Mashine ya kuzalisha mikate

Mashine ya kuzalisha mikate

Ungependa kujua historia ya mikate, hili ni jukwaa la historia...
Haya bana, hii hapa historia ya mikate....


Historia ya mashine za kuoka mikate
Kulingana na wanahistoria wa chakula, Wamisri wa kale walikuwa utamaduni wa kwanza kuonyesha ustadi wa hali ya juu wa kuoka . Kamusi ya Kiingereza ya Oxford inafuatilia neno la Kiingereza keki hadi karne ya 13. Ni linatokana na neno 'kaka', neno la Kinorse cha Kale. Waokaji wa Ulaya wa zama za kati mara nyingi walitengeneza keki za matunda na mkate wa tangawizi.
"Tanuri" za kwanzaza kuoka mikate zilianzia kipindi cha kwanza cha kilimo cha historia ya mwanadamu, wakati wa makazi ya kwanza ya kudumu ya wanadamu.
Tanuri iliyotengenezwa na chakula cha kwanza ambacho wanadamu walijua kupika: nafaka za kukaanga, kisha mikate ya gorofa na hatimaye mkate uliotiwa chachu. Inasemekana kwamba mkate uliotiwa chachu ulivumbuliwa kwa bahati mbaya miaka 5000-6000 iliyopita katika Mashariki ya Karibu: unga wa mkate wa bapa ambao ulikuwa umewekwa kando kwa muda ulianza kuchacha na kuinuka kabla ya kupikwa!
Tangu wakati huo, kupitia vipindi na tamaduni tofauti, wanadamu wameendelea kuboresha mbinu za kupikia mkate , hatimaye kuunda tanuri ya kuni tunayojua leo.

Asili ya Misri na Mesopotamia​

Ustaarabu huu uliwajibika kwa tanuri za mkate za kwanza (karibu miaka 5000 iliyopita). Chungu kikubwa cha udongo kiliwekwa juu chini juu ya makaa na makaa. Baada ya sufuria ya udongo kuwashwa moto mkate wa gorofa au unga uliwekwa ndani na kupikwa kwa mara ya kwanza na joto kutoka pande zote.

Tanuri hii ya msingi iliboreshwa baadaye na maendeleo ya tanuri ya kwanza ya "Tandur", ambayo bado inatumiwa leo, hasa nchini Pakistani kupika mkate maarufu wa "Naan".

Tanuri hizi zilitengenezwa kwa udongo na nyasi na umbo la kiuno kirefu, lililopinda, lililokuwa wazi. Moto na makaa ya moto kwenye pipa ilipasha moto oveni. Kuoka mkate ilikuwa shughuli iliyopangwa vizuri ambayo ilifanyika katika maduka halisi ya mikate, na mkate ulikuwa muhimu sana ulitumiwa kama malipo ya aina ya mishahara na kodi.

Mkate​

Mkate ni chakula kinachotengenezwa kwa kuoka kinyunga cha unga na maji. Mara nyingi viungo fulanifulani huongezwa kwa kubadilisha ladha. Kuna pia mikate inayotiwa kiasi kidogo cha mafuta.

Namna za mkate​

Kimsingi kuna aina mbili za mkate:
  • mkate wa kinyunga kilichochachuka
  • mkate wa kinyunga kisichochachuka
Mikate bapa aina ya chapati hutengenezwa katika sufuria, kaango au hata juu ya jiwe la joto. Mikate minene huhitaji joko (oveni) yaani jiko lenye chumba ndani yake. Lakini kuna pia aina za mikate bapa inayotengenezwa katika oveni.
Kama kinyunga kinatengenezwa kwa kuongeza mafuta mengi, sukari na maziwa si mkate tena bali keki.




Mkate wa Ufaransa.

Mkate mweusi wa Ulaya ya Kati na Mashariki unaotengenezwa kwa unga la ngano nyekundu.
Mkate wa Kijerumani uliotengenezwa kwa ngano nyekundu.

Chapati.

Tortilla.


Aina ya mikate isiyochachuka​

Chapati ni aina ya mkate usiochachuka pamoja na tortilla ya Mexico na mikate mbalimbali za Ulaya. Hapa unga na maji hukorogwa kuwa aina ya ugali mzito, halafu kinyunga huandaliwa kwa umbo la sahani bapa na kuwekwa juu ya jiwe la joto au ndani ya sufuria juu ya moto.
Aina mbalimbali za chapati hizi zinaongezewa ladha kwa kutiwa mafuta au viungo ndani yake.
Aina hizi zote ni nyembamba kwa sababu kinyunga huwa kizito mno bila kuchachuka.
Hii ni mbinu asilia wa kutengeneza mikate.

