KERO Mashine ya Reach Stacker Chuo cha Bandari Dar ni mbovu, inatukwamisha, tunashindwa kujifunza kwa vitendo

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Kero yangu ni kuhusu Chuo cha Bandari kilichopo Tandika Jijini Dar es Salaam, sisi tunaosoma kozi fupi ya Reach Stacker tunapokwenda kwenye mafunzo kwa vitendo pale NASACO Bandarini hukuta mashine moja, pia mashine yenyewe ni mbovu na chakavu.

Tunaishia kufundishwa kwa maneno na kubadilishiwa mashine nyingine inaitwa Empty Handler, ukiwaeleza walimu wa chuoni wanasema hili si kosa lao kama uongozi wa bandari hawana hiyo mashine wao wataipata wapi?

Kwahiyo tunamaliza mafunzo na kupewa vyeti lakini ujuzi tunakua hatuna.


Mfano wa Mashine ya Reach Stacker


Mfano wa mashine tunayobadilishiwa - Empty Handler​
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…