Mashabiki wa soka wa Nchi gani wanaongoza kwa utukutu?

Mashabiki wa soka wa Nchi gani wanaongoza kwa utukutu?

bryan2

JF-Expert Member
Joined
Jun 8, 2016
Posts
3,323
Reaction score
4,679
Hatupo mbali sana na kombe la dunia kule kwa mzee Putin Russia Tumeona makundi ndo hayo tiyari yametoka huyu akipangwa na yule ili mradi burudani.

Zaidi ya burudani ya soka kiwanjani pia mashabiki nao wanatoa burudani tosha kuna wale dakika 90 wao ni kushangilia hata kama timu yao imepigwa goli kadhaa na kuna wale watukutu/wakorofi mnoo wao ni fujo mwanza mwisho.

Tulishuhudia pale Ufaransa kombe la mataifa Ya Ulaya mashabiki wa Soka wa Uingereza wakichapana ngumi kavukavu na wale wa Kirusi nusura Timu ya Taifa ya Urusi irudishwe Moscow kabla ya mashindano kwisha.

Kipindi cha Nyuma kidogo tulishuhudia Liverpool wakienda kucheza na club mmoja ya Uturuki kama sikosei Galatary mashabiki walichapana mnoo na mwishowe Vifo vilitokea.

Pale Italia San siro/Giusepe Meaza uwanja umepigwa nyaya kwa ajili ya kuzuia ukorofi wa mashabiki wa vilabu vya Inter Milan na Ac Milan.

Je tukienda kwenye Kombe la Dunia ni Mashabiki wa nchi gani wanahitaji Ulinzi wa ziada kutokana na utukutu wao???
 
Hawa nao ni tukutu mnooo mechi ya Galatasary,Fenerbance,Besiktas na fujo mwanzo mwisho na pia linachangiwa na political instability ndan ya nchi yao.
 
Argentina,,brazil na egypt...hawa nao kwenye nchi zao ni balaa
Hawa Egpyt nao sio salama mechi za Zamalek,Ismailia,Alhaly Mabomu ya machozi ni kawaida,viwanja bila mashabiki ni kawaida,Afrika ya kaskazini ina mashabiki watukutu mnoo tena utamu wameingiza timu 3 Kombe la dunia,Egypt,Morroco,Tunisia.
 
Simba noma sana kwanza washang'oaga viti uwanjani na kuvunja mageti
 
Back
Top Bottom