Mashindano ya Dk. Samia, Gekul Cup yahitimishwa Babati Mjini, washindi wajinyakulia Tsh. Milioni 1

Mashindano ya Dk. Samia, Gekul Cup yahitimishwa Babati Mjini, washindi wajinyakulia Tsh. Milioni 1

Cute Wife

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2023
Posts
1,906
Reaction score
5,000
Wakuu,

Ila siasa bwana, mnahenyesha watu wee kwa Milioni 1? Ila sisi wananchi tumekuwa cheap sana, na hatujui thamani yetu kabisa. Ni mwendo wa kutumiwa tu kila inapokaribia uchaguzi, na sisi bila hiyana kama nyumbu tunatimiza azma zao!

=====

Screenshot 2024-11-11 152328.png

Mashindano ya Dk. Samia and Gekul yamehitimishwa rasmi kwa kucheza fainali katika uwanja wa Darajani November 10

Ambapo timu zilizofika fainali kwa Kundi la timu za Kata ni Kata ya Sigino na Bagara ambapo Kata ya Bagara ikiibuka mshindi kwa magoli mawili

Huku kundi la timu za taasisi zilizofika fainali ni Timu ya Bajaji na Eagle ambapo timu ya Eagle ilibuika mshindi kwa magoli sita.

Screenshot 2024-11-11 152336.png

Washindi wa Timu hizo zote mbili kila moja ameondoka na Milioni moja huku washindi wa pili wakiondoka na laki Tano na kufanya jumla zawadi zilizotolewa kuwa Milioni tatu Tsh 3,000,000.

Akihitimisha michuano hiyo Mbunge wa Jimbo la Babati Mjini Mheshimiwa Pauline Gekul ambaye ndiye alikuwa muasisi wa mashindano hayo ambayo awali aligawa mipira kwenye mitaa 35, Vijiji 13 Kata 8 na Taasisi 27 zilizokadiriwa kuwa thamani ya zaidi ya Million ishirini 20,000,000 huku Gharama za uendeshaji wa Ligi hiyo zikiwa zaidi ya Million kumi Tsh 10,000,000 hivyo kufanya Jumla ya Gharama zote kufika zaidi ya Million thelathini na tatu Tsh 33,000,000

Ametumia nafasi hiyo kuzipongeza timu zote kwa kufika hatua ya Fainali huku akisema wachezaji waliopatikana wapatao 40 kutoka kwenye timu zote zilizoshiriki watatafutiwa kocha ili kuwaendeleza na kuwa na Timu ya Jimbo.

Screenshot 2024-11-11 152345.png

Akitoa salamu za chama Cha Mapinduzi Katibu wa Chama hicho Wilaya ya Babati Mjini Ndug MOHAMED CHOLLAJE amempongeza Mbunge huyo kwa kutekeleza ilani ya Chama hicho kwa vitendo

Kwa upande wa Chama Cha mpira wa Miguu Wilaya ya Babati ambao wamepewa Jukumu ya kuwa walezi wa timu ya Jimbo wameahidi kuendeleza kile alichokianzisha Mheshimiwa Mbunge
 
Siasa ni maisha, maamuzi ya kisiasa yaweza sababisha biashara kushamili ama kufa kabisaa
 
Back
Top Bottom