Pre GE2025 Masheikh 12 waliochiwa na mahakama kutokana na tuhuma za ugaidi Machi 4 wakamatwa tena na kurudishwa gerezani!

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Hapo utakuta kesi ya ugaidi walikosa ushahidi wakaamua kusema hawana nia ya kuendelea na shauri ili waachiwe huru na wakamatwe kwa kufunguliwa mashtaka mapya hapo usikute wamefunguliwa kosa la uchochezi
 
Yani wamesota gerezani miaka 10 yote hiyo inamaana waliwatoa wa nini kama wana mashaka nao..
Huo ni ujinga wapewe haki zao.
 
Wakuu, mambo yameamka huku

====

Jana Machi 4, 2025 Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam chini ya Jaji Kirekiano iliwaachia huru MASHEIKH 12, walio kaa gerezani miaka 10, kwa tuhuma za Ugaidi.

Baada ya hukumu hiyo Shura ya Maimamu Tanzania ilitoa taarifa ya kuachiwa huru Masheikh hao.

Wakati taarifa hiyo ikitolewa Masheikh hao walikua wako chini ya itifaki za watu wa usalama na ndugu walitakiwa kwenda kituo cha Polisi cha stakishari kwaajili ya kukamilisha itifaki hizo.

Hata hivyo majira ya magharibi ndugu walipofika stakishari waliambiwa masheikh hao hawajafikishwa pale.

Aidha leo asubuhi ndipo zilipopatikana taarifa kuwa ndugu Masheikh hao wapo katika gereza la Ukonga walilpokuwapo awali.

Ni wazi baada ya Mahakama kuwaachia huru Masheikh hao, watu wa usalama walitumia mbinu mbalimbali wakafanikiwa kuwakamata tena na kuwafungulia mashtaka mapya bila ya ndugu zao kufahamu.

Kwa hakika tukio hili linadhihirisha jinsi ambavyo serikali iliyopo madarakani isivyojali haki za binadamu. Watu hawa wamekamatwa toka 2015, mpaka leo serikali imeshindwa kuthibitisha tuhuma dhidi yao lakini inaendelea kuwanyima haki za msingi na kuwatesa.

Pia soma: Pre GE2025 - Masheikh 12, waliokaa gerezani miaka 10, kwa tuhuma za Ugaidi waachiwa huru

Katika taarifa ya jana tumeeleza madhila yaliyowakuta baadhi yao ikiwa ni pamoja na kupoteza wenziwao na wengine kufia gerezani.

Hivi viongozi wetu wanashindwa kuvihoji vyombo vyao juu ya matukio haya yaliyo kinyume na sheria na utu.

Hivi inaingia akilini mzee Sleiman Ulatule miaka 90, achukue familia yake ya zaidi ya watu 7, waende kuvamia kituo cha polisi?

Katika wasifu huo watawala watakua na uso gani wa kusimama mbele ya wananchi wakiwemo Waislamu kuwaomba ridhaa ya kuongoza nchi.

Ni zuzu wa kiasi gani atakayewapa ridhaa watawala wasio zingatia haki za binadamu, uhuru na haki za kuishi zinazolindwa na Katiba ya nchi.

Aidha tutumie fursa hii kuwaomba Waislamu wote nchini kutumia fursa hii ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani kuomba dua makhsusi na kumkabidhi Mwenyezi Mungu Mtukufu atoe hukumu kwa haya wanayotendewa wanyonge nchini Tanzania.

Atakayeacha kuomba dua hii maana yake ameridhia haya wanayotendewa binadamu wenzake wasio na hatia yoyote.

Shura ya Maimamu Tanzania

Hii mbaya sana aisee, bora wasinge raise hope zao, hii mbaya sana ndugu zangu!
 
watu wana tuhuma za ugaidi, na shura ya maimamu inawatetea. tuweke conclusion gani hapo?
TUhuma umuweke ndani miaka 15 bila ya conviction ina make sense? Na wewe ukituhumiwa uwekwe ndani bila ya hukumu ya mahakama?
 
What are you insinuating? Kwamba Shura ya Maimam nao ni magaidi au walikuwa part and parcel ya huo ugaidi uliowasababisha hao maimam kuwa gerezani?
Whatever it is, miaka yote hiyo how come jamaa hao bado ni remandees? Ni upelelezi gani wa miaka 10?
kwamba sijawahi kuona wakilaani ugaidi, ila wale ambao evidence zinaonyesha ni magaidi huwa wanatetewa na hii shura, wale wenye misimamo mikali ya kigaidi kama kina Ponda, shura hii huwa inawatetea. hakuna asiyejua yale waliyoyatenda hao watu waliopo gerezani tangu enzi za kikwete ambaye ni muislam mwenzao, na hata sasaivi samia ni muislam, wangekuwa wakristo watupu mngesema pengine mmeonewa, ila hata waislam wenzenu wanajua hiki hawa watu wanafanya, mambo ya kibiti, amboni tanga na mtwara, ulishawahi kusikia shura ya maimam ikilaani hata siku moja vitendo hivyo? kama jibu ni siyo, kwa nini tusiamini kwamba na wao wanasapoti ugaidi?
 
Mzee ulivokutana na zile tuhuma za kubakwa,unataka yule aliyetuhumiwa kukuingilia kinguvu asitetewe?........Si ndio maaa Kuna mahakama kuthibitisha uhalali wa makosa?
sasa wewe ndio maana huwa tunasema hata funga yenu ni takataka tu haiwabadilishi mioyo, umeandika uchafu gani huu sasa ndugu gaidi?
 
Serikali ishikilie hapo hapo. Hakuna kuachia hao magaidi.
 
Kinachoshangaza ni Shura ya Maimamu pekee ndiyo wanapaza sauti. BAKWATA wenyewe wako busy na dua ya kumuombea Mama ili aishi milele.
Bakwata ni chombo cha cha serikali kinachotumia jina dini ya kiislam Bakwata haikuwekwa na Waislam imeanzishwa na Serikali kwa chochote kitakacho fanywa na serikali Bakwata haiwezi kupinga chochote .Bakwta inafuata mkia iko nyuma ya Serikali.
 
Wakuu, mambo yameamka huku

====

Jana Machi 4, 2025 Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam chini ya Jaji Kirekiano iliwaachia huru MASHEIKH 12, walio kaa gerezani miaka 10, kwa tuhuma za Ugaidi.

Baada ya hukumu hiyo Shura ya Maimamu Tanzania ilitoa taarifa ya kuachiwa huru Masheikh hao.

Wakati taarifa hiyo ikitolewa Masheikh hao walikua wako chini ya itifaki za watu wa usalama na ndugu walitakiwa kwenda kituo cha Polisi cha stakishari kwaajili ya kukamilisha itifaki hizo.

Hata hivyo majira ya magharibi ndugu walipofika stakishari waliambiwa masheikh hao hawajafikishwa pale.

Aidha leo asubuhi ndipo zilipopatikana taarifa kuwa ndugu Masheikh hao wapo katika gereza la Ukonga walilpokuwapo awali.

Ni wazi baada ya Mahakama kuwaachia huru Masheikh hao, watu wa usalama walitumia mbinu mbalimbali wakafanikiwa kuwakamata tena na kuwafungulia mashtaka mapya bila ya ndugu zao kufahamu.

Kwa hakika tukio hili linadhihirisha jinsi ambavyo serikali iliyopo madarakani isivyojali haki za binadamu. Watu hawa wamekamatwa toka 2015, mpaka leo serikali imeshindwa kuthibitisha tuhuma dhidi yao lakini inaendelea kuwanyima haki za msingi na kuwatesa.

Pia soma: Pre GE2025 - Masheikh 12, waliokaa gerezani miaka 10, kwa tuhuma za Ugaidi waachiwa huru

Katika taarifa ya jana tumeeleza madhila yaliyowakuta baadhi yao ikiwa ni pamoja na kupoteza wenziwao na wengine kufia gerezani.

Hivi viongozi wetu wanashindwa kuvihoji vyombo vyao juu ya matukio haya yaliyo kinyume na sheria na utu.

Hivi inaingia akilini mzee Sleiman Ulatule miaka 90, achukue familia yake ya zaidi ya watu 7, waende kuvamia kituo cha polisi?

Katika wasifu huo watawala watakua na uso gani wa kusimama mbele ya wananchi wakiwemo Waislamu kuwaomba ridhaa ya kuongoza nchi.

Ni zuzu wa kiasi gani atakayewapa ridhaa watawala wasio zingatia haki za binadamu, uhuru na haki za kuishi zinazolindwa na Katiba ya nchi.

Aidha tutumie fursa hii kuwaomba Waislamu wote nchini kutumia fursa hii ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani kuomba dua makhsusi na kumkabidhi Mwenyezi Mungu Mtukufu atoe hukumu kwa haya wanayotendewa wanyonge nchini Tanzania.

Atakayeacha kuomba dua hii maana yake ameridhia haya wanayotendewa binadamu wenzake wasio na hatia yoyote.

Shura ya Maimamu Tanzania

Kwanini wamekamatwa tena?Kuna wakati tunajizima data. Kupanga uhalifu au kutekeleza uhalifu sio misingiya dini ya aina yoyote.

Hakuna dini ambayo waumini wake wamepewa ruksa ya kudhuru waumini wa dini nyingine.
 
Back
Top Bottom