Mashabiki wa Yanga wanataka kumpoteza Mayele

kwisha

JF-Expert Member
Joined
Sep 9, 2021
Posts
1,779
Reaction score
4,982
Mayele alivyochukua maamuzi ya kubaki, nilimuona amefanya maamuzi mabaya sana tena sana. Katika watu ambao huwa hawana shukrani ni mashabiki wa Yanga, asubuhi unaweza kuwasaidia ikifika jioni ukikosea kidogo, wanasau mazuri yako yote ambayo umeyafanya.

Mashabiki wa Simba wanaweza kukusema kwa mdomo lakini siyo watu ambao wanafikia hatua ya kukosea adabu. Kwa mantiki hiyo, mashabiki wa Simba wanajielewa zaidi kuliko wa Yanga.

Hata hivyo, nataka niongee swala hili la Mayele, Yanga bado hawana mshambuliaji mzuri kama Mayele. Wala msitishwe na maneno ya watu kuwa Mayele kapotea, ila ninyi ndiyo mnataka kumpoteza kwa kumshambulia na maneno mabaya.

Leo hii kwenye picha za Mayele watu wanajaa kuweka maoni ya matusi, wengine wanamuita garasa, wengine kuwa ni mchoyo na wakati ndiyo halali ya namba 9 kuwa mchoyo.

Wanasahau kwenye 100% ya ubingwa wa Yanga msimu uliyopita, Mayele peke yake kachangia 60%.
 
Sema hizi comments za kwenye social media sio za kuziamini sana kuwa zinatolewa na mashabiki wa timu husika

Zinaweza kuwa ni comments za mashabiki wengine kabisa na sio Wa Yanga ila hatuwezi kukataa ukweli ambao umesemwa

Mayele yuko katika kipindi kibaya kwenye swala la ufungaji kwa sasa
 
Hebu fanya ku edit hiki ulichoandika hapa. Kuna baadhi ya maneno hata hayaeleweki. Sijui ulikuwa unakimbilia wapi!!
 
Chunguza hao mashabiki utagundua ni wa upande gani hizo sarakasi tusha zoea
 
Tafuta msuluhishi Kati yako na Kiswahili, maana mahusiano yenu yanàathiri Sana wasomaji.
 
Kweli mashabiki wa yanga ni mafuta ya taa. Leo hii Mayele wanamtukana? Huyu si ndio anaewachezesha nyoyo wanaume huyu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…