Yoyo Zhou
Senior Member
- Jun 16, 2020
- 199
- 322
Siku hizi Wachina wanaoishi sehemu mbalimbali duniani wamefanya mashindano ya Mashua ya Dragoni ili kusherehekea Tamasha la kijadi la Mashua za Dragoni. Katika miaka ya hivi karibuni, mashindano hayo yamekaribishwa na watu wa nchi mbalimbali duniani. Kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa na Shirikisho la Kimataifa la Mashua za Dragoni, mchezo huu sasa unafanyika katika zaidi ya nchi 85, ukiwa na jumla ya washiriki zaidi ya milioni 50.
Ni nini kinachofanya mashindano ya Mashua za Dragoni yavutie watu kutoka tamaduni tofauti? Sababu kuu ni kwamba haihitaji tafsiri yoyote. Labda ni vigumu kwa wageni kufahamu alama za Tamasha la jadi la Mashua za Dragoni la China ikiwemo hadithi ya Qu Yuan, na chakula cha “Zongzi”, lakini midundo ya ngoma, mwendo wa kupiga makasia, na ushirikiano katika mashindano ya Mashua za Dragoni ni lugha ya mwili, ambayo mtu yeyote anaweza kuelewa mara moja anapoingia kwenye mashua. Huko Hungaria, sauti ya ngoma za Mashua za Dragoni kando ya Mto Danube imekuwa utamaduni wa majira ya joto kwa wenyeji. Nchini Ujerumani, vilabu vingi vinachukulia mashindano ya Mashua za Dragoni kama shughuli zao za kujenga timu.
Kadri mbio za mashua za Dragoni zinavyopata umaarufu ng'ambo, swali linaibuka: kwa kuwa si mashindano ya michezo tu, je, mila za kitamaduni zilizomo katika mashindano ya Mashua ya Dragoni ikiwemo shughuli za kuabudu dragoni, na karamu ya Mashua za Dragoni zitafanyika vipi? Baadhi ya waandaaji wa mchezo huo wamekuwa na mbinu ya kutatua suala hilo. Badala ya kuzitaka timu za kigeni kuiga kila desturi ya kale ya Kichina, wanapanga sherehe rahisi ya kabla ya mbio kuu. Wanawaalika wazee kutoka jamii ya Wachina kufanya ibada ili “kuamsha” mashua ya Dragoni, ikiambatana na maelezo kwa Kichina, na kuwaambia wapiga makasia wa kigeni kutazama na kugusa kichwa cha mashua ili kuhisi urithi tajiri wa kitamaduni ulio jumuishi.
Mashua ya Dragoni imesafiri kutoka kumbi za mababu za ukoo wa Wachina, ikipitia karne nyingi za historia hadi kutia nanga katika bandari za nchi mbalimbali duniani. Inabeba sio tu hadithi za zamani zinazopatikana katika majumba ya makumbusho, bali pia inaonesha uhai mpya wa utamaduni wa China. Mashua hizo zinawaleta pamoja watu wa lugha na rangi tofauti kwenye chombo kimoja, wanaungana katika juhudi zao za kusonga mbele.
Huenda hii ndiyo siri ya mvuto wake wa kudumu