kuwa sio kila mechi inapokuwa ngumu lazima utafute mtu wa kumshushia lawama, wakati mwingine unakubaliana na matokeo, mnapeana moyo mnaendelea, hii ikiweza kuingia kwenye kila timu basi hata maendeleo katika soka yatakuwepo.

ALL IN ALL PRISONS HAWAJAMLAUMU REFA IL
 
Kilichifanya tulizike ni jinsi mpira ulivyokua unachezwa unaona kabisa simba kawa mbogo anashambulia kwa nguvu pasi zinaonekana mashuti yanaenda golini kipa anapangua energy kubwa ata tungefungwa tungekubali lakini kama tunaenda droo na mpira wa ovyo ovyo akuna atakae kuelewa kila mtu aliona akakubali.
 
Team ikiwa na muendelezo wa matokeo mazuri na mpira mzuri na mnaona kabisa wachezaji wanapambana. Siku ikienda vibaya unaona kabisa hii leo game imetukataa. Yaani jana hata kama sare tusingepata asingekuwepo wa kulaumu na angetokea ningeshiriki kumshangaa.

Kuna wakati huna budi kuuheshimu mpira na hali halisi.
 
Team ikiwa na muendelezo wa matokeo mazuri na mpira mzuri na mnaona kabisa wachezaji wanapambana. Siku ikienda vibaya unaona kabisa hii leo game imetukataa. Yaani jana hata kama sare tusingepata asingekuwepo wa kulaumu na angetokea ningeshiriki kumshangaa.

Kuna wakati huna budi kuuheshimu mpira na hali halisi.
kabisa kwa mashambulizi Yale utamlaumu nani utaanzia wapi utajionea aibu mwenyewe prison walibaki nyuma simba alifanya kila jitiada ili apate goli ata ile penati akuna aliekumnuka kama tulikosa penati kutokana na timu ilivyo pambana ki mpira safi
 
Bado mnajitetea tu?? Sisi tumesahau hayo tunasubir tar 16😂😂😂😂
 
Hawajabalika chochote, bado ni mbumbumbu kama alivyosema Rage,ukitaka kuamini angalia comments zao humu.
 
Simba wa sasa ni Simba Nyikaa anawinda kwa akili na maarifa na nguvuu. Simba Nguvu moja
 
SIO KWELI..kinachowapa 'busara' mashabiki wa simba ni ile performance ya timu yao kwenye CCL...ila subiri itokee droo nyingine au kule CCL mambo yaende ndivyo sivyo tutakuja kuufukua huu uzi.
 
SIO KWELI..kinachowapa 'busara' mashabiki wa simba ni ile performance ya timu yao kwenye CCL...ila subiri itokee droo nyingine au kule CCL mambo yaende ndivyo sivyo tutakuja kuufukua huu uzi.
Lakini pamoja na Uvumilivilu wetu mwambieni Kocha Mugalu ni KIMEO, Mugalu hana kiwango cha kucheza Simbaaaaa
 
Simba kwa Prisons ni wachumba tu. Mechi ya awali walifungwa ugenini, na mechi ya marudiano wameponea tu chupu chupu kunyukwa tena nyumbani na hao wababe wao!
 
Mashabiki wa Simba tuna relax iwe Simba inashinda,inafungwa ama inadroo.
Kama ni lawama basi uwa ni chache sana kwa wachezaji wasioonyesha jitihada uwanjani.
 
Back
Top Bottom