Mussa01Moses
New Member
- Sep 14, 2021
- 1
- 0
MASHAURI KUMI (10) JUU YA UTAWALA BORA TANZANIA
Nawasalimu kwa Salamu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Kwangu mimi uzalendo sio kuvaa bendera, bali ni kufanya mambo anuai kwa ajili ya maendeleo ya taifa na wananchi wake kwa ujumla. Kutokana na chembechembe za Uzalendo zilizonikaa moyoni mwangu, nimeamua nami Kama kijana kuandika yatayonufaisha taifa langu kupitia utawala bora. Wapo watawala au viongozi wanaojitahidi kufanya kazi kwa uweledi na uchungu juu ya maendeleo yetu lakini tukiri wapo pia wengi zaid ambao huturudisha nyuma na kushindwa kupiga hatua ndefu tena Kwa mwendo wa haraka.
Utawala bora ni ule utawala wenye kuleta athari chanya kwenye nyanja tofuati tofuati. Utawala ambao unatizama kwa jicho la moyo ustawi wa raia, kiuchumi, kiutamaduni, kiafya, na kimaendeleo kwa ujumla.
Kutokana na hilo, utaona kwenye mashauri yangu nimeonelea nimege matonge kutoka kila aina ya sahani ili kuhakikisha maendeleo yetu yanafikika kwa kuwa na utawala bora. Zifuatazo Ndio sifa wananchi wanapenda kuziona ziwepo serikalini ili kuibatiza Serikali kufikia kiwango cha utawala bora.
1) ECONOMIES OF SCALE
Tumekuwa tukisikia miongozo ikitolewa kwa mamlaka husika pamoja na Wizara ya Fedha ikipewa maelekezo mazuri kuhusu kuzidisha makusanyo ya mapato hadi kufikia tril 2 kwa mwezi. Hilo ni jambo jema mno kwa mustakbal wa maendeleo ila tunashauri wigo wa wachangiaji pato la taifa uongezeke ili mzigo usiangukie wachache. Njia zipo nyingi kufanikisha hilo, miongoni mwazo ni kuongeza watumiaji wa umeme na gesi. Iwezekanike umeme ufikishwe kwa watumiaji wengi zaid na ile gesi iliyovutwa toka mikoa ya kusini isambazwe majumbani ili watumiaji wawe wachangizi kwenye pato la taifa Kama tunavyolipia LUKU. Trillion 2 kwa mwezi ni kiasi kidogo tukiamua kuzalisha mipango mbadala mingi bila kumuumiza mwananchi. Wachangizi wa taifa wakiwa wengi mno hata wakiwa wanalipa kwa kiasi kidogo basi unaweza ukakusanya zaid ya unachokusanya toka kwa wachache tunaowabana walipe kiasi kikubwa.
Kuongeza wigo wa walipaji husaidia kuondoa mzigo kwa wachache na bado taifa litapata faida zaidi bila kuumiza wananchi. Mathalan tukiwa ni taifa lenye takriban raia milioni 56, kitakwimu watu wanaolipia umeme kwa Tsh 50,000 kwa mwezi hata wakiwa idadi yao ni mil 10, bado hawawezi kufikia pato linalopatikana ikiwa watu mil 40 wakichangia tsh 15,000 tu Kwa kipindi hichohicho
2) SERA ZA TAIFA
Inasikitisha taifa letu akiondoka kiongozi mmoja uoga wa muendelezo wa miradi huwagubika wananchi. Hii inaonesha kuna udhaifu kwenye sera za taifa. Hatujajua tunataka nini au vipaumbele vyetu ni vipi ndani ya kipindi fulani. Aghalab tunaongozwa na atavyoamka kiongozi na hii sio ishara njema kwenye utawala bora. Sera zinamfanya Rais aongoze kufata mpango huo na sio mipango itokee kichwani mwa mtu mmoja. Kama ndani ya familia tu watu hufanya (Shura) mashauriano, vipi kwenye taifa mapendekezo yategemee kichwa cha mtu mmoja. Hilo jambo ni hatari kwa afya ya taifa.
Kutokuwa na sera endelevu za taifa (National Policies) kumefanya gesi itolewe kusini mpaka Dar kwa pesa za ummah katika awamu ya nne Kisha awamu ya tano isiwe na mipango nayo zaid.
