Mashabiki wa Simba wamebaki na Historia tu

bryan2

JF-Expert Member
Joined
Jun 8, 2016
Posts
3,323
Reaction score
4,679
Hakika miaka inaenda mbio sana hawa mashabiki wa Simba wao wanataka kufa tai Shingoni hawataki kukubali timu yao inahitaji mabadiliko wamebaki kukalia ishu za Yanga na wachambuzi wao wa kimchongo.

Walianza kumlaghai Feisal kuihujumu Yanga wakidhani kuondoka kwa feisal yanga itayumba Yanga ndio ikazidi kusimama imara chini ya Mwamba Eng Hersi na Kocha wa Viwango Nabi Nyuma ya Feisal kuna mambo mengi sana na pia kuna watu wengi mnoo achana na ishu ya mkataba hiyo cha mtoto tu.

Simba baada ya kuona Yanga wameshindikana uwanjani wakaja na gia hafifu ya kumlaghai Feisal aliyekua kati ya wachezaji tegemeo wa Yanga how comes mchezaji imara unasusa huku timu yako ikiwa na mchezo mgumu mbeleni kuna mikono ya watu.

Yanga ishukuru sana ilisinya wachezaji wengi wa nje wanaolewa maana ya kazi yao na wenye kufocus mbele take it from me Yanga ingekua na wachezaji wengi wa ndani ingekua inafungwa magoli ya ajabu ajabu sana wangepitishiwa bahasha za khaki na kuuza gemu, kuna kipa mmoja kipindi cha nyuma kuna shuti alidaka huku kakunja mikono.

Simba achaneni na historia mpira unabadilika wacheni janja janja mkiendelea na janja janja zenu hizo wapinzani wakubwa wa yanga watakuja kuwa Azam.

Shukuruni kundi lenu mmepangwa na timu nyepesi mnoo mngekua kundi la Mamelodi, Al hilal, Al ahly na coton sport mngeshakataana mapema sana, wakushukuriwa zaidi ni Vipers kwa kuwa mgawa pointi.

Wekezeni kwenye Mpira kwa manufaa ya soka la nchi yetu
 
Hivi na nyie mnaona kama navoona mm? Mtoa mada anadai simba kutwa kuiongelea yanga wakati yeue ndio naona anaiongelea simba hapa wakati haimuhusu.

Sasa yanga wanakwama wapi kuishitaki simba caf kwa kumrubuni fei wakati ana mkataba na yanga. Ni kosa kisheria mwambieni hersi aishtaki simba avune mijihela. Vinginevo basi huko wenye akili kichwani wawili tuu wengine woote mmejaa vinyesi kichwani.
 

Umemaliza mwamba wa Lusaka
Nimemkumbuka Rage sana baada ya kupitia comment yako

Kunywa maji utulize roho then jipige kifuani mara 2 huku ukisema hakika rage hakukosea
 
Mpira ni burudani ila mahaba yakipita kikomo unateseka sana.
 
Jitahidi kuwa na uandishi mzuri, wenye kujenga na kutetea hoja zako.

Unaandika hovyo sana
Binafsi nimeshindwa KUKUELEWA.
 
Jitahidi kuwa na uandishi mzuri, wenye kujenga na kutetea hoja zako.

Unaandika hovyo sana
Binafsi nimeshindwa KUKUELEWA.

Sawa boss next time ntakuja kivingine zaidi nimeandika huku nakimbizwa
 
Mpira ni burudani ila mahaba yakipita kikomo unateseka sana.

Sio kwa mashabiki wa Simba wao ngumi mkononi ashukuriwe vipers kaponya majeraha hali ingeendelea kuna siku mtu angekula makonde
 
Sio kwa mashabiki wa Simba wao ngumi mkononi ashukuriwe vipers kaponya majeraha hali ingeendelea kuna siku mtu angekula makonde
Wewe tu na mashabiki wenzako mnaoshabikia pamoja. Simba haina tatizo.
 
Simba achaneni na historia mpira unabadilika wacheni janja janja mkiendelea na janja janja zenu hizo wapinzani wakubwa wa yanga watakuja kuwa Azam.
Nje ya mada: Hivi si tulikubaliana kwamba tunagomea bidhaa za Azam? Nimekumbuka tu hiki kitu wakati nimeshanunua Azam embe hapa
 
Nje ya mada: Hivi si tulikubaliana kwamba tunagomea bidhaa za Azam? Nimekumbuka tu hiki kitu wakati nimeshanunua Azam embe hapa

We kunywa hata tano masta pesa yako tu.
 
Jf hakuna kipimo cha akili kweli au
#GreatThinker.....tuna safari ndefuuu
 
Kama mna team bora shirikisho mmefuata nini!?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…