MamaSamia2025
JF-Expert Member
- Mar 29, 2012
- 14,588
- 32,361
Hii ni special case. Wanafunzi 1032 kwa darasa moja ni wengi sana. Hapo unapata mikondo 26 kwa wastani wa wanafunzi 40 kila mkondo. Shule kama Tanga Tech, Moshi Tech, Ilboru, Mzumbe na zingine za kitaifa huwezi kuta kwenye darasa moja kuna wanafunzi zaidi ya 50. Hao wa kata hawatendewi haki. Hapo wanafunzi 1032 unakuta kuna waalimu wasiozidi 10 wakati ilitakiwa wawe zaidi ya 50. Kwenye practicals waliingia kwa session ngapi?
Viongozi wa wanaojinadi kumsaidia Mama Samia kazi wajitafakari upya. Kusimama majukwaani na kutoa sifa kwa mama ni kama kichaka chenu cha kuficha madhaifu yenu. Leo siwalaumu hao vijana zaidi ya 400 waliopata sifuri. Kulikuwa hakuna namna.