Mashabiki Yanga wampiga ngumi shabiki wa Simba

Mashabiki Yanga wampiga ngumi shabiki wa Simba

[emoji38][emoji38][emoji16][emoji16][emoji38][emoji38]kina waliochomanaga visu Kivule kule miaka km miwili iliyopita wakauana
 
ni kuto jielewa baina ya washabiki wa pande zote sio lazima umtanie mtu kias cha yeye kukasirika mpka akupige na pia sio lazima kupigana mtu kakutanoa umekereka bas ondoka zako kuepusha mambo kama hayo
 
Habari wakuu,

Katika hali inayoonekana si ya kawaida, shabiki mmoja wa Simba ameambulia kichapo kutoka kwa mashabiki wawili wa Yanga jana mnamo saa 2 usiku, pale Keko(Temeke, Dar Es Salaam).

Mashabiki hao awali inasemeka walikuwa wakibishana kawaida tu, ila shabiki wa Simba alionekana kuwatania sana Yanga huku akiwaita majina yanayokera na kuudhi mashabiki hao wa Yanga.

Baada ya muda inasemekana wana Yanga hao uvumilivu uliwashinda ndipo mmoja kati yao alipotoa lugha ya kuonya kurusha ngumi endapo mwana Simba huyo ataendelea na utani. Jambo ambalo lilitimia baada ya shabiki huyo kumpiga ngumi kijana huyo iliyompeleka chini, na ndipo wote wawili hao walionekana kumchangia kwa kumpiga kwa hasira mwana Simba huyo na kutokomea.

Mpaka watu wa pembeni wanaenda kutetea ugomvi huo, tayari yule shabiki alishachakazwa vibaya huku wana Yanga hao wakionekana kukimbia mbio mbali na eneo hilo.

ANGALIZO: Mashabiki kuweni makini na utani wenu, isifikie hatua kama hiyo inayotaka kufikia kwakweli.

Pia kuweni makini na wana Yanga, maana kwa sasa ni kweli wana msongo wa mawazo na wamechanganyikiwa na hali halisi, MSIWATANIE SANA maana siyo vizuri na ni hatari.

Pia mashabiki wa Yanga, jaribuni kuwa na busara za kimichezo, jambo kama hili ni la kipuuzi, hata kama una hasira.
Acha post za Kichochezi
Wewe mwenyewe umeandika kuwa umesikia ina maana umesimuliwa...
Ningekuwa Admin post kama hizi na delete tu
 
Acha post za Kichochezi
Wewe mwenyewe umeandika kuwa umesikia ina maana umesimuliwa...
Ningekuwa Admin post kama hizi na delete tu
Mbona kama una msongo wa mawazo?? Kuna sehemu hapo umeona nimechochea??
 
Yaani nafanya kazi ya kuonya huyu mwamba ananiambia na chochea hivi hii ni akili kweli??
 
Afya ya akili imekuwa changamoto kwa tz..hata ile kusema kat ya watu kumi wawili wana tatizo la afya ya akili naweza kukataa..yawezkana wote kumi wanatatzo sema sample size yao imekuwa jumuish sanaa...wakafanye ivo kwa mashabik wa yanga kama hata mmoja atakuwa mzima...hili lishawahi kusemwa ma msemaj wao aliefungiwq
 
Mkuu Catel mbona umeongea kwa msisitizo sana, [emoji16][emoji16][emoji16][emoji16]
Ina maana yanga ni wagonjwa wa akili au vipi
 
Mkuu Catel mbona umeongea kwa msisitizo sana, [emoji16][emoji16][emoji16][emoji16]
Ina maana yanga ni wagonjwa wa akili au vipi
Kabxaa mkuu....iv ushabik unaweza kukupelekea kujeruhi au kuua kisa tu timu yako haifanyi vzur...hili kwa kwel ni lq kutazamwa kama mama anavyosema...sasa hiv si utani na ushabiki tena...imekuwa ni uhasama
 
Yani na mkae nao mbali baada ya jpili maana mtauliwa kabisaa. Wengine midomo yetu ni humu humu JF.
 
Walipiga mtu pale arusha mpaka akapoteza uhai hakuna hata mmoja aliye paza sauti nguruwe pori akajikausha kama hakijatokea kitu vile
 
Humu JF zingekua zisha pigwa ngumi kuna watu wana matusi na wanakera sana
 
Asee kama mmempiga msela sio poa asee. Halafu unakimbilia hapa Jeiefu
 
Walipiga mtu pale arusha mpaka akapoteza uhai hakuna hata mmoja aliye paza sauti nguruwe pori akajikausha kama hakijatokea kitu vile
Hizi ndio kauli zinazoleta ugomvi unamuita mtu nguruwe pori atavumilia? be smart vitu vingine unatumia uungwana tu
 
Back
Top Bottom