Mashabiki wa Simba wamepekua jezi za Yanga wakaona mkono na tano ila wameshindwa kuzipekua jezi zao wakaona 1 5

Mashabiki wa Simba wamepekua jezi za Yanga wakaona mkono na tano ila wameshindwa kuzipekua jezi zao wakaona 1 5

Smt016

JF-Expert Member
Joined
Jan 11, 2016
Posts
3,012
Reaction score
4,300
Jezi za Simba zilitangulia kutoka kabla ya jezi za yanga, mashabiki wa Simba walisifia ubunifu ila kasoro ikawa ni neno SANDA peke yake. Sijajua mbunifu wa jezi za Simba aliwaza nini kuweka 1 5 kwenye jezi za Simba lakini uzuri hakuna aliyechukulia hilo kama nia mbaya ama mashabiki wa Simba kufikia kupekua hilo.

IMG_20240725_191819.jpg

Ila cha ajabu baada ya jezi za Yanga kutoka, tayari mashabiki wa Simba wameonesha kukereka na kitendo cha mbunifu wa jezi za Yanga kuweka namba tano na kuweka mkono. Hivi aliyeweka tano na mkono na aliyeweka 1 5 ni ipi inakera zaidi? Mmeacha kukereka kwenye jezi zenu wenyewe kwa kuwekewa matokeo ya November 5. Yaani kwa kifupi bango la matangazo waliokuwa wanaangaika kubandika Yanga barabarani, saivi utakutana nalo kwenye jezi za Simba ila wenyewe hawakereki wanakereka na jezi za Yanga.

yanga.jpg

Ama kweli Rage aliona mbali sana.

Pia soma: Naanza kupata wasiwasi na Sandaland kama mtengenezaji wa jezi za Simba
 
Attachments

  • IMG_20240725_191605.jpg
    IMG_20240725_191605.jpg
    205.8 KB · Views: 12
Mbunifu kaamua kuwafanya wajisikie uchungu kwa matokeo hivyo watapambanda kulipa kisasi. Hivyo hiyo moja kwa tano ni sehemu ya ukumbusho
 
Hawa jamaa tunawafrustrate kabla ya kuanza kwa msimu,yaani mpaka ligi iianze watakuwa wamechoka sana na bahati nzuri tunaanza nao ngao,tunawapasua bikra mapema kabisa,ligi ikianza watakuwa chawote
 
Hawa jamaa tunawafrustrate kabla ya kuanza kwa msimu,yaani mpaka ligi iianze watakuwa wamechoka sana na bahati nzuri tunaanza nao ngao,tunawapasua bikra mapema kabisa,ligi ikianza watakuwa chawote
Ingekuwa vizuri kabla hawajakaa sawa una refresh kwanza na goli zingine tano.
 
Back
Top Bottom