Mikate iliyochachuka​

Kwa aina nyingi ya mikate kinyunga huchachuka. Kuna dawa mbalimbali zinazofaa kuwa chachu kama hamira. Vijidudu vya chachu viko hewani, kwa hiyo kinyunga kitachachuka kikikaa hewani kwa muda wa siku moja au zaidi (chachu asilia).
Njia ya haraka na uhakika ni kutia dawa ya hamira iliyonunuliwa. Kama friji ipo inawezekana kuweka akiba ndogo ya kinyunga kilichochachuka kando kila safari. Kitatunzwa katika hali baridi halafu kukorogwa katika kinyunga kipya.
Mikate iliyochachuka huokwa katika oveni.
Kuna aina nyingi sana za mkate duniani. Tofauti za rangi na ladha zinatokana na aina ya unga na namna ya kuoka katika oveni. Kwa jumla mikate inayotumia unga wa nafaka yote huwa nyeusi zaidi. Mikate myeupe-myeupe hutokana na unga wa nafaka iliyokobolewa.
Nafaka kama ngano nyekundu na shayiri huleta pia mkate mweusi zaidi.

Mkate na utamaduni​

Mkate kama chakula cha kila siku ni sehemu ya utamaduni wa nchi nyingi. Takwimu kuhusu matumizi ya mkate katika nchi mbalimbali zinatiofautiana. hata hivyo inaonekana kwamba Uturuki na Iran wana matumizi makubwa, zaidi ya kilogramu 100 kwa mwaka kwa kila mtu. Nchi nyingine yenye matumizi makubwa zinapatikana katika maeneo ya Bahari Mediteranea, pamoja na Ulaya ya Kati.
Mkate wa Ujerumani umekubaliwa katika orodha ya urithi wa Dunia ya UNESCO, ilhali nchi hii inajivunia kuwa na aina nyingi za mkate.
Nje ya miji mikubwa kuna bado kawaida ya kuoka mikate nyumbani katika nchi kadhaa, hasa za Asia Magharibi.

Mkate na dini​

Mkate uliingia pia katika sala kuu ya Ukristo "Baba yetu", ambayo ilitungwa na Yesu Kristo mwenyewe na kuripotiwa katika Injili ya Mathayo na Luka ikiwa na tofauti ndogo kuhusiana na urefu wake.
Ombi la nne katika Mathayo linataja "mkate wa kila siku". Katika tafsiri za Kiswahili za sala hii ombi limetafsiriwa kwa njia mbili tofauti.
Utamaduni wa Waafrika wengi haukujua mkate kama chakula. Neno "mkate" kiasili kilimaanisha kipande cha chochote kilichokatwa kutoka sehemu kubwa zaidi.
Wamisionari Wazungu Walutheri waliofika Afrika ya Mashariki walitoka Ujerumani ambako mkate si chakula cha kila mlo wakajua katekesimo ya Martin Luther ambamo swali, "Mkate wa kila siku unamaanisha nini?", linajibiwa: "Chochote tunachohitaji kwa mwili na maisha kama vile kula, kunywa, nguo, viatu, nyumba, kaya, shamba...". Hapo waliona kuna neno la Kiswahili "riziki" kinachotaja maana ya chakula ambacho wakati ule hakikujulikana kwa Waafrika.
Wamisionari Wakatoliki walitoka nchi kama Ufaransa na Italia ambako mkate ni sehemu ya kila mlo kwa hiyo walitafuta neno linaloweza kutaja chakula chenyewe wakiona "mkate" unakatwa walichukua neno hili. Pamoja na utamaduni wao wa nyumbani, unaofanana zaidi na ule wa Wayahudi, walisisitiza kama mababu wa Kanisa wote uwemo wa Kristo katika ekaristi kuwa chakula cha roho kilichotolewa na Yesu kama mkate wakati wa karamu ya mwisho.

Picha​

  • Mkate bapa wa Uturuki uliochachuka
    Mkate bapa wa Uturuki uliochachuka
  • Mkate wa Kiingereza
    Mkate wa Kiingereza
  • Kuandaa mkate bapa
    Kuandaa mkate bapa
  • Mikate midogo
    Mikate midogo
  • Ganda la mkate
    Ganda la mkate
  • Mkate dukani
    Mkate dukani
  • Mikate ya fimbo
    Mikate ya fimbo
  • Mkate duara wa Poland
    Mkate duara wa Poland
 
Bwashee, kwanza utambur fika mikate haizalishwi! Mikate inaokwa. Na mpaka ifikie hiyo hatua ya kuokwa, inapitia michakato mbalmbali.
Na michakato hiyo inaweza ikahusisha mashine tofauti tofauti kulingana na uwezo wako, au baadhi ya michakato unaweza hata kutumia mikono yako.

Na ili uifikie hiyo hatua ya mwisho kabisa ya kuoka, nasi ni lazima uwe na oven ya kuokea hiyo mikate. Na kama una uwezo wa kuchimbua makaburi ya humu jukwaani, basi utakutana na mada kibao tu zinazohusiana na hiyo biashara ya kuanzisha bakery!
 
Back
Top Bottom