Mashindano ya kuwabeba wake/wapenzi yafanyika Uingereza

Mashindano ya kuwabeba wake/wapenzi yafanyika Uingereza

kirerenya

JF-Expert Member
Joined
Aug 27, 2013
Posts
1,696
Reaction score
2,253
uk.jpg

Haya ni mashindano ya 11 ya mbio za kubebana nchini Uingereza.

Chris Hepworth, akiwa amembeba Tanisha Prince kutoka West Drayton, London, alikimbia na kuibuka mshindi wa mbio za umbali wa mita 380.

Waandaaji wa michuano hiyo wanasema zoezi hilo lilianza mwezi June mwaka 793 AD.

mshindi 3.jpg


Washindani walikimbia umbali wa mita 15 kupandisha kwenye mwinuko na kushuka ambapo wameeleza kuwa ni kazi ngumu.

Washindani si lazima wawe na ndoa lakini angalau wawe marafiki.

Sheria inasema wenza wawe na zaidi ya miaka 18 na uzito wa kilo 50 na kuna adhabu ikiwa utamuangusha mwenza wako, ikiwa uzito ni chini ya kilo 50 aliyembeba analazimika kubeba furushi lenye vikopo ili kuongezea uzito.

Mshindi anasema kupanda mlima ilikuwa rahisi kuliko kuteremka.

Washindi wataenda kwenye michuano ya dunia mwezi Julai nchini Finland

Bwana Hepworth ana matumaini ya kushinda.

Waandaaji walitoa tahadhari wakisema kuwa ''kumbeba mke kunaweza kuwa jambo la hatari, kunakoweza kusababisha majeraha kama ya uti wa mgongo, kuvunjika miguu na mikono, majeraha usoni, kwenye fuvu la kichwa na hata kifo."

Ben na Hanna Brackenbury waliingia kwenye mashindano hayo kuadhimisha mwaka wa kwanza wa kumbukumbu ya ndoa yao

Wenza hao wamesema walikuwa wakifanya mazoezi kwenye bustani na kwenye mvua wakijiandaa na michuano.
Mshindi alipata pipa lenye bia anayeshika nafasi ya mwisho anapatiwa tambi na chakula cha Mbwa.

Chanzo: BBC Swahili

Mytake: Mashindano haya yakija bongo ama yataua au hakuna wataojitokeza kushiriki. Wengi wetu wake zetu ni vitipwatipwa🙂🙂🙂
 
Kibongobongo tunarahisisha mambo,tutatumia ungo chap na haraka tunamaliza.
 
Yaletwe na huku kwetu kama wanaume wengi hatujaishia kuvunjwa migongo..!!
 
[emoji23]ha [emoji23]ha [emoji23]h!! Umenichekesha kweli kweli, nguvu zipo rafiki mazoezini huwa tunabebana kama hivyo
Hahahaaa. Haya bana.

Ikija kutokea niite bana rafiki na mie nipate kukuona. Lol
 
VIDEO: Mashindano ya kuwabeba wake/wapenzi yafanyika Uingereza

2018


2017
 
Back
Top Bottom