Nikifa MkeWangu Asiolewe
JF-Expert Member
- Feb 26, 2024
- 6,944
- 14,351
Heri kwenu wakuu.
Kwanza nianze Kwa kusema wakuu jibane bane ujenge uwe na kwako.hata kama ni chumba na sebule tu.Ni heshima kubwa mno kwako na hata Kwa demu/mke wako.
Kipindi hicho Sina ramani za maana nilipata chumba Kwa jamaa mmoja Hivi.
Chumba hakikuwa kizuri sana yaani Cha kawaida kulingana na pesa yangu.
Masharti niliyopewa
1:Hakuna kuleta mwanamke/wanawake.
2:Hakuna kupiga mziki Kwa sauti ya juu japo hata bufa sikuwa nayo maskini Mimi.
3:Kuingia ndani mwisho saa3 usiku geti likifungwa lala ulikokuwa.
Hii ndo ilikuwa mwanzo wa kupanga nilijua labda ndo mfumo wenyewe ulivyo unapopanga hivyo sikuwa na maswali.
Ukizingatia nyumba nyingi niliambiwa bei ya juu nikachomoa.
Basi nikaleta godoro langu la kishikaji meza ya mabox
Vyombo vya kuzugia na jiko la mkaa maisha yanaendelea kama kawaida.
Wiki ya kwanza ikaisha ya pili nayo ikakata. Ya tatu nimezoea nikaona huu upuzi huu yaani Nina geto halafu niwe nalipa 10-15k loudge Kwa ajiri ya mwanamke na geto lipo haiwezekani kwakweli hii haipo.
Ilikuwa jpili mapema tu saa3 manzi akaingia geto yeye na familia yake wakiwepo.
Alikuja kupanua napoishi maana siku mingi tangu nimuache kijijn japo haikuwa mbali sana.
Tulikaa nae kama masaa3 -4 Hivi akaaga akaondoka maana aliaga kiaina tu huko kwao.
Kipindi narudi kutoka kumsindikiza nikakuta kakaa mlangoni kakasirika vibaya mno.
Nikafika nataka kuingia ndani. akasema ana mazungumzo namimi.
Akaniambia makubaliano yetu ya awali japo hatukuandikishana nae hayo masharti yake sehemu yoyote Ile.
Nikamwambia wewe umejuaje kuwa huyu ni mchumba wangu au? Unatabia ya kuwa unakuja kutusikilizia na kuchungulia?
Pia Mimi ni mwanaume mkubwa tu Cha ajabu ni kipi kuwa na mwanamke humu ndani mwangu?
Mzee wangu kama umenichoka Wala usiwe na sababu nilipe Hela yangu ilibaki niende nikapange sehemu nyingine nikuachie chumba chako.
Akaanza kuongea muda huo mi Niko ndani navaa niende kitaa nikatoka nikasepa nikamuacha.
Tukakutana mtaani akaniita Tena amekuwa mpole akaniambia kijana mambo hayaendwi hivyo Kuna kuzungumza kijana.
Akasema hofu yangu Mimi ni wale mabinti zangu iwapo utakuwa unabadiri wanawake ni vyepesi sana kurubunika Hawa pia.
Nikamwambia mzee wangu yule binti ni mchumba wangu nyumbani anafahamika na baadhi ya ndg Wanamjua.
Hata yeye kumpeleka loudge angenielewa vingine.
Kuanzia hapo mzee akawa mpole sana nikawa naleta mzigo kama kawaida.
Lile shart la bufa Mimi sikuwa nayo hivyo halikuni athiri Kwa lolote.
Basi lile la kurudi saa3-4 usiku. Nilitii siku chache tu nikamwambia kazi yangu inaniladhimu kuja Kwa kuchelewa naomba funguo Moja mpe dada fln (huyu alikuwa mpangaji mwenzangu alikuwa anauza makongoro kuanzia saa10 jioni Hadi saa1-2 usiku yanakuwa yameisha)
Nilimwambia akakubali kuwa atanifungulia muda wowote nikimuamsha maana alikuwa na mtoto anasoma Kila asbh nilikuwa naenda nae Mimi na kuhakikisha mtoto Nampa buku ama buku2 ya kula shule.
Inshort mtoto alinipenda sana Hadi nikawa nalala nae kwangu maana alikuwa wa kiume.
Nikajipata Kwa kiasi fln nikahamia mji mwingine.
Hapo Sasa ilinibidi niangalie nyumba yenye usalama zaidi
Maana nilinunua vitu mhimu sana na vya gharama Kaisi fln Kwa level yangu
Nilinunua godoro inchi12
Smart tv
Vyombo set kadhaa
Jaba makubwa3
Bufa nk
Hata siku nahamia sikwenda na boda Tena Bali nilikodi canter maana mizigo ilikuwa mingi.
Kwanza nilienda kama nyumba3 nzuri sana ila nauliza swali moja tu kijana umeona? Nami nilijibu Bado sijaoa baada ya kuchemka Kwa nyumba hizo3 basi nikawaza hapa Sasa naenda kukubali nikipata nyumba nyingine nikubali mke ninae kabisaa.
Kweli nikaelekezwa nyumba nyingine Tena hii ilikuwa nzuri sana Kwa mwonekano nikamkuta kijana tu kama Mimi ndo kashaachiwa na mzee wake kushughulika na wapangaji nayeye akiuliza vilevile bila kusita nikamjibu ndio ninae na mtoto1.
Nikaonyeshwa chumba Tena self kikubwa Kizuri nikaomba vitendea kazi nifanye usafi.nikafanya usafi.
Siku nahamia ndo nikapewa vigezo na masharti kama kawaida hatukuandikishana nikakubali yote
Masharti niliyopewa hapa
Kununua ufagio wa nje✓
Kudeki choo Cha Nje (Big no)
Hakuna kuja usiku sana yaani mwisho saa5 (Big no)
Umeme kuchangia 10,000 Kwa mwezi(Big no)
Kutoa Hela ya mfanya usafi wa nyumba nzima(Big no)
Kuchimbisha karo la uchafu (Big no)
Hayo ndo masharti niliyopewa na nililotekeleza ni Moja tu LA kununua ufagio wa Nje yaani 3000
Mengine nilikataa yote la umeme nililipa mwezi mmoja huku namwambia mwenye yumba anitafutie MITA yangu nikiwa nimemuahidi Hela 20k akifanikiwa japo hata hiyo ya MITA ni juu yangu hili alifanikiwa nikawa na Mita yangu.
Kuhusu kufanya usafi choo Cha Nje nikamwambia Mimi sikitumii siwezi
Kuhusu Hela ya usafi na karo nikamwambia ni jukumu lako mwenye nyumba kufanya hivyo maana tunalipia kwenye Kodi ya nyumba. Hapa mkataba ulikuwa wa mwaka mzima nilikuwa nimelipa.
Alileta Dana Dana mwisho akatulia tuli na wengine
wakafata wote wakawa hawalipi akaja mzee mwenyewe akatukalisha kikao nikamwambia vilevile kuwa jambo la usafi mzee wetu hasa kusesa ni jukumu la mwenye nyumba hata karo na choo Hilo Hali mhusu mpangaji.
Akaniuliza kuhusu mke wangu nikamwambia hatuishi pamoja yeye ni askari Police yupo Siginda atakuwa anakuja mara1 Moja.
Ebu dondosha nawewe vigezo na masharti uliyopitia/unayopitia Kwa mwenye nyumba wako.
Leo huyu hapa mfanyakazi mwenzangu kaya kanyaga.