Tunashindwa hata kumfunga Azam aliyechezeshewa bao mbili na Mbeya City, Sisi tuna akili kweli?
Kwa namna hii ya Uchezaji Mnategemea tungefanya nini jipya kwenye michuano ya Shirikisho CAF?
Gape la alama 10. Mechi 6 zimesalia.
Maana yake Yanga apoteze mechi 3 kati ya hizo 6, halafu Atoe sare game 1, Halafu ashinde 2 tu...Hayo yakitokea ndio Simba tunaweza kuwa Mabingwa.
Ni nani mwenye akili timamu wa kuamini kuwa litaweza kutokea jambo hilo?
Tuna takataka sinazo ng’aa na tunapaswa kuzitupa ili tuwe washindani tena.
Tulichobakisha msimu huu ni kumcheka Mayele tu, Hatuna Jipya la kufanya.