Nimeona kuna mashindano ya MissJF 2023, ilikuwa wazo zuri ila lina ubatili mtupu. Naona kama mbinu nyingine ya udhalilishaji mkubwa wa wanawake unaofanyika jukwaani kila iitwapo leo. Sababu za kuiita mashindano haya kuwa ni "ubatili" mtupu ni kama ifuatavyo.
Mashindano haya hayana vigezo: Mashindano yoyote ni lazima kuwe na vigezo kwa washiriki wote ili kura zipigwe kwa haki na kigezo kisiwe kimoja, mashindano haya hayana kigezo chochote cha maana na kama mnavyojua mashindano ya U-Miss ni lazima kuwe na vigezo kwa washiriki wote ili Haki itendeke kwa washiriki wote.
Upendeleo kwa washiriki: Katika mashindano haya ambayo yameanzishwa kwa wazo la mtu mmoja tu, kumekuwa na upendeleo mkubwa sana, kuna baadhi ya watu hawajashirikishwa katika mashindano haya , na kuwafanya wahisi kutengwa na kufanya kuwa mashindano ambayo yana interests za upande mmoja wa shilingi.
Hakuna mchujo, ni mashindano ya kukurupuka: Kwa mara ya kwanza tunashuhudia mashindano yasiyokuwa na mchujo hasahasa mashindano ya U-Miss ambayo yana heshima kubwa sio tu nchini bali duniani. Mwandaaji wa shindano hili alikurupuka tu na kuwaza kuweka mashindano ambayo hayana mchujo, ametumia hisia zaidi kuliko ufahamu, mashindano haya yalipaswa kufanya muda mrefu sana yakiwa na mchujo mkali ili mshindi halali apatikane.
Mashindano haya kuna uwezekano wa nia ya kufichua identities za watu: Sijajua lakini ila naona ina mwelekeo huo. Maana baadaye utasikia watataka picha wakati hii ni platform ambayo inaficha privacy ya mtu.
Udhalilishaji kwa wanawake: Kutokana na kuanzishwa kwa mashindano haya, kuna baadhi ya wanajamvi wameanza kuwadhalilisha washiriki kwa maneno yao , jambo ambalo si nzuri, tumeona nyuzi nyingi zikidhalilisha utu wa wanawake na wala hazichukuliwi hatua.
Mwisho mashindano haya yako one sided(upande mmoja), vigezo havipo na imeanzishwa kihisia zaidi pasipo na matumizi ya akili. Niishie hapo.