Mashairi ya Kitambo Tupia la kwako

Mashairi ya Kitambo Tupia la kwako

Wakulonga

JF-Expert Member
Joined
Oct 29, 2012
Posts
762
Reaction score
771
1. Karudi baba mmoja,
toka safari ya mbali,
Kavimba yote mapaja,
na kutetemeka mwili,
Watoto wake wakaja,
ili kumtaka hali,
Wakataka na kauli iwafae maishani.

2. Akatamka mgonjwa,
ninaumwa kwelikweli,
Hata kama nikichanjwa,
haitoki homa kali,
Roho naona yachinjwa,
kifo kimenikabili,
Semeni niseme nini,
kiwafae maishani.

3. Yakawatoka kinywani,
maneno yenye akili,
Baba yetu wa thamani,
sisi tunataka mali,
Urithi tunatamani,
mali yetu ya halali,
Sema iko wapi mali,
itufae maishani

4. Baba aliye kufani,
akajibu lile swali,
Ninakufa maskini,
baba yenu sina hali,
Neno moja lishikeni,
kama mnataka mali,
Kama mnataka mali,
mtayapata shambani.

5. Wakazidi kumchimba,
baba mwenye homa kali,
Baba yetu watufumba,
hatujui fumbo hili,
akili zetu nyembamba,
hazijajua methali,
Kama tunataka mali,
tutapataje shambani?

6. Kwanza shirikianeni,
nawapa hiyo kauli,
Fanyeni kazi shambani,
mwisho mtapata mali,
haya sasa buriani,
kifo kimeniwasili,
Kama mnataka mali,
mtayapata shambani.

7. Alipokwisha kutaja,
fumbo hili la akili,
Mauti nayo yakaja,
roho ikaacha mwili,
Na watoto kwa umoja,
wakakumbuka kauli,
Kama mnataka mali,
mtayapata shambani.

8. Fumbo wakatafakari,
watoto wale wawili,
wakakata na shauri,
baada ya siku mbili,
wote wakawa tayari,
pori nene kukabili,
Kama mnataka mali,
mtayapata shambani.

9. Wakazipanda shambani,
mbegu nyingi mbalimbali,
tangu zile za mibuni,
hadi zitupazo wali,
na mvua ikaja chini,
wakaona na dalili,
Kama mnataka mali,
mtayapata shambani.

10. Shamba wakapalilia,
bila kupata ajali,
Mavuno yakawajia,
wakafaidi ugali,
Wote wakashangilia,
wakakumbuka kauli,
Kama mnataka mali,
mtayapata shambani.

11. Wakanunua na ng'ombe,
majike kwa mafahali,
wakapata na vikombe,
mashine na baiskeli,
Hawakuitaka pombe,
sababu pombe si mali,
Kama mnataka mali,
mtayapata shambani.

12. Wakaongeza mazao,
na nyumba za matofali,
Pale penye shamba lao,
wakaihubiri mali,
Wakakiweka kibao,
wakaandika kauli...

"KAMA MNATAKA MALI
MTAIPATA SHAMBANI".
🚶🚶🚶🚶🚶🚶

Miaka hiyo tuliimba tu kama kujifurahisha wala hatukujua maana yake, leo twatambua nini maana yake

Nawakumbusha tu
🏃🏾

*BACK IN THE DAYS* 😅🤣
 
Pumzika kwa Amani Mtu wa Malati Nguvumunda.
 
Mimi namtaka mke na mke yuwanitaka,
Hawataki wazazi wake jambo hili kufanyika,
Acha na wangu watete hawataki kadhalika,
Nifanye nini niowe ili nipatetulia?


Tunapendana kwelikweli pendo letu la udhati,
Tumekutana wawili kama wali na kibati,
Wazee wa pande mbili wazidisha mikakati,
Nifanye nini niowe ili nipatetulia?


Hivyo tunavyopendana ajua yeye jalali,
Tukapanga kuoana kwenye ndoa ya halali,
Wazee wapinga sana tena zote pande mbili,
Nifanye nini niowe ili nipatetulia?


Mimi nampenda yeye mfano wa roho yangu,
Akanambia na yeye habadili kuwa wangu,
Kumbe vile hatimaye wazee wanamachungu,
Nifanye nini niowe ili nipatetulia?




Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pole sana mkuu inaonekana hili limegusa kweli kweli mpaka ukaamua utoe ya moyoni
Mimi namtaka mke na mke yuwanitaka,
Hawataki wazazi wake jambo hili kufanyika,
Acha na wangu watete hawataki kadhalika,
Nifanye nini niowe ili nipatetulia?


Tunapendana kwelikweli pendo letu la udhati,
Tumekutana wawili kama wali na kibati,
Wazee wa pande mbili wazidisha mikakati,
Nifanye nini niowe ili nipatetulia?


