George Betram
JF-Expert Member
- Oct 10, 2015
- 4,672
- 6,272
How Broh..?power of marketing
Mimi ni shabiki kindakindaki wa NEWCASTLE UNITEDMimi ninaamini hivi:
Timu zote kubwa za Uingereza zimepata mashabiki kutoka Afrika kutokana na popularity iliyotokana na mafanikio yake katika kipindi fulani..!
Tukianza na Man Utd, timu hii ilianza kukusanya mashabiki wengi kipindi cha Fergie,usisahau na ule msimu wa mafanikio ya kutisha ya Fergie ndani ya Man Utd,msimu ambao Man Utd ilibeba vikombe vitatu vikubwa,Man Utd hii ilipata mashabiki wengi sana ulimwenguni,hii trend ya kuongezeka mashabiki wa Man Utd ulimwenguni iliongezeka mpaka Fergie alipoondoka...
Tukija kwa Liverpool, hii timu imepata umaarufu mkubwa na kujikusanyia mashabiki wa kutosha hapa Afrika kipindi cha Rafa Benitez,hii ndio ile Liverpool iliyoenda kufanya maajabu Istanbul, Liverpool ya akina Gerard,Kuyt na wenzake wengine,KUMBUKA kuwa Liverpool haijabeba ubingwa wa EPL kwa kipindi cha miaka 20 na kitu...
Upande wa Arsenal, hawa wamejipatia mashabiki wengi huku Afrika kipindi cha Mzee Wenger na Henry, hawa walitengeneza ile Arsenal isiyofungika...
Tukija kwa Chelsea, hawa Ndio huwa wananishangaza sana nikiona wanaicheka Man City na mashabiki wake,Chelsea imejikusanyia mashabiki wa kutosha sana Afrika kipindi cha ujio wa Jose Mourinho na yule tajiri wa Kirusi,hapa Mourinho alikuwa ametoka kuipa ubingwa wa Ulaya Porto,akaja kuipa Chelsea back to back EPL championships,Hii ilikua miaka ya 2005-2007 hapo..
Sasa jambo la kushangaza ni kuwa kwasasa mashabiki wa hizo timu tajwa hapo juu wanahoji uhalali wa Man City kuwa na mashabiki..!
Hakika inashangaza sana..!
Mimi naamini ya kuwa mashabiki wote wa timu kubwa za ulaya ni "Glory Hunters",kwasababu chimbuko la ushabiki wao kwa timu hizo ni mafanikio ambayo timu hizo zimeyapata ndani ya kipindi fulani,pia naamini kuwa timu inavyokuwa na mafanikio zaidi basi ndivyo inavyokuwa maarufu zaidi na watu kuanza kuifuatilia na hatimaye kujitengenezea mashabiki duniani kote..!
Kwangu mimi mashabiki wengi (kama sio wote) wa timu za Ulaya ambao yupo Afrika ni "Glory Hunters" tu..!
Je,nini mawazo yako,timu inapataje mashabiki nje ya mipaka ya nchi yake..?
Ukiacha kufanya vizuri kwa Simba na Yanga ligi ya Tanzania, sababu nyingine kuu ni kwa vile ni timu za mji mkuu, Dar enzi hizo kila kitu ilikua ni Dar ,Good topic halafu why mashabiki wa soka Tanzania wengi wao wapo Simba na Yanga tu?why Simba inapokwenda pale Iringa kucheza na Lipuli bado watajiona kama wako nyumbani,wao mashabiki wa Iringa hawaishabikii timu yao(maana bila Lipuli kuwepo wasingeona hizi timu zikija kwao)why hatuwi kama mashabiki wa UK ambao wanashabikia timu zao za nyumbani no matter what?
