Mashimo ya Choo yasiyojaa ni kama yako Over-Charged hivi

Daah 89 hadi leo si wanasema ni ya kileo/kisasa? Kumbe tangu zamani yalikuwako? Asante kwa ushuhuda.
Kuna uwezekano mtu akaishi leo lakini ana vision ya miaka 25 ijayo.

Hapo ndio utajua Knowledge is power.
 
Nipe hiyo kazi, Mimi ni fundi wa hayo mambo.
 
Haya ndio mashimo mazuri sasa na yanaweza kukaa muda mrefu na kipindi cha masika hayataweza kusumbua kabisa
 
Kaka naomba connection na uyo fundi wako tuyajenge
 
Gharama zipoje
 
Gharama
Hellow atariii
 
Wanatoaga hata ya Miaka mitano, but je Guarantee hiyo ni "Legal Binded"?? Au ndio kuanza kuanzisha kusumbuana kwengine?
Sasa kama wana uhakika kwamba hayatajaa kwa nini tena watoe guarantee ya miaka mitano?
 
Hivi kwa kulinganisha haya mashimo ya kawaida kwa sasa ujenzi wake unaweza kugharimu kiasi gani ili kuhalalisha bajeti ya 2m na zaidi kwa kujenga haya mashimo ya kisasa?
 
mimi ni wewe kabisa,ndo vitu vyangu hivyo.
 
Ukitaka karo la majitaka lisijae wewe ukishachimba hakkkisha kuta zake zina matundu kunyonya maji na toboa sakafu yake matundu madogo madogo maji yapige kisha huko shimoni wshusha kiroba cha chokaa na chumvi.
Miaka 100 halijai

Mimi nina mwaka wa 20 huu hata nusu halijafika
 
Baada ya kufuatilia hii mada nimegundua mambo haya.

1. Hii technologia ya uchimbaji wa 'mashimo yasiyojaa', hapa imeelezwa kwa namna tatu tofauti pasipo wachangiaji wengi kujua. Kuna mashimo ya:
-mashimo mawili tofauti ya zege
-Shimo moja la zege na Kupanga mawe
-Shimo moja la kupanga vitofali vyenye nafasi.

2. Teknolojia zote za huo uchimbaji hazifanani, na zote ni sayansi yenye ufanisi tofauti, gharama za material hazifanani.

3. Ukubwa wa gharama za uchimbaji zimejificha kwenye siri ya ujuzi wa fundi na nguvu ya soko na sio kwenye material. Mafundi wengi wakijua kuifanya hii kazi ni wazi huenda gharama zitapungua kwa karibu ya nusu.

4. Sio kila mtindo wa uchimbaji huu wa haya mashimo unafaa kwa kila mazingira au ukawa na matokeo sawa sawa kwenye mazingira yote. Kila kitu kiko tofauti.

5. Neno '.....yasiyojaa' huenda linapotosha, nadhani ilipaswa iwe "....yasiyojaa kwa haraka/urahisi"
 
Hivi kwa kulinganisha haya mashimo ya kawaida kwa sasa ujenzi wake unaweza kugharimu kiasi gani ili kuhalalisha bajeti ya 2m na zaidi kwa kujenga haya mashimo ya kisasa?
Mashimo hayo yalikuepo toka miaka ya nyuma isipokua jamii haikuyaona umuhimu wake kwa sababu idadi ya watu ilikua ndogo na maeneo yalikua mkubwa sasa watu wameongezeka na maeneo yamepungua badala ya kujenga mashimo ya kunyonya tunageukia hayo yasiyonyonywa tahadhari kwa mabosi wawe makini na mafundi maana ukimchukua fundi kishoka utajuta na ndo wengi humumtandaoni
 
Exactly,tatizo wanaingizwa chaka na mafundi vishoka,ufanyaji kazi hauna tofauti,ili mfumo uwe Sawa lazima kuwe na vitu viwili
1,Septic tank
2,Suck away pit

SEPTIC TANK ;lazima isakafiwe kuta zote na itengenezwe kitaalam Kwa mujibu wa michoro ya kihandisi ili liweze kuchuja maji na kuyatoa kwenda katika SUCK PIT na kubakiza taka zote hapo ndio bacteria na wadudu wanaokuwa katika kinyesi kukua na kuzaliana na kazi yayo ni Kula uchafu wote unaobaki hapo,
Hapo ni ngumu hayo mashimo kujaa isipokuwa kama eneo Lina chemchem ni vema kwenye SUCK PIT ukaweka mawe huwa yanahamisha ile water table eneo lile na kurusu maji yanayokuja kupata nafasi,kumbuka hayo maji yakitoka vyooni na kwenye masinki yanakuja na mchanganyiko wa sabuni na mafuta hivyo SEPTIC TANK ikikosewa na ikawa inatuamisha hayo maji ya sabuni na mafuta hutengeneza utando juu ya maji na kusababisha joto Kali sana na oxigen kukosekana hupelekea wadudu hao kukimbia na wengine kufa ndio unaweza kuiona funza,minyoo na mende kwenye masinki.hivyo ni vema ukatumia wataalam na sio vishoka.
 
ISHI KISASA ZAIDI....!!!!!!
Tunatoa Hudumu ya ujenzi wa mashimo ya vyoo vya kisasa ni vyoo Bora na salama Kwa matumizi ya kila mtanzania

Sifa za vyoo vya kisasa.
[emoji1666] Ni Imara na vina ubora wa Hali ya juu.

[emoji1666] Ujenzi wake Hutumia eneo dogo

[emoji1666] Ni rafiki Kwa mazingira (Havitoi harufu mbaya)

[emoji1666] Hudumu kwa mda mrefu (si rahisi kujaa)

[emoji1666] Vinafaa Kwa matumizi ya makanisani/ miskitini, shuleni, hospital, nyumba za kuishi n.k

[emoji1666] Vinafaa maeneo yote yaani sehemu za kichanga, mfinyanzi, n.k

[emoji1666] Urefu futi 10 na upana futi 6 baada ya kuset tofari zinabaki futi 4 hadi 4.5

Na Haya mashimo gharama yake ni 1,500,000/ kwa mikoa Yote Tanzania

NB. Gharama zote za vifaa ni ndani ya bei tajwa yaani ni juu yetu.

Tunapatika Temeke Dar es salaam Tanzania na tunafanya kazi mikoa yote Tanzania bara na visiwani. Kwa mawasiliano zaidi tupigie 0789005562 au njoo wasap kwa link hii Wa.me//255789005562

By

Kelvin Hk
 
Jibu mada iliyoko mezani, why mnafanya bei kubwa?
And why hayajai ?
 
Jibu mada iliyoko mezani, why mnafanya bei kubwa?
And why hayajai ?
HaYana gharama kubwa! Gharama ni Kulingana na kazi inaYofanyika! Na HayaJai kwa sababu Ya mifumo Ya ujengaji! Tunatumia tofali zenye uwazi hivyo maji yanapotea hapo lakini pia tunapoteza kabla hayajafika kwenye shimo! So sio kwamba HaYajai milele Ila Yanachukua muda mrefu kujaa tofauti na mashimo Ya kawaida...Hii tunakupa hata miaka 50
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…