Mashaka kuhusiana na mchezo wa kubahatisha wa TATU MZUKA unaochezehwa na Zembwela

Mashaka kuhusiana na mchezo wa kubahatisha wa TATU MZUKA unaochezehwa na Zembwela

Freed Freed

JF-Expert Member
Joined
Jun 27, 2017
Posts
6,547
Reaction score
7,167
Huu mchezo ambao mara nyingi nimekuwa nikiutazama ITV umenipa mashaka. Mara nyingi washiriki hupata milioni tano kurudi chini.

Kumbuka hapo Kuna milioni 50, 60 hadi 70.
Cha ajabu watu hawashindi hela hizo nyingi. Jamaa anachokifanya baada ya kufunga mchezo anachomoa vile vibao vyenye hela nyingi akituaminisha watu wameshindwa kubahatisha.

Wasiwasi wangu: Nahisi Kuna USIRI MKUBWA Kati ya Zembwela na Mmiliki wa bahati nasibu ya TATU MZUKA.

Kumbuka kwenye Tv Kuna muda Mwingine huoni ule ubao wenye vibao baada ya washindi kupatikana. Utamwona Zembwela tu akibwabwaja japo kwa muda mfupi sana.

Sasa hapo ndipo bila Shaka Kuna MTU KAANDALIWA kutimiza usanii ili kuvutia watu waendelee kucheza bila kukata tamaa.

Wasalaam.
 
Kama maisha yako ni lazima upambane ndio upate basi achana na michezo ya kubahatisha utalaumu makampuni kila siku na utahisi watu vibaya kumbe ww huna bahati tu
 
Nishaona alieshinda 10m pale pale itv kwahyo usilaumu huna bahati ww pambana upate maisha mwenye bahati hata akicheza mara moja anakula. Mfano nina mfanyakazi wangu chalii tu siku moja kasema ngoja nicheze buku kwenye efm kacheza kwenye saa kumi na nusu hivi saa kumi na mbili kwenye kipindi cha stori kile kala kwanja m3 na ndio mara yake ya kwanza kucheza. Siku inayofuata hakuja kazini na kwa mbwembwe akanipiga na 50k kunipooza 😂😂😂
 
Nina wasiwasi naye, hii michezo Kuna Siri aisee.
i-went-kindergarten.jpg
 
Huu mchezo ambao mara nyingi nimekuwa nikiutazama ITV umenipa mashaka. Mara nyingi washiriki hupata milioni tano kurudi chini.

Kumbuka hapo Kuna milioni 50, 60 hadi 70.
Cha ajabu watu hawashindi hela hizo nyingi. Jamaa anachokifanya baada ya kufunga mchezo anachomoa vile vibao vyenye hela nyingi akituaminisha watu wameshindwa kubahatisha.

Wasiwasi wangu: Nahisi Kuna USIRI MKUBWA Kati ya Zembwela na Mmiliki wa bahati nasibu ya TATU MZUKA.
Kumbuka kwenye Tv Kuna muda Mwingine huoni ule ubao wenye vibao baada ya washindi kupatikana. Utamwona Zembwela tu akibwabwaja japo kwa muda mfupi sana.

Sasa hapo ndipo bila Shaka Kuna MTU KAANDALIWA kutimiza usanii ili kuvutia watu waendelee kucheza bila kukata tamaa.

Wasalaam.
NOTE:
Ule mchezo aurushwi live ko kuna namna wanafanya. Ungekuwa unaenda live hewani apo wangeshikika.. kuna siri kubwa
 
Mimi sijawahi shiriki huo utopolo hata siku Moja na Wala sitokaa nishiriki
 
Watu 1000000*tsh1000=1bn...chukua m400 toa expenses zote +kodi baki m600... Hiyo ndio namna rahisi ya kukusanya pesa kutoka kwa maskini walio desparate kwa maisha magumu... Kumbuka.. Hakuna ataeshinda zaidi ya m15🤣🤣🤣
 
Alafu hii michezo sio ya wazawa, wamiliki wengi ni wahindi na waarabu.
 
Back
Top Bottom