Hivyo tunavyopendana ajua yeye jalali,
Tukapanga kuoana kwenye ndoa ya halali,
Wazee wapinga sana tena zote pande mbili,
Nifanye nini niowe ili nipatetulia?


Mimi nampenda yeye mfano wa roho yangu,
Akanambia na yeye habadili kuwa wangu,
Kumbe vile hatimaye wazee wanamachungu,
Nifanye nini niowe ili nipatetulia?




Sent using Jamii Forums mobile app
 
Maji na moto

Mimi naitwa moto, sifa zangu mwazijua
Mimi ni mtoa joto, watu nawasaidia
Wazee pia watoto, wanipenda kuzidia
...................

Nimesahau
 
Shairi langu favourite ni la chai "linalokandia" nyumba ndogo/michepuko japo nakumbuka mstari mmoja tu;

Chai ile ya nyumbani, si ile ya hotelini
Nimefanya tathmini,........
 
Shairi langu favourite ni la chai "linalokandia" nyumba ndogo/michepuko japo nakumbuka mstari mmoja tu;

Chai ile ya nyumbani, si ile ya hotelini
Nimefanya tathmini,........
😂😂😂 diffensive mechanism
 
"JIBWA LILOKUNJA KIA NI VIGUMU KULINYOSHA"
Andanenga huyo.
 
1. Karudi baba mmoja,
toka safari ya mbali,
Kavimba yote mapaja,
na kutetemeka mwili,
Watoto wake wakaja,
ili kumtaka hali,
Wakataka na kauli iwafae maishani.

2. Akatamka mgonjwa,
ninaumwa kwelikweli,
Hata kama nikichanjwa,
haitoki homa kali,
Roho naona yachinjwa,
kifo kimenikabili,
Semeni niseme nini,
kiwafae maishani.

3. Yakawatoka kinywani,
maneno yenye akili,
Baba yetu wa thamani,
sisi tunataka mali,
Urithi tunatamani,
mali yetu ya halali,
Sema iko wapi mali,
itufae maishani

4. Baba aliye kufani,
akajibu lile swali,
Ninakufa maskini,
baba yenu sina hali,
Neno moja lishikeni,
kama mnataka mali,
Kama mnataka mali,
mtayapata shambani.

5. Wakazidi kumchimba,
baba mwenye homa kali,
Baba yetu watufumba,
hatujui fumbo hili,
akili zetu nyembamba,
hazijajua methali,
Kama tunataka mali,
tutapataje shambani?

6. Kwanza shirikianeni,
nawapa hiyo kauli,
Fanyeni kazi shambani,
mwisho mtapata mali,
haya sasa buriani,
kifo kimeniwasili,
Kama mnataka mali,
mtayapata shambani.

7. Alipokwisha kutaja,
fumbo hili la akili,
Mauti nayo yakaja,
roho ikaacha mwili,
Na watoto kwa umoja,
wakakumbuka kauli,
Kama mnataka mali,
mtayapata shambani.

8. Fumbo wakatafakari,
watoto wale wawili,
wakakata na shauri,
baada ya siku mbili,
wote wakawa tayari,
pori nene kukabili,
Kama mnataka mali,
mtayapata shambani.

9. Wakazipanda shambani,
mbegu nyingi mbalimbali,
tangu zile za mibuni,
hadi zitupazo wali,
na mvua ikaja chini,
wakaona na dalili,
Kama mnataka mali,
mtayapata shambani.

10. Shamba wakapalilia,
bila kupata ajali,
Mavuno yakawajia,
wakafaidi ugali,
Wote wakashangilia,
wakakumbuka kauli,
Kama mnataka mali,
mtayapata shambani.

11. Wakanunua na ng'ombe,
majike kwa mafahali,
wakapata na vikombe,
mashine na baiskeli,
Hawakuitaka pombe,
sababu pombe si mali,
Kama mnataka mali,
mtayapata shambani.

12. Wakaongeza mazao,
na nyumba za matofali,
Pale penye shamba lao,
wakaihubiri mali,
Wakakiweka kibao,
wakaandika kauli...

"KAMA MNATAKA MALI
MTAIPATA SHAMBANI".
🚶🚶🚶🚶🚶🚶

Miaka hiyo tuliimba tu kama kujifurahisha wala hatukujua maana yake, leo twatambua nini maana yake

Nawakumbusha tu
🏃🏾

*BACK IN THE DAYS* 😅🤣
Mmefanya la maana ujuzi uongezeni, Mali kawapa labana kutoka uko shambani, zakilimo nazo zana nasema ziboreshen, Kama unataka Mali 🇲🇱 mtaipata shambani

Mali ikipatikana hesabu daftarini, kalamu mkitukana Mali si habarini, msije mkakosana urafi kuingieni, Kama unataka Mali mtaipata shambani
 
Vijana naona mzuka wa mashairi kawapanda.
Huo ulimwengu bado uhai japo una changamoto nchini Tanzania.
 
Back
Top Bottom