Tukimaliza hilo la mashabiki wa mpira. Tujiulize wasanii wa Kimarekani wanaweza kupata listeners wa nyimbo zao kwa mataifa mengi duniani ?Ukiacha kufanya vizuri kwa Simba na Yanga ligi ya Tanzania, sababu nyingine kuu ni kwa vile ni timu za mji mkuu, Dar enzi hizo kila kitu ilikua ni Dar ,
Ahahaaaaah...Mimi ni shabiki kindakindaki wa NEWCASTLE UNITED
MAGPIES
GEORDIES
THE LADS
TOON ARMY
THE CHRONICLES
BLACK AND WHITE PRIDE
Unasemaje kuhusu hilo
Yeah...Kwa kila kizazi huwa team fulani inapata sana washabiki hasa wale ambao walikuwa neutral kipindi hicho kwa kuangalia ubora wake... mfano chelsea miaka ya 2000 mwanzoni, mancity miaka ya 2010, n.k.
Swali zuri sana mkuu..!Good topic halafu why mashabiki wa soka Tanzania wengi wao wapo Simba na Yanga tu?why Simba inapokwenda pale Iringa kucheza na Lipuli bado watajiona kama wako nyumbani,wao mashabiki wa Iringa hawaishabikii timu yao(maana bila Lipuli kuwepo wasingeona hizi timu zikija kwao)why hatuwi kama mashabiki wa UK ambao wanashabikia timu zao za nyumbani no matter what?
Asante sana Broh kwa kuniweka sawa...George Betram naomba nirekebishe kidogo kwa Liverpool.
Liverpool ilipata washabiki wengi miaka ya 70 - 90, kipindi hiki ndicho kipindi ambacho Liverpool ilikuwa na mafanikio makubwa domestically na Europe kwa ujumla, chini ya Bill Shankly, Bob Paisley, Joe Fagan na Kenny Daglish.
Baada ya hapo, Liverpool imeendelea kusafiria huo upepo wa mafanikio mpaka leo hii, impact ya Benitez ilikuwa ndogo sana kuongeza washabiki ukilinganisha na misingi aliyoiweka Bill Shankly.
Nakubaliana na wewe kwa Man United, wamewahi kuwepo kwenye mafanikio chini ya mkongwe Matt Busby, lakini Ferguson ndiye aliyewapa mafanikio kwa kipindi cha 1990s - 2013. Same to Liverpool now, Man United anatembelea upepo wa Fergie leo.
Nini point yangu kuweka hiyo miaka:-
Kutengeneza loyal fans si kitu cha muda mfupi, na wale ambao wanashuhudia mafanikio kwa kipindi cha muda mrefu wanakuja kukaa na hiyo timu kwa kipindi cha muda mrefu kwa sababu inakuwa kama ndoa iliyokaa muda mrefu, hivyo unakuwa unaona hata nikiachana naye naenda wapi.
Arsenal, Chelsea zina washabiki, lakini misingi iliyojengwa kwa washabiki wa Liverpool na Man United ni imara kupita ya Arsenal na Chelsea.
Ndiyo maana ukiangalia asilimia kubwa ya washabiki wa Man City ni wanaotoka Arsenal na Chelsea, au wale wanaonza ushabiki kipindi hiki.
Na kama ghafla City akapoteza utawala wake utaona mashabiki wanarudi walikotoka au kuhamia kwa timu itakayoibuka.
Mpaka sasa Man City bado hajashinda kiasi cha kutengeneza strong bond kati yake na washabiki wake.
Ni kweli washabiki wote ni glory hunters, lakini kwenye hunting inafika sehemu unatengeneza loyalty, na hiyo lazima iwe ya muda mrefu hasa.
Ila BONGO noma sana aisee..!Wana utaratibu usiyoyumba,maamuzi ya haraka,wanatenda haki,wanafanya mambo kiweledi.
Nani ataishangilia ligi na viporo 10?
Acha tuendelee kuenjoy soka la Ulaya tuIla BONGO noma sana aisee..!
Viporo 10..!?
Mmmmh...Tukimaliza hilo la mashabiki wa mpira. Tujiulize wasanii wa Kimarekani wanaweza kupata listeners wa nyimbo zao kwa mataifa mengi duniani ?