Mashairi ni hapa

Mashairi ni hapa

Dr leader

JF-Expert Member
Joined
Jun 28, 2016
Posts
893
Reaction score
1,021
SHAIRI :: MAKINIKA UTAPATA
JIBU KWA DR SAUL KALIVUBHA ( nitapataje mkamilifu)



1 Yakaribie maziwa, nasaha nitazikupa
Na mikono yako nawa, wala usiwe na pupa
Uwaweza kuchaguwa, ila uwapata dupa
Wakamilifu wapapo, makinika utapata

2 Ukiingia ndoani, ufanye kujihafadhi
Si ujuzi tu chumbani, bali uchunge lafudhi
Usiweke hadharani, shaini lenda kwa kadhi
Wakamilifu wapapo, makinika utapata

3 Itoe yako aibu, utampata kisura
Uende kwa taratibu, muweze kuifanya gura
Mdomo usiwe bubu, msemeze yule Sara
Wakamilifu wapapo, makinika utapata

4 Wamekithiri wabora, waliofundishwa kazi
Punguza wako ukora, utajionea wazi
Kisha na uwe imara, ufuatishe wazazi
Wakamilifu wapapo, makinika utapata

5 Wazuri waona wengi,na kesha walo sifika
Kama Fatuma haringi, ijapo umemruka
Weye ingali ni Kingi, chunga usijipe buka
Wakamilifu wapapo,makinika utapata


[emoji2399]Abuuabdillah[emoji1614]
+255744883353
Arusha -- Tanzania

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Niliitua kalamu, sio juzi wala jana,
Kiwako wataalamu, nasi tungali vijana,
Leo nimeshikwa hamu, kisa ni hii korona.
Si mchezo si dhihaka, tujikinge tuwakinge

Andanenga na ngogomo, na tabora joka kuu,
mlichotupa kisomo, hamkuwa na makuu,
Mlilumba na michomo, udugu uso makuu,
Si mchezo si dhihaka, tujikinge tuwakinge

Nguvumunda na wengine, wengi walotangulia,
Na ya kheri tulingane, pepo kuwafungulia,
Tusidhanie wengine, nani atatangulia?
Si mchezo si dhihaka, tujikinge tuwakinge

Janga limeshatufika, letu sio lake yule,
Kuyadhania mashaka, kwamba yamekoma kule,
Na kujitia wahaka, si yetu ya misukule!
Si mchezo si dhihaka, tujikinge tuwakinge

Na zake kubwa dalili, ni kwenye koo kuwashwa,
Ingine yake dalili, pafu hewa kukaushwa,
Na wala usende mbali, kohozi kavu wahishwa,
Si mchezo si dhihaka, tujikinge tuwakinge

Joto kali ukihisi, usifanye mazoweya,
Kupumua kama ngisi, na maumivu kupeya,
Kichomi kama yabisi, na mwili kukulegeya,
Si mchezo si dhihaka, tujikinge tuwakinge

Haina dawa korona, ila inazuilika,
Haitaki konakona, huku na kule pilika,
Tulia kaya na wana, sijitie hekaheka,
Si mchezo si dhihaka, tujikinge tuwakinge.

Ewe mola wanusuru, nasi pia ikhwani,
Imesomba misururu, pande zote duniani,
Nani wa kutunusuru, kama si yeye Manani?
Si mchezo si dhihaka, tujikinge tuwakinge.

Hapa naweka tamati, kalamu nabwaga chini,
Nimekumbusha umati, nawe umefanya nini?
Ni ya watu sio miti, sijitie majangani,
Si mchezo si dhihaka, tujikinge tuwakinge
Leta na la corona
 
Eeh waah hapa ss tunaongea lugha moja
Ngoja nilisome
 
Back
Top Bottom