Albinoomweusi
JF-Expert Member
- Oct 28, 2016
- 3,433
- 8,585
Anaandika @exaud_msaka_habari
Kuna kitu kikubwa sana kimebadilika kwenye mfumo wa Mashabiki wa Simba wa kuisapoti timu yao, nadhani sio mbaya na wengine wakajifunza kwao.
Jana nilibahatika kuona ile mechi na nilikaa na mashabiki wa Simba hata kabla hawajapata goli walikuwa wameshakubali kuwa jana haikiwa siku nzuri kazini.
Nimefuatilia Mahojiano yao nje ya uwanja baada ya mechi nimegundua wanaanza kuelewa maana ya Soka, wanaanza kuelewa ile kauli ya mpira una matokeo ya Kikatili.
Kwa baadhi ya Matukio ya uwanjani wengi tulitegemea kusikia lawama nyingi kwa watu mbalimbali.
Goli la Mugalu ambalo mwamuzi alisema ni Offside lazima mwamuzi angetoka na ulinzi wa Polisi pale, na leo tungeona Press ya kuuliza "SJUI TUJITOE".
Kushikwa mkono kwa Shomari Kapombe ndani ya Box na mwamuzi kutokuona nakwambia ingekuwa zamani leo kusingekalika huku.
Kwa idadi ya Magoli aliyokosa jana Mugalu nina uhakika leo mjadala ungekuwa aondoke au asiondoke, ila kitu cha kushangaza hakuna lawama.
Kuanza nje kwa Morrison na Chama na baadae wakaingia na kubadilisha mchezo basi leo Gomezi angekuwa amewekwa kiti cha moto akijadiliwa uwezo wake, ila naona wametulia ina maana wameelewa.
Jana baada ya mchezo kuna makala ilikuwa inatembea mitandaoni ya mashabiki wa Simba wakiwapongeza wachezaji wao na kuwapa moyo, jambo ambalo ni mpya sana kwenye soka la Tanzania ni nadra mno kuona.
Nadhani kubadilika kwa mashabiki wa Simba kunatokana na imani waliyonayo kwa wachezaji wao, kunatokana na kutokuwepo kwa makundi ndani ya timu, lakini pia kiwango cha uwanjani kilichoonekana.
Tunajifunza kuwa sio kila mechi inapokuwa ngumu lazima utafute mtu wa kumshushia lawama, wakati mwingine unakubaliana na matokeo, mnapeana moyo mnaendelea, hii ikiweza kuingia kwenye kila timu basi hata maendeleo katika soka yatakuwepo.
ALL IN ALL PRISONS HAWAJAMLAUMU REFA IL