Mashindano ya Olimpiki Ufaransa 2024

Tunaweza tukafunikwa pia 😄
Naamini tunaweza kupata japo medali za shaba, maana Tanzania kila baada ya nyumba kadhaa kuna Guest house na Lodge za kutosha.
 
Naamini tunaweza kupata japo medali za shaba, maana Tanzania kila baada ya nyumba kadhaa kuna Guest house na Lodge za kutosha.
😀😀 haya majengo ndo yanakuaminisha huko tunaweza?? Ila Olympics ina michezo mingi tungetafuta moja tujikite huko ili ijayo tupeleke watu wetu
 
😀😀 haya majengo ndo yanakuaminisha huko tunaweza?? Ila Olympics ina michezo mingi tungetafuta moja tujikite huko ili ijayo tupeleke watu wetu
Tatizo sio kama hakuna wanamichezo wa kuweza kushiriki kwenye mashindano ya Olympic, shida ipo kwenye vigezo vinavyotumika pamoja na maandalizi. Raia wa Tanzania ambae ni mwanamichezo endapo atashiriki hayo mashindano na kushinda kwenye mchezo fulani ndipo utasikia anaanza kusikika na hapo ndipo utakapoona Wizara, waziri mwenye dhamana husika anaanza kuwa karibu pamoja na kumsapoti huyo mwanamichezo. Tatizo ni je kabla ya huyo mwanamichezo kushinda walikuwa wapi katika kumtambua na kumuandaa? Lakini pia mara hii kwenye Riadha wapo wanamichezo kama vile Alphonce Simbu.
 
Vile vile inaonekanaTanzania tumelega kwenye kutafuta vipaji na kuviendeleza kuanzia ngazi za shule na kuendelea. Na kwanini tusiwe na Centre ambazo zitakuwa zinajishughulisha na mambo ya michezo kwa wenye vipaji ambapo moja ya kazi yao ni kuwaandaa na kuwasapoti vijana wenye vipaji katika michezo mbali mbali. Ili endapo itatokea uhitaji wa kushiriki kwenye mashindano watapata nafasi ya kushiriki ili hata kama mbeleni wakiwa wanamichezo maarufu watajulikana ni wapi walipoanzia.
 
Mimi napenda sana hii michuano! Inaanza UEFA CHAMPIONS LEAGUE, WORLD CUP halafu OLYMPIC SEASON 🏆🏅
Mimi sipendi mpira so olimpiki ndio hua unanipa hamasa ya kuiangalia hasa kuogelea kwa aina yoyote, kukimbia, handball ama volleyball game za wanawake, kulenga shabaha, kutembea, kuendesha baiskeli na michezo mingine mingi ila sio mpira
 
Au wanaogopa atasifiwa zaidi ya mwanasiasa
 
Kuna madada yanacheza volleyball yamepanda, ni warembo acha
 
Kamepata uhuru juzi na bado kana vita
 
Kamati ya Olimpiki Tanzania hawaja promoti michezo mingi, wamewekeza zaidi kwenye mbio hasa marathon. Kuna michezo kama kulenga shabaha, kurusha mkuki, mishale, weight lifting nk. Bahati nzuri siku hizi kila sehemu kuna gym, hawa mabaunsa wakifundishwa tunaweza kupata washiriki.
 
Wakuu, mwenye connection inayotrend kwasasa naomba anitumie pm nimechelewa kuipata🙏
 
Mtu anaumia kwenye kupasha dakika 5 labla ya race
 
waziri alienda na timu, tunataka akirudi aliambie taifa wameleta dhahabu au hata shaba tu au walikuwa perdiem bure.
 
waziri alienda na timu, tunataka akirudi aliambie taifa wameleta dhahabu au hata shaba tu au walikuwa perdiem bure.
Tegemea sentensi hii “tunaenda kujipanga na kujiandaa kwaajili ya mashindano mengine”
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…