Soka la ulaya lilianza kupendwa baada ya kuanza kuonyeshwa kwenye setilite TV na kuanza kuonekana Africa. Kwa EPL timu kubwa zilikuwa ni United, Liverpool, Aston Villa, Nottingham Forest, Westham na Spurs.
Arsenal, Chelsea, na timu nyingi za kawaida zilizokuwa zikitoka nje ya london hazikuwa tishio kabisa, yaani zilikuwa za kawaida kabisa kama ilivyo kwa sasa timu kama New castle, everton,nk.
Ila kwa hapa Africa soka la ulaya hususani england lilikuja kushika wengi mwishoni mwa miaka ya 90 baada ya Arsenal chini ya meneja Arsene wenger kumsajili kiungo/mshambuliaji wa kiNageria Nwanko Kanu, ambaye alivuma sana kwenye mashindano ya Olimpic ya Atalanta mwaka 1996 nchini marekani.
Kwa kifupi, mtu aliyelitangaza soka la uingereza barani Africa kwa kiwango kikubwa ni Nwanko Kanu. Na % kubwa ya mashabiki wa mwanzo wa Arsenal chanzo kikubwa kilikuwa ni Kanu. Nakumbuka kumsikia mtu m1 kwenye kibanda umiza akisema anahamia Pouthmous baada ya kanu kusajiliwa huko akitokea Asernal.
Kwa chelsea, City, nyingine sijui nini kiliwavutia.