KWELI Mashine za Kunyolea nywele zinaweza kusambaza VVU

KWELI Mashine za Kunyolea nywele zinaweza kusambaza VVU

Taarifa hii imethibitika kuwa ya kweli baada ya kufanya tathmini ya kina
Kisayansi na kibaiolojia virusi wanasifa ya kutokuwa hai pale wanapokuwa nje ya seli ya kiumbe mwingine(host) na wanaweza kukaa muda mrefu bila kuwa na dalili zote za viumbe hai mpaka pale watapoingia kwenye seli ya kiumbe.

Inakuwaje sasa tunaambiwa HIV haambukizwi kwa mashine za kunyolea saloon kwa kigezo cha kwamba hawawezi kuishi katika mashine na ilihali wao ni vijidudu visivyo hai wanapokua nje ya host?

804A5D72-8B77-4730-A582-E3B90D52FE9A.jpeg
 
Tunachokijua
HIV ama Human Immunodeficiency Virus ni kirusi kinachoshambulia mfumo wa kinga mwili, ambacho baada kuishi mwilini kwa kipindi fulani kinaweza kusababisha upungufu wa kinga mwilini (UKIMWI).

Virusi hawa wanaweza kumwingia mtu kupitia ushiriki wa tendo la ndoa ambapo majimaji ya uke, uume au shahawa ndiyo hubeba virusi hawa, kushirikiana vitu vyenye ncha kali, kubadilishana damu na mazao yake au maambukizi ya mama na mtoto wakati wa ujauzito, kujifungua na kunyonyesha.

Virusi hawa wenye sifa ya RNA, hubeba aina 15 za protini pia huzungukwa na kuta mbili za mafuta. Hushambulia seli hai zenye vipokeo vya CD4 pekee, hubadilika mara kwa mara pamoja na kupoteza sifa ya kuishi kikiwa kwenye mazingira yasiyo rafiki.

Ili virusi viweze kuingia mwilini na kusababisha madhara huhitaji mambo matatu ya msingi-
  1. Damu au Majimaji ya mwili
  2. Kitendo hatarishi
  3. Upatikanaji wa moja kwa moja wa mishipa ya damu
Kunyoa salon ni kitendo hatarishi, lakini hukosa sifa mbili za ziada za kutoa mazingira yenye majimaji ya mwili pamoja na upatikanaji wa moja kwa moja wa mishipa ya damu ili virusi waingie.

Hii ndiyo sababu inayofanya watu wengi wasiambukizwe VVU kupitia salon na siyo kutokuishi kwa virusi kwenye mashine kama hoja ya mdau ilivyo.

Hata hivyo, JamiiForums inatambua kuwa hali hii haitoi maana kuwa salon haziwezi kabisa kuambukiza VVU hasa katika hali ambazo mazingira yote matatu yatakuwepo.

Ni muhimu kwa wamiliki wa salon kutakasa mashine zao kila mara pamoja na kuchukua tahadhari zote za kulinda wateja ikiwemo kutowakwangua sana ili kuepusha uwezekano wa kuichubua mishipa ya damu, kitendo kinachoweza kutoa nafasi ya kuingia kwa virusi mwilini.
MADAI
Kisayansi na kibaiolojia virusi wanasifa ya kutokuwa hai pale wanapokuwa nje ya seli ya kiumbe mwingine(host) na wanaweza kukaa muda mrefu bila kuwa na dalili zote za viumbe hai mpaka pale watapoingia kwenye seli ya kiumbe.

Inakuwaje sasa tunaambiwa HIV haambukizwi kwa mashine za kunyolea saloon kwa kigezo cha kwamba hawawezi kuishi katika mashine na ilihali wao ni vijidudu visivyo hai wanapokua nje ya host?

View attachment 2391953
Heeh mbombo jilipo
 
Nadhani hizi mashine bei zake si kubwa sana. Tujali afya zetu.
Tubebe mashine, vitana, apron, spirit, baada ya kunyoa rudi nyumbani jisafishe mwenyewe

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hivi inakuaje kwa mbu anaetoka kunyonya damu ya mtu mwenye HIV halafu akaenda kumnyonya mwingine ambae sio muathirika?
 
MADAI
Kisayansi na kibaiolojia virusi wanasifa ya kutokuwa hai pale wanapokuwa nje ya seli ya kiumbe mwingine(host) na wanaweza kukaa muda mrefu bila kuwa na dalili zote za viumbe hai mpaka pale watapoingia kwenye seli ya kiumbe.

Inakuwaje sasa tunaambiwa HIV haambukizwi kwa mashine za kunyolea saloon kwa kigezo cha kwamba hawawezi kuishi katika mashine na ilihali wao ni vijidudu visivyo hai wanapokua nje ya host?

View attachment 2391953
Ni ngumu mno kama ingekua rahis hivyo watu wote wangekuwa wameambukizwa ukimwi
 
Hivi inakuaje kwa mbu anaetoka kunyonya damu ya mtu mwenye HIV halafu akaenda kumnyonya mwingine ambae sio muathirika?
Mbu hawana T cells ambazo ndo hufanya virusi kuishi na kuzaliana kwenye mwili wa binadamu hivyo virusi wanapoingia kwenye mwili wa mbu humeng'enywa na kufa. Pia mbu ana sehemu mbili kwenye mdomo wake moja hunyonya damu na sehemu nyingine humuingiza mtu mate pale anapomng'ata.
 
Wazee wa kuzingatia "Angle" uzi huu unawahusu.

Serikali yetu kupitia wizara ya afya imekua ikitumia jitihada kubwa sana katika kuhakikisha maambukizi ya VVU yanapungua nchini. Moja ya jitihada hizo ni utoaji wa elimu kwa jamii namna mbalimbali za kujikinga na maambukizi hayo, mfano kuepuka ngono zembe, na kuepuka kuchangia vifaa vyenye ncha kali kwani vitu hivyo husababisha kwa kiasi kikubwa kuenea kwa maambukizi.
f87340cdb14be9544d2e727a6948e41a.jpg

Ningependa kufahamu ikiwa mashine ya kunyolea ni moja ya vifaa vyenye ncha kali, Je ni kweli mashine za kunyolea saluni husababisha kuenea na maambukizi ya VVU?
Kama jibu ni ndio, kwanini mkazo usiwekwe katika utoaji elimu hususani mashuleni, kwenye vyombo vya habari, na taasisi zingine za umma kuhusiana na matumiz i sahihi ya mashine hizi? kwana sababu kwenye wanaume 100 kuna uwekakano wanaume za zaidi ya 80 wananyoa saluni kwa kutumia mashine za kuchangia. Kama ni kweli nyia hii inaambukiza hamuoni watu wengi tupo kwenye hatari kubwa?

Nimefanya uchunguzi, kwenye saluni 15 unaweza kubahatika kukuta saluni 1 tu ambayo ina sterilizer, tena utakuta imewekwa kama fashion tu, haitumiki ipasavyo kama vile baada ya mtu mmoja kunyolewa.

Ushauri: Kama unajiweza kiuchumi ni bora ukanunua mashