Mashabiki wamvaa Irene Paul, wasusia movie zake

Mashabiki wamvaa Irene Paul, wasusia movie zake

warumi

R I P
Joined
May 6, 2013
Posts
16,218
Reaction score
18,440
Baada ya siku kadhaa muigizaji Irene Paul, kupokea Tuzo ya muigizaji bora wa kike mwaka 2015 (TAF) , Msanii huyo amejikuta kwenye wakati mgumu baada ya hivi karibuni kufanyiwa mahojiano na kituo kimoja cha Television, ambapo aliulizwa swali na Mwandishi, ni movie ipi ya Kibongo anayoikubali?

Ndipo msanii huyo alipofunguka bila kumung'unya maneno kuwa sio muangaliaji wa Bongo movie, hivyo hajui chochote. kauli hiyo ilizua tafrani kwa baadhi ya mashabiki zake ambao walimjia juu muigizaji huyo mwenye makeke ya aina yake awapo mbele ya Camera.

Baadhi ya Comments;

# 1: Huyu dada anajisikia sana, hajui kuwa sisi ndio tuliomfanya awe mtu, bila kuigiza nani angemjua apa mjini? Sijapenda kauli yake hata kidogo.

# 2: Najuta kabisa kwanini nilimpigia kura, kama yeye msanii haangalii Bongo movie, sasa sisi tuangalie ili iweje? Atakula jeuri yake mwaka huu, hiyo tuzo ndio ya mwisho.

# 3: Kwanza mie sionagi uigizaji wake zaidi ya kupiga kelele ovyo na kujitutumua kama anataka kukata roho, mimi simkubali huyo dada anajisikia sana.

# 4: Kuna siku nilikutana nae Mlimani nikamuomba kupiga nae picha akaniambia yeye sio Irene Paul nimemfananisha, hata hivyo niliomba tu kupiga nae picha kwa kuwa nilimpenda, jibu alilonipa eti mi msumbufu sana, yeye yupo busy na mambo yake, kweli anatujibu hivyo mashabiki zake? Nilisikia aibu sana kwa kweli aliniaibisha mbele za watu, sitakaa nimpende.

# 5: Kama haangalii kazi wanazofanya wenzie atajuaje changamoto zilizopo kwenye filamu na kuzifanyia kazi? Kauli yake sio nzuri, kwa hiyo anatuona tunaoangalia kazi zao hatuna akili?

# 6: Muongo mkubwa anajishaua tu, anajifanya anafanana na Angelina Jolie na mishavu yake kama panya, simpendi huyo dada.

# 7: Mi namkubali sana irene paul, ila hiyo kauli sio nzuri, ata kama ni kweli aangalii ni bora angefikiria kabla ya kuongea, by the way mi namkubali tu.

#8 : Kwanza hiyo tuzo kapewa kwa uigizaji upi? Mi sijaona anachoigiza zaidi ya kutumia nguvu kuliko akili, kama haangalii Bongo movie anaigiza ili iweje? Basi akaigize Ulaya.

# 9: Huyu dada anajiona mzuri wakati kakomaa kama nazi, kwanza kuigiza hajui, kanichefua sana, tutakua hatuangalii movie zao tuone hizo jeuri watapatia wapi.

# 10: Kwa hiyo kapata Tuzo ndio anajidai kuropoka? Sasa akipata Oscar si ndio ataikana kabisa kuwa yeye sio muigizaji wa Tanzania?
 
Muigizaji irene paul.
 

Attachments

  • 1432975495323.jpg
    1432975495323.jpg
    23.1 KB · Views: 1,687
Jamani binamu si nimesikia umepigwa ban? Nilikua sina raha kabisa bora nimekuona....bila wewe jukwaa haliendi kabia.
Pole zao haters walioshangilia wakidhani umepigwa ban.
 
Mmh ila best umekomaa kwa kweli khaa hapana
 
Mmh ila best umekomaa kwa kweli khaa hapana

Hahahahahaa warumi nilikua sijasoma comments nimechekaje?
Umezitoa wapi hizo? Aisee hivyo sio vichambo ni balaa.
Bora na sisi huku JF.
 
Last edited by a moderator:
Jamani binamu si nimesikia umepigwa ban? Nilikua sina raha kabisa bora nimekuona....bila wewe jukwaa haliendi kabia.
Pole zao haters walioshangilia wakidhani umepigwa ban.

Wataisoma namba, yani apa kama wamenifufua upyaa nianze kazi kwa kasi, kuna watu wanashilikiana kunifanyia fitna, mbona watachora hewani mwaka huu
 
Mhhhhh! Huyu dada ana shape nzuri balaa ila hiyo sura yake hapana kwakweli.Na hiyo picha uliyoweka sasa......

Hahaaaa jamani hyo sura hapana na huo mdomo akijipaka rangi ya mdomo ndo usiseme. Nilivomuona tu nikajisemea hapana.
 
Hahahahahaa warumi nilikua sijasoma comments nimechekaje?
Umezitoa wapi hizo? Aisee hivyo sio vichambo ni balaa.
Bora na sisi huku JF.

Instagram uko uko, yani wamemchambaje hadi nikamuonea ila huruma, ila irene kauzu nyie akaanza kuwajibu
 
Last edited by a moderator:
Jamani hyo sura yake hapana aisee nilimuona nika choka. Hafu ndo anajifanya Angelina Jolie na ile sura.

Jana walimchambaje insta? Alikoma aiseh, nyie kuna watu wamepinda jaman khaa nilikuwa nacheka
 
Jana walimchambaje insta? Alikoma aiseh, nyie kuna watu wamepinda jaman khaa nilikuwa nacheka

Achwabwe kabisa yani ni muigizaji wa movie hafu haangalii. Alikua anategemea nini kujishaua tu anajiona maarufu eeh. Wamkomeshe kabisa.
 
Achwabwe kabisa yani ni muigizaji wa movie hafu haangalii. Alikua anategemea nini kujishaua tu anajiona maarufu eeh. Wamkomeshe kabisa.

Na mimi nikaingia nikamchamba maana nilizidiwa kwa kweli, watu walikuwa wanaporomosha matusi mpaka wakanikosha nikaunga tela
 
Mi nami mmoja wapo lakini sina tuzo ya yeyote kwahiyo am free to say anything! Nasikia tu Wema bonge la Mwigizaji... ukiniwekea dau la US $100 million nitaje movie moja aliyocheza Wema na nikipatia nadaka mpunga; yaani hayo madolali nitayakosa vivi hivi!!

Nimecheka mie maana boti hilo tupo wengi

Mie nilipoangalia zamani hata majina sikumbuki yaani walivyokua wote wanavuta sauti wanaume kwa wanawake kama vile lazima wote waongee hivyo nilichoka, nikakuta sio mimi tu pia kuona hivyo.

Mtu huwezi kusema ndivyo tuongeavyo wanaharibu kutoacha wasanii watumie sauti zao za kawaida...huo mvutooooo sijui wa kabila au eneo gani unaboaaa na nikasepa mie kitambooooooo
 
Huyu irene kweli kachemha hatac aliyoigiza yeye haijui mwigizaji huyu
 
Back
Top Bottom