Mashabiki wa soka ruksa kuingia viwanjani kushangilia kabumbu

Mashabiki wa soka ruksa kuingia viwanjani kushangilia kabumbu

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
Serikali imeruhusu mashabiki wa soka kuhudhuria uwanjani kwa kuzingatia taratibu za afya, isipokuwa kwa mechi kubwa wataingia nusu.

Mei 21 Rais Magufuli alitoa tamko la kuruhusu michezo yote na shule kuendela kuanzia Juni 1, 2020 kwa kuwa #CoronaVirus imepungua nchini. Alizitaka Wizara ya Afya kuweka taratibu za kushangilia.

Michezo yote ilizuiliwa tangu mwezi Machi baada ya #kuthibitishwa maambukizi ya #CoronaVirus nchini.

----
Serikali imetoa mwongozo wa kufuata katika michezo ya Ligi Kuu za Soka Nchini ambazo zinatarajiwa kuanza Juni Mosi, 2020, hivyo ni muhimu kuzingatia na kwa yoyote atakayekiuka taratibu hizo hatua kali zitachukuliwa dhidi yake - Dkt. Hassan Abbasi.

Katika kuzingatia Mwongozo wa Afya Michezoni, Serikali kupitia wizara zenya dhamana ya Afya na Michezo ilishatoa mwongozo wa mei 28, 2020 unaoelekeza hatua za kuchukuliwa katika kila hatua za kuendesha michezo nchini - Dkt. Hassan Abbasi.

Kuhusu mtindo wa uendeshaji wa Ligi za Soka, Serikali inaruhusu Ligi za Soka ambazo kikanuni timu zinatakiwa kucheza nyumbani na ugenini kwa kuzingatia kanuni na taratibu za kiafya - Dkt. Hassan Abbas.

Serikali imeridhia ligi zote zilizoruhusiwa kurejea kwa mashabiki watakaotaka kuhudhuria viwanjani waruhusiwe kwa taratibu za kawaida isipokuwa tu kwa mechi zitakazotathminiwa - Dkt. Hassan Abbasi.

===
1590923706566.png

1590923733290.png
 
Hayo masharti mbona ni marahisi sana kutekelezeka. Kuna haja ya kuruhusu pia ligi ya wanawake nayo iendelee kwa kuwa huwa haihudhuliwi na mashabiki wengi. Pia watu wanaofanya mazoezi wananafasi kubwa sana ya kupona hata wakiambukizwa Covid - 19.

Kimbembe nakiona huku mtaani kwenye vibanda umiza, sio rahisi kuzuia misongamano. Ila kwa kuwa CORONA imeisha hakuna tatizo.
 
Wiki iliyopita pia wizara ya afya walitoa release ukisoma ilibainisha haya yote.
 
SASA JAMANI mh! TUNAKOKWENDA HII VIDICO 91 ITARUDI TENA MI NAONA. AU NYIE MNAONAJE?
 
Covid hiyooo inaletwa kwa kasi kuliko hata ya VodaCom
 
Back
Top Bottom