Herbalist Dr MziziMkavu
Platinum Member
- Feb 3, 2009
- 43,112
- 34,951
kunguru ndege mjanja hafugiki asilani,
hata ukimpa chakula hatotulia nyumbani,
amezowea mizoga inayotupwa jaani,
nilikudhania ndege unaefugika tunduni,
nikakupa cheo na taadhima pamoja na ihsani,
kumbe ni sawa na kunguru rangi yako sio shani,
wapo wenye rangi nyeupe wale wanaoshi pwani,
mwanzo nilikudhania njiwa sana nikakuamini,
sasa nimeshakujua huwezi kutulia abadani,
sasa ruka nenda zako ukweli nimeubaini,
hatuwezi kubaki pamoja tabia hatulingani,
kwa heshima nakuruhusu tena nakupa shukrani.
Ruka nenda kwa wenzako tausi aingie ndani.
Mkuu Mkereketwa_Huyu Mimi sipo kabisa na Siasa zenu za Ki-Tanzania ingawa mimi pia ni M-Tanzania kama wewe lakini sijishughulishi na Siasa za Tanzania mkuu. Hiyo ni shairi tu sio shairi la matusi.Mkuu, mbona naona kama unawatukana CCM moja kwa moja au ndiyo unaona 2015 inachelewa tena?
Mkuu Mkereketwa_Huyu Mimi sipo kabisa na Siasa zenu za Ki-Tanzania ingawa mimi pia ni M-Tanzania kama wewe lakini sijishughulishi na Siasa za Tanzania mkuu. Hiyo ni shairi tu sio shairi la matusi.
Mkuu, mbona naona kama unawatukana CCM moja kwa moja au ndiyo unaona 2015 inachelewa tena?