Ipo hv mkuu, uzuri nilikuwepo unguja kipindi sakasaka hili linatokea, masheikh wa miadhara (uhamsho) wao walikuwa na ajenda yao kubwa ya kuamsha wazanzibar waliolala juu ya swala zima la nchi yao, wao kipindi wapo walikua wanawakumbusha wazanzibar kuwa si ccm wala chadema wala cuf itakayowakomboa kutoka kwenye maisha ya dhiki bali ni kufata mwenendo wa quraan na sunna za mtume.
Hawa masheikh hawakuvutiwa na cuf wala chadema wao walikuwa na sera yao kuwa demokrasia ni ukafiri ndio maana kila walipokuta bendera ya cuf au ccm wao walikua wakizishusha na kupandisha zao ambazo zina rangi nyeupe tupu na maandishi meupe kati yaliyosomeka kwa kiarabu hakuna mola anaepaswa kuabudiwa kwa haki isipokuwa Allah na muhammad ni mjumbe wa mwenyezi mungu, wao wao walikuwa wanaamini kuwa kwa umoja wao basi walikua na uwezo wa kuiforce serikali ya ccm kutoka madarakani na wao kuchukua mamlaka kamili, nakumbuka wakati huo mambo mengi yalijitokeza wanawake waliovaaa nusu uchi walipigwa fimbo sn mitaani na vijana wafuasi wa uhamsho, walipinga sn siasa ndani ya zanzibar maana wao hawakuwa na chama, wakawa wanadamana kudai mamlaka kamili ndiipo serikali iliposhtuka na kuona hawa watu wakiachiwa mambo yataharibika Muda si mrefu ndio ikabidi wakamatwe.
Na ndio wakati huo huo viongozi baadhi wa makundi ya kijihad waliwakebehi uhamsho kwa style yao ya kutaka utawala utolewe na kuuita style za kizamni bimana kwenye uislam hakuna maandamano , hvy walitakiwa washike silaha na kuutoa udhalimu. Note sina uhakika sn inavyosemekana kukamaktwa kwa wale watu agizo lilitoka marekani na kusema hao watu ni htr sn hvy wakamatwe kwa makosa ya ugaidi wapo wanaodai kuna viongozi wa uhamsho walifanya training kandahar, na wakati huo raia wa kigeni huko zenji kipindi cha uhamsho walikutwa na madhira mengi sn like kumwagiwa tindi kali na kufanyiwa vitendo visivyofaa. hayo ndio yaliyowasibu uhamsho hadi leo America wanatazama kwa jicho la mwewe if watatoka au laa kesi ngumu.