3) TUTUMIE RASILIMALI ZETU VEMA
Tanzania ni nchi iliyobarikiwa sana. Kuanzia ardhi yenye rotuba ya kutosha, bahari, maziwa, madini, gesi n.k
Nilisisimka sana siku namuona aliyekuwa Rais wa awamu ya tano Akisema kumegundulika gesi Rukwa inayoweza kuuzwa duniani kwa takribani miaka 20 bila kuisha. Tunasubiria nini kupata faida kwenye hilo?!
Inasikitisha pale mtanzania ambaye hana kazi rasmi anapoulizwa kazi yake hujibu kwa dharau "Andika Mkulima tu". Tuna Karibu asilimia 60 ya ardhi ambayo haijatumika na wizara ya Kilimo haina mpango wowote kabambe wa kuhakikisha ardhi hiyo inawafaidisha wananchi na serikali. Kila atakayezunguuka Tanzania ni shahidi jinsi mapori yalivyo kaa bila mpango madhubuti wa kuingizia taifa pato. Tungetegemea wataalamu wa ardhi na kilimo wangeshirikiana kushauri maeneo yote ya nchi yatumike kuingizia utajiri wananchi na taifa kwa sera njema za kilimo kushirkiana na halmashauri husika. Taifa letu lina uwezo wa kulima bila kutegemea msimu wa mvua kwa kutumia maziwa yaliyozunguuka. Mipango mema itakayofanywa itaamsha ustawi wa jamii vijijini na kushawishi watu kupungua mijini.
Serikali isione uzito kuingiza fedha Kiasi kwenye jamii kwa ajili ya kuja kukusanya zaid. Mfano, kama watalipa wataalamu watafiti kupitia maeneo yote ili kuelekeza jamii ubora wa ardhi husika na Aina ya zao la mkakati litakalokuwa bora kulimwa hapo. Napongeza Serikali kugawa miche ya mikorosho kwenye mashamba tofuati tofuati kwenye taifa zima ili tuje kupata faida kubwa zaid baada ya kipindi fulani. Usiishie kwenye mikorosho, Njombe pekee imeingiza bil 12 kwenye pato la taifa mwaka jana. Vipi tukiwekeza zaid katika maeneo mengi zaid na Serikali kuvuta maji ya maziwa Kama Nyasa, Tanganyika au Victoria kufika maeneo yanayohitajika kwa kilimo zaid
4) SIASA/DIPLOMASIA NJEMA KWA MATAIFA YA NJE
Tumefundishwa toka utotoni kuwa kilimo ni uti wa mgongo wa taifa lakini watu wasiposaidiwa na serikali kutafutiwa masoko nje basi kilimo chetu kitaendelea kutoonesha tija. Hili linatakiwa lipatikane kupitia uhusiano wetu mwema na mataifa 'makubwa'. Mataifa hayo yanahitaji bidhaa nyingi za kilimo toka kwetu, tukituliza akili tutaruka kwa kasi ya ajabu.
5) WAWEKEZAJI WAHAKIKISHIWE USALAMA WAO NA WA MIKATABA YAO
Vijana wahangaikaji tunajitahidi sana kuvuta wawekezaji kutokana na kukosa uwezo wa kujiendesha pale tunapoona fursa lakini wengi wao wanaogopa kwa kukosekana uhakika wa muendelezo wa mikataba yao kwa siku za usoni. Fikiria unajitahid kumvuta mwekezaji mpaka hapa na Mashine zake kisha anaanza kusumbuliwa na urasimu au kisiasa ili Waziri fulani aonekane kwenye luninga anafanya kazi kwa jinsi anavyokaripia wengine. Anamfukuza bila kusikiliza na kufikiria njia mbadala za kuokoa kazi za wengi walioajiriwa kwenye kiwanda husika.
Mwekezaji mwengine anakwambia kama bilionea mkubwa katika nchi yenu anapotea kusipojulikana kwa siku 9, mie nitamuhakikishiaje usalama wake yeye mwengine akija! Maswala Kama haya yanachafua na kuharibu maendeleo yetu. Sasa ili umvute mwekezaji inabidi achukue dhamana kwa Benki ya Dunia jambo ambalo linaongeza ugumu wa kazi.
Kutoweza kuhakikisha usalama wa raia na wawekezaji sio katika sifa za utawala bora.
6) kuhakikisha bidhaa zote zinazohitajika kilazima kila siku na wananchi zinapatikana kwa bei rahisi mno.
Sukari, unga, mchele, mafuta, saruji n.k ni bidhaa ambazo zinatumika kila kukicha na wanafamilia wa kitanzania. Na imani tumezungukwa na watu waerevu na wenye ustadi mkubwa. Hapa nitashauri moja Kwa moja kwa mama kwani ukiacha majukumu yake ya kiutawala anauchungu wa malezi ya mama kwa wananchi wake. Kuwahurumia raia ni sifa adhim katika utawala bora.
7) sheria kali zitungwe dhidi ya wahujumu Uchumi na mafisadi
Tunafaham sheria kali haziwekwi ili kukomoa bali kuzuia tatizo. Saudia ni taifa unaweza ukaacha duka lako wazi ukaenda msikitin na asiichukue mtu kitu bila kulipa. Sheria yao ya kukata mkono mwizi haiwafanyi wawe na raia wengi wenye mikono butu bali wizi unaondoka. Sawa na China kuua Waziri atakayekutwa katumia ofisi kwa maslahi binafsi, adhabu yao ya kifo ni kubwa mno hadi inatisha lakini imechangia taifa lao kupiga hatua kubwa kiuchumi.
Katika sheria za kutungwa tungependa kuona wabunge wanaandaa mikutano kwa wananchi wao majimboni ili wasaidie kutatua kero kila baada ya kipindi kifupi.
Viongozi wajue kujitathmini iwe kwa kushurutishwa ama la. Waliomtuma mbunge wana haki ya kujua kipya kilichofanywa na mjumbe wao Kwa kipindi fulani. Waziri ajiulize siku hiyo aliyoenda kazini ametekeleza au kubuni lipi jipya Kwa ajili ya maendeleo ya wananchi
Mikataba iwe wazi kabla ya kusainiwa na atakaegundulika kuhusika kujinufaisha binafsi tokana na mkataba wa taifa awajibishwe ipasavyo kwa mujibu wa Sheria hizo Kali. Utawala bora hauishii kwenye kutumbuliwa kiongozi na watu wakashangilia tu.
8) Mtaala wa elimu ubadilishwe na umri wa kustaafu upunguzwe ili wazee wapumzike mapema na vijana waingie kwenye kundi la Waajiriwa.
Elimu inayofundisha tumetoka kwa masokwe haitusaidii kitu chochote hata kama imemfanya waziri kuitwa profesa. Tunataka mtaala utakaogundua vipaji na uwezo wa kazi wa watu. Mtaala utakao muandaa mtoto kimaadili na atoke akiwa na elimu kubwa ya kilimo na ufundi wa aina zote. Kuwezeshwa kwa wahitimu wa vyuo vya ufundi zaidi kwani wengi wao hawatembei na bahasha kuhangaikia kazi baada ya kuhitimu masomo.
Tusione aibu kujifunza toka mataifa yaliyotuzidi kama Japan ambapo kuanzia darasa la kwanza mpaka la nne hawafanyi mitihani Ila wanafunzi wanajua kutengeza calculators (vikokotozi) na Wamejazwa nidhamu.
Kiufupi nyenzo zote zitakaoandaa watawala bora basi zinatakiwa kufanyiwa kazi kuanzia kwenye elimu ya msingi.
9) KUEPUKA KUSIFIWA NA WANAOJIPENDEKEZA ILI WAPATE VITU VINONO
mtawala bora asikubali kuzunguukwa na Washirikina/watazamiaji nyota au viongozi wa dini ambao ukiwapa dakika 10 wakushauri, basi watatumia dk 9 na nusu kukusifu tu ili uwaone. Hofia sana kukubali kusifiwa mbele yako au mtu akiona kamera. Watanzania wanapenda kwenda na upepo. Most of them are opportunists. Tuogope sana
10) Kumuamini Mwenyezi Mungu Mmoja tu na dua zielekee kwake tu. Ni YEYE tu mwenye uweza wa kila kitu. Bila Yeye hatuwezi kufanya utawala ukawa bora. Kumuogopa Yeye kutafanya mtawala aishi kwa mipaka na kuhofia kumbe nae atakuja kuulizwa kwa aliyoyasimamia.
.ahsante.
Kijana wenu
MUSSA Moses
0712216745
Kibaha

Upvote
0