Mashine ya kutengenezea mkaa wa kisasa inauzwa

Mashine ya kutengenezea mkaa wa kisasa inauzwa

Biashara2000

JF-Expert Member
Joined
Nov 9, 2013
Posts
649
Reaction score
547
Habari zenu. Mnamo mwezi wa nne mwaka huu nilinunua mashine ya kutengeneza mkaa wa kisasa kwa kutumia matakataka makavu kwa sh. 850,000 kutoka katika shirika la wafaransa liitwalo ARTI Energy ARTI Energy ambao wako pale Mbezi tanki bovu. Mashine hii inatumia motor ya umeme na ina uwezo wa kutengeneza viroba vile vya kilo hamsini vya mkaa 5 kwa siku. Kwa maana hiyo ni kuwa kama uko Dar na unatengeneza magunia 5 ya mkaa na kuuza kwa sh. 15,000 tu, kwa siku unatengeneza sh. 75,000. Mimi naiuza mashine hii kwa sh. 500.000. Kwa maana hiyo chini ya siku 10 utakuwa usharudisha hela yako. Utakaponunua mashine hii utapata na pipa bla kuchomea matakataka na training kutoka kwangu bure.

Sababu ya kuiuza mashine hii ni kuwa, nimeamua kuukuza mradi wangu zaidi kwa kununua mashine kubwa kidogo ya hii kutoka katika shirika hilo hilo.

Kwa ambaye yuko interested awasiliane na mimi ili apate kuja kuiona mashine yenyewe.

Asanteni.
 
daah me niko mbali bt inaonekana ni biashara poa. Unaweza kunisaidia jinsi ulivyoanza na inakuwaje hii biashara? Namba yako tafadhali kama hutojali
 
Nashukuruni kwa watu wote mlioniandikia msg. Karibu wote wameniandikia wakiniomba niwaelekeze jinsi mkaa huo unavyotengenezwa. Kuna wengine wao wameniomba waje watembelee mradi waone hiyo mashine nimewapa namba yangu. Na kuna wengine wameniomba niwaeleze jinsi ya kutengeneza mkaa huu bila kutumia mashine kwa kuwa hawawezi ku afford kununua mashine hizi.

Inawezekana kutengeneza mkaa huu nyumbani kwako kama una eneo la kutosha bila kuwa na mashine. Ila utahitaji pipa. Naweza kutoa mafunzo kwa watu wanaotaka. Gharama yake ni sh. 40,000/= pamoja na 1500/= ya nauli. Mafunzo haya ni kwa mkazi anayeishi Dar. Kutengeneza bila kutumia mashine utakuwa unatengeneza gunia 1 - 2 kwa siku kutegemeana na spidi ya mikono yako. So kwa kuweka investment ya 41500/= ndani ya siku 2 usharudisha investment yako (kama utakuwa unatengeneza gunia 2).

Asanteni
 
Hongera sana
 
Back
Top Bottom