KWELI Mashine za Kunyolea nywele zinaweza kusambaza VVU

Taarifa hii imethibitika kuwa ya kweli baada ya kufanya tathmini ya kina
Heeh mbombo jilipo
 
Nadhani hizi mashine bei zake si kubwa sana. Tujali afya zetu.
Tubebe mashine, vitana, apron, spirit, baada ya kunyoa rudi nyumbani jisafishe mwenyewe

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hivi inakuaje kwa mbu anaetoka kunyonya damu ya mtu mwenye HIV halafu akaenda kumnyonya mwingine ambae sio muathirika?
 
Ni ngumu mno kama ingekua rahis hivyo watu wote wangekuwa wameambukizwa ukimwi
 
Hivi inakuaje kwa mbu anaetoka kunyonya damu ya mtu mwenye HIV halafu akaenda kumnyonya mwingine ambae sio muathirika?
Mbu hawana T cells ambazo ndo hufanya virusi kuishi na kuzaliana kwenye mwili wa binadamu hivyo virusi wanapoingia kwenye mwili wa mbu humeng'enywa na kufa. Pia mbu ana sehemu mbili kwenye mdomo wake moja hunyonya damu na sehemu nyingine humuingiza mtu mate pale anapomng'ata.
 
Wazee wa kuzingatia "Angle" uzi huu unawahusu.

Serikali yetu kupitia wizara ya afya imekua ikitumia jitihada kubwa sana katika kuhakikisha maambukizi ya VVU yanapungua nchini. Moja ya jitihada hizo ni utoaji wa elimu kwa jamii namna mbalimbali za kujikinga na maambukizi hayo, mfano kuepuka ngono zembe, na kuepuka kuchangia vifaa vyenye ncha kali kwani vitu hivyo husababisha kwa kiasi kikubwa kuenea kwa maambukizi.


Ningependa kufahamu ikiwa mashine ya kunyolea ni moja ya vifaa vyenye ncha kali, Je ni kweli mashine za kunyolea saluni husababisha kuenea na maambukizi ya VVU?
Kama jibu ni ndio, kwanini mkazo usiwekwe katika utoaji elimu hususani mashuleni, kwenye vyombo vya habari, na taasisi zingine za umma kuhusiana na matumiz i sahihi ya mashine hizi? kwana sababu kwenye wanaume 100 kuna uwekakano wanaume za zaidi ya 80 wananyoa saluni kwa kutumia mashine za kuchangia. Kama ni kweli nyia hii inaambukiza hamuoni watu wengi tupo kwenye hatari kubwa?

Nimefanya uchunguzi, kwenye saluni 15 unaweza kubahatika kukuta saluni 1 tu ambayo ina sterilizer, tena utakuta imewekwa kama fashion tu, haitumiki ipasavyo kama vile baada ya mtu mmoja kunyolewa.

Ushauri: Kama unajiweza kiuchumi ni bora ukanunua mashine yako binafsi ili unapoenda kunyolewa saluni utumie mashine yako mwenyewe, hii itasaidia kuepuka kupata hata magonjwa mengine kama vile ya ngozi.
 
Mzee ukianzisha sterilization ya machine si saloon za vichochoroni itakuwa ni 20k
Au unaongelea disinfection ya kutumia split
 
kuna daktari keshawahi kumuona kirusi wa HIV kwenye darubini???mana kuna dhana zinasema ukimwi kama ukimwi ulikuwepo tangu zamani shida ni huyo virus anayejukikana kama HIV inasemekana hayupo.Picha tunazoona kwenye vitabu ni za kuchora.....anyway kina Deception wana majibu zaidi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…