kwisha
JF-Expert Member
- Sep 9, 2021
- 1,779
- 4,982
Mayele alivyochukua maamuzi ya kubaki, nilimuona amefanya maamuzi mabaya sana tena sana. Katika watu ambao huwa hawana shukrani ni mashabiki wa Yanga, asubuhi unaweza kuwasaidia ikifika jioni ukikosea kidogo, wanasau mazuri yako yote ambayo umeyafanya.
Mashabiki wa Simba wanaweza kukusema kwa mdomo lakini siyo watu ambao wanafikia hatua ya kukosea adabu. Kwa mantiki hiyo, mashabiki wa Simba wanajielewa zaidi kuliko wa Yanga.
Hata hivyo, nataka niongee swala hili la Mayele, Yanga bado hawana mshambuliaji mzuri kama Mayele. Wala msitishwe na maneno ya watu kuwa Mayele kapotea, ila ninyi ndiyo mnataka kumpoteza kwa kumshambulia na maneno mabaya.
Leo hii kwenye picha za Mayele watu wanajaa kuweka maoni ya matusi, wengine wanamuita garasa, wengine kuwa ni mchoyo na wakati ndiyo halali ya namba 9 kuwa mchoyo.
Wanasahau kwenye 100% ya ubingwa wa Yanga msimu uliyopita, Mayele peke yake kachangia 60%.