avogadro
JF-Expert Member
- Apr 30, 2013
- 8,082
- 14,457
Nimesikitishwa sana na kitendo cha Tv za bongo kutokuonyesha mashandano ya riadha ya kimataifa yanayofanyika nchini marekani , ambapo kwenye mashindano hayo baada ya kutafuta channel zote za Tanzania nilikosa nikafanikiwa kuyaona live kwenye channel ya Kenya iitwayo KBC
Nilishangaa kumwona kijana Mtanzania katika marathon akipambana kwenye kundi la kuongoza ( leading group) mwanzo mwisho kwenye mashindano hayo magumu yaliyokuwa yamepaniwa na manguli wa riadha duniani, ilikuwa bado kidogo tu apate medali ila alizidiwa kaufundi kidogo na kubahatika kushika nafasi ya 7 dunia nzima👏👏👏👏 tena kwa muda mzuri sana
Sasa hivi bongo limezuga gonjwa baya sana la kuambukiza na linaoua vizazi ya michezo mingine, gonjwa hilo liitwalo SOKA au kabumbu limeingia kwenye ubongo wa Watanzania hivyo kuanzia asubuhi mpaka jioni Tv zinazungumzia soka, mitaani soka, wazee soka , katoto kanazaliwa kanaanza kulazimishwa kuwa kashabiki kwa kuvalishwa jezi za soka.
Kama taifa tunaharibu, lazima tuipe kila michezo uzito unaofaa.
Taifa letu vipaji vya asili ambavyo si vya kulazimishwa ni Riadha na ndondi hii soka tunalazimisha sii asili yetu. Tukitaka bendera ya nchi yetu ipeperushwe huku wimbo wa Taifa unaimbwa tuwekeze kwenye riadha