Tumekuwa tukishuhudia pindi Yanga anapokuwa uwanjani, basi mashabiki wa Simba hukaa upande wa wapinzani wa yanga ili kuwazomea.
Je katika mechi ya jumatano YANGA V/S AZAM mashabiki wa Simba watashangilia timu gani?
Nauliza hivyo nikiwa na maana yangu, kwa sababu imetokea kutokuelewana kati ya timu ya SIMBA vs AZAM kutokana na sakata la mchezaji RAMADHANI SINGANO (MESSI) mpaka baadhi ya viongozi wa Simba wakasusa na kusema hawatotumia bidhaa yoyote ile inayozalishwa na kampuni ya AZAM.
Je siku hiyo mashabiki wa simba watakaa upande gani?