Mashimo ya Choo yasiyojaa ni kama yako Over-Charged hivi

Mimi nitengeneza hizi system, huyu anaesema ni cheap namshangaa.

Gharama yangu ni kati ya 2m-2.5m kulingana na mazingira yalivyo. Kunawakati ukikosea kustudy site hiyo hela inakata najikuta natumia gharama zangu. Hapa jf kila mtu anajifanya mjuaji
Ungeweka mchanganuo wa hiyo 2m-2.5m inavyotumika materials + ufundi ili watu tukuelewe.
 
Hu
Mimi nitengeneza hizi system, huyu anaesema ni cheap namshangaa.

Gharama yangu ni kati ya 2m-2.5m kulingana na mazingira yalivyo. Kunawakati ukikosea kustudy site hiyo hela inakata najikuta natumia gharama zangu. Hapa jf kila mtu anajifanya mjuaji
Hujatuelezea kitaalamu kama mwana jf.
 
Mkuu niunganishe na fundi na mimi ninunue vifaa aje anitengenezee nimlipe ufundi...
 
kwan hayajai? ni wanakwambia yana tofali za kuruhusu maj kupenya na wengine wanasema wanapandikiz bacteria kula kimyes.ila bei ndio nashangaaaga sana mana material ni hay haya bomba ya nchi 6,mawe,cement
 
Eti taka zinageuka wadudu. Kumbe hadi wakati huu kuna watu wanaamini spontaneous generation theory ya aristotle?
 
Daah 89 hadi leo si wanasema ni ya kileo/kisasa? Kumbe tangu zamani yalikuwako? Asante kwa ushuhuda.
Wapo mafundi wataalamu mitaani wanaoielewa vyema taaluma hii ya ujenzi ili shimo lisiweze kujaa lakini enzi hizi mashimo haya yamepewa jina jipya na labda utaalamu umeongezewa ubora kidogo.
 
Haya mashimo inategemeana!

Mfano sehemu kama dar changamoto za mashimo kujaa maji ni kubwa sana kwa sababu shemu kubwa ni za maji maji yani ukichimba futi 12 tu tayari unakutana na maji ndio maana hii teknolijia mpya watainyaka sana watu wa dar maana ndio wenye changamoto nyingi za mashimo kujaa!

Lakini hata haya mashimo ya kawaida kama upo sehemu ya udongo mkavu usio na chemchemi ya maji unaweza kukaa nalo hata miaka 30 solijae kabisa.

Anacho kifanya fundi wakati wa kulijenga anaacha nafasi baina ya tofali na tofali kila baada ya hatua kadhaa! Zile nafasi ndio zitakazokuwa zinawezesha maji kutorokea ardhini ila ule uchafu mgumu unaendelelea kubaki huku ukioza. Nafikiri waliokaa vijiji mashaidi vile vyoo vya mashimo ya kuchungulia vilikuwa mpaka miti inaoza ndio mnabadilisha shimo lingine.

Kinachofanya shimo la choo kujaa ni yale maji ndio maana hata wakija kunyonya huwa kwenye lile bomba la kunyonyea wanaweka kama chujio na hivyo wanaondoka na maji tupu huku taka ngumu zikibaki humo humo shimoni. Ndio maana kama upo sehemu isiyo na changamoto ya chemchemi za maji haya mashimo ya kawaida utakaa nayo milele ili mradi fundi wako akuwekee mfumo wa kuwezesha maji kutoroka na hatakiwi kulisakafia.

Ama kwa upande wa haya mashimo ya kisasa kuna jamaa huku mtaani kwetu kuna changamoto ya mvua ikinyesha zinaota chemchemi nyingi na hivyo alikuwa na chngamoto ya kuvuta kila mwka ila toka ajenge hilo shimo la kisasa huu ni mwka wa tatu hajavuta.
 
na hatakiwi kulisakafia
Nimebuni aina fulani ya mashimo ya vyoo (septic tank za kisasa). Aina hiyo inatumika kwenye ngazi ya familia na kwenye jamii. Kitu cha kwanza kwenye mashimo hayo ni kusakafia kwa zege, na kuhakikisha hakuna tone la maji linaloingia wala kutoka, isipokuwa pale tu ilipokusudiwa. Ufanisi wa matenki hayo ni mkubwa sana.
 
Wizi mtupu sema wabongo wanaponzwa na ule utengenezani wanavyoremba pale juu na kulifukia lisionekane lakini kujaa linajaa sema yale maji wanayotoa kwenye choo kuelekea kwenye mawe ndio yanakoishia maana yale mawe yanafyonza maji. Na inategemea na sehemu (ardhi) hapa ununio baari beach ninapoishi walichimba hivyo haifika mwaka saa hivi ni dimbwi hakuna cha yale mawe wala choo kote kumejaa ni dimbwi..
Ngoja nikufundishe kinachofanyika pale.
Lile choo linachuja mzigo(nya)na bomba (pvc)linalotoka kwenye choo (septick tank)linaelekezwa sehemu ambayo wamechimba mtaro kama wenge upana wa 5×15 na urefu wa 2mtrs kwenda chini alafu wanapanga mawe yanajaa hadi juu kidogo wanaacha kama urefu wa 2 ft kujaa usawa wa ardhi wanafunika yale mawe kwa nylon (ili maji ya juu mvua ikinyesha yasiingie kwenye hayo mawe)alafu wanafunika kwa udongo.(yalw mawe hayapati udongo kabisa)hapo sasa lile joto la mawe kule chini halipati kwa kuhemea hivyo maji yakiingia pale maana mawe yana kiu ndio mawe yanameza maji taka yako.
Hiyo ndio sayansi wanayosema eti choo cha kisasa kisichojaa[emoji2][emoji2]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Dah[emoji1787][emoji1787]
 
Sasa anazuiaje maji ya pembeni kuingia ndani na kulifanya lijae??
Yaan akama anaacha upenyo maji yatoke nje, si upenyo huo unaweza kufanya maji ya nje yakaingia ndani likawa linajaa haraka zaidi?
 
Na haya ndio maelezo yako yakiwa katika picha,



 
Sasa anazuiaje maji ya pembeni kuingia ndani na kulifanya lijae??
Yaan akama anaacha upenyo maji yatoke nje, si upenyo huo unaweza kufanya maji ya nje yakaingia ndani likawa linajaa haraka zaidi?
Hapana hiyo ni kwa ajli ya sehemu ambazo hazina historia ya chemchemi za maji
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]Jf ni zaidi ya chuo aisee!
 
Dah[emoji1787][emoji1787]
Ulitaka kupatia ila hujaelewa kinacha fanyika. Mawe hayanyonyi maji ni arhi pekee ndio hufanya kazi hiyo, sehemu zenye mfinyanzi ni Bora uchimbe shimo kubwa kuliko kuweka ring,tatizo mnakutana na mafundi wenye tamaa badala ya kutoa ushauri kabla ya makubaliano ya kazi. Mbezi arthi si rafiki kwa mashimo hayo.
 
Mafundi hawatoi ushauri ili wapige pesa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…