Masharti ya kuwekeza Zanzibar kwa Mtanzania bara na mgeni

Kuna mambo mengine tusiwe tunapayuka tu watu weusi. Zanzibar ni ndogo. Tuache tamaa na uroho. Huku bara ardhi ipo ya kutosha na bado imebaki kuwa unproductive haizalishwi.
Haya yamefanywa kulinda jamii na ustawi wa tamaduni za visiwani zisipotee. Visiwa popote duniani vina taratibu za tofauti.
Ikisemwa tu iachwe kuwa suala la maamuzi ya wananchi wenyewe, wazenji watauza ardhi yao holela kwa ushawishi wa pesa nyingi na kujikuta hawana ardhi na kupoteza kila kitu.
 
Suala la udogo wa ardhi siyo hoja! Hoja hapa ni usawa baina ya wananchi wa pande mbili. Kwa udogo huo huo wangeruhusiwa wachache kupewa kama ambavyo wao wanapewa huku bara na ikiisha si imeisha tu.
Wazanzibari ndio wanataka usawa kwenye muungano huu. Tokea hapo zamani wanataka kuwe na Serikali ya tanganyika na ya Zanzibar na ijuilikane matuizi na mapato yake. Kwa kujifanya wajanja mukaiuwa Tanganyika yenu na nyinyi mukawa Watanzania tu. Wazanzibari wao ni Wanzanziabari na vile vile ni Watanzania. Kwa hio Wazanzinziba kisheria wanayo haki ya kumiliki Ardhi Tanganyika na Zanzibar. Nyini ni watanzania tu, kwa hio hamuna haki ya kumiliki ardhi Zanzibar.
Ni sawa na Uraisi Mzanzibari kisheria anaweza kuwa Raisi wa Zanziba na Tanzania. Lakini Mtangangiyika hawezi kuwa Raisi wa Zanzibar.
Kuondoa utata huo, kwanza irudisheni ile Tanganyika yenu muliyoiuwa kwa ujannja ujanja sio muwalaumu wazanzibari ambao wao tokea mwanzoni ni wawazi kwa hilo
 
Sawa..ila kumtreat mtanzania mwenzao kama mgeni hii ndio haiko fair kabisa..bora wangelegeza kwa mtanzania..huu ndugu wa kwenye majukwaa ipo siku utisha..hakuna anayefurahishwa na haya.

#MaendeleoHayanaChama
 
Watanzania wengi wanakuwa treated kama wageni kufuatia sheria zilizopitwa na wakati. Mfano issue ya Diaspora - mtanzania aliezaliwa, kukulia, kusoma bongo kachepuka kwenda kutafuta maisha nje ya nchi ( ili kufanikisha hili akaomba uraia wa nje) akirejea bongo anakuwa treated kama mgeni na anapoteza haki ya kumiliki assets zote including viwanja vya urithi !!
 
Katiba mpya ndiyo suluhisho! Tayari kuna rasimu ya katiba ya Warioba, tunaweza kuanzia hapo!
 
Kwani Si mlituvamia Na kutuuwa Na kutuibia wenyewe?
 
Katiba mpya ndiyo suluhisho! Tayari kuna rasimu ya katiba ya Warioba, tunaweza kuanzia hapo!

Hakuna cha katiba mpya, muondoe majeshi yenu ya kivamizi Zanzibar Tu , yaishe walau tupumue
 
Hao walioondoka sawa..nazungumiza mtz bara kwenda zenji..hata tofauti na mkenya akienda zenji..sasa huu muungano au upuuzi.

#MaendeleoHayanaChama

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni uwongo kuwa sababu kuu ni kuhofia Wabara wasije wakamaliza ardhi Zanzibar! Kwanza si Wabara wengi wanaotaka kuhama na kununua ardhi kwingine. Kenya ambako siasa za ardhi ni free sana, Watanzania wangapi wamenunua huko? Na kama ni tatizo la Zanzibar kuwa na eneo dogo....mbona visiwa kama Comoro, Madagascar havijanunuliwa vyote na wawekezaji?
 
Huu upumbavu wa akina Nyerere na genge lake ikome , hatuhitaji muungano isiyo na usawa. Kama wanaweza kumiliki ardhi bara kwa kofia ya utanzania kwa nini Wabara isiywe hivyo huko? Hatutaki . Kero kubwa kuliko zote katika muungano huu wa hovyo kabisa. Nilipata kufika nje ya Tanzania ,eti siku inayotambulika kimataifa siyo siku ya uhuru wetu bali ni ile ya Muungano. Watanganyika tuchw ujinge. Waziri aje atuambie hii kero haioni?
 
Hakuna cha katiba mpya, muondoe majeshi yenu ya kivamizi Zanzibar Tu , yaishe walau tupumue
Nadhani jeshi letu ni mchanganyiko wa Watanganyika na Wazanzibari, hivyo wapo pande zote mbili, kwa maana hawajatenganishwa.
 
Nadhani jeshi letu ni mchanganyiko wa Watanganyika na Wazanzibari, hivyo wapo pande zote mbili, kwa maana hawajatenganishwa.

Siku 3 baada ya mavamizi , Tanganyika ilileta jeshi lake rasmi Zanzibar n halijaondoka Tokea wakati ule mpaka leo
 
Siku 3 baada ya mavamizi , Tanganyika ilileta jeshi lake rasmi Zanzibar n halijaondoka Tokea wakati ule mpaka leo
Sawa ni wakati huo! Lakini kwa sasa ni mchanganyiko hata Wazanzibari wapo huku Tanganyika ingawa siyo kwa vikosi vinavyojitegemea!
 
Sawa ni wakati huo! Lakini kwa sasa ni mchanganyiko hata Wazanzibari wapo huku Tanganyika ingawa siyo kwa vikosi vinavyojitegemea!

Hawa Wazanzibari waliomo jeshini hawawashi hawazimi ni mateka wa Nyerere
 
Maneno matamu maneno ya mwenye akili asietanguliza chuki ibarikiwe
 
Mzanzibar anaweza kuwa makamu wa rais au rais anaweza kuwa waziri pia lkn mtanganyika hawezi kuwa rais wa Zanzibar au waziri.....kwaiyo acheni kelele za ardhi.
Mtanganyika hawezi kuwa hata Diwani Zanzibar but uku mzanzibari anashika mpaka Urais
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…