Mashabiki wa Yanga waonesha weledi mkubwa sana kwenye soka letu, wapewe maua yao

Mashabiki wa Yanga waonesha weledi mkubwa sana kwenye soka letu, wapewe maua yao

Timu yetu imetupa mafanikio mengi, nyakati chache kama hizi za kuanguka haziwezi kuondoa heshima na furaha walivyotupatia.
Sasa mbona kelele nyingi mtaani Mara mnalogwa.Sijui uwanja wa Azam hauwafai.Mara TFF,Tena jana msiseme Refa anapemdelea sababu penalt ya kipumbavu mmepewa mkakosa.
 
Mashabiki wa Yanga wana akili timamu. Na hata panapotakiwa kukosoa (penye udhaifu), huwa tunakosoa kwa staha, na pia kwa kujenga hoja!
 
Masau Bwire anauliza: "Mnasema mna kikosi kipana lakini baadhi ya wachezaji wakikosekana mnaanza kulia lia, je mmepanuka wapi nyuma, mbele, katikati au wapi?
 
FB_IMG_17310088003139456.jpg
 
Kalpana njoo utupe pole na kutupongeza kwa kutovurugana na kutuhumiana kama Magoli na Mangungu walivyo toa tuhuma Simba ilipopoteza.
Hongera mtani labda ni wewe tuu nikwambie... ila sehemu zingine mashabiki wa uto ni fujo na balaaa...
 
Ukweli ni kwamba mnajitutumua ili muonekane wastaarabu ila nyie ni wale wale kasoro tarehe...bwahahahhaahh mtupishe huko...
Mmefungwaa na walina asali...mnapumulia tuu kwa ndani
 
Jana baada ya mechi ya Yanga Vs Tabora kumalizika, licha ya timu ya yanga kupoteza mara ya pili mfululizo kwa bao 3-1 tena wakiwa uwanja wa nyumbani, mashabiki wa yanga karibia asilimia 80 walisimama na kuwapigia makofi wachezaji wao kuwapongeza kwa kazi kubwa waliyoifanya.

Hii ni maturity ya hali ya juu sana katika mpira wetu hasa pale hizi timu mbili za mizimu ya nchi zinapofungwa na mashabiki wakaungana na wachezaji wao kuwapongeza kwa kazi nzuri

Yawezekana wameanza kulielewa soka la dunia linavyoenda kuwa kila timu lazima ipitie kipindi kibaya hasa pale inapokuwa imepata mafanikio makubwa msimu wa nyuma yake pamoja na kuwapoteza key players wake. Safu ya ulinzi ya yanga imekumbwa na majeraha pamoja na kadi kiasi cha kumlazimu mwalimu Gamondi awatumie viungo wakabaji na mawinga km mabeki (Aucho, Andambwile na Nkane) jambo linalofanya wapitike kiurahisi kwa kuwa hawana uzoefu wa kutosha kucheza km mabeki

Hiki kitu ndo kinachowakumba hata man city msimu huu wamefungwa mechi nne mfululizo!
Kwahiyo mnataka tuwasaidieje?
 
Mashabiki wa Yanga wana akili timamu. Na hata panapotakiwa kukosoa (penye udhaifu), huwa tunakosoa kwa staha, na pia kwa kujenga hoja!
Etiiew..mna akili..si walisema wenye akili ni wawili tu
 
Back
Top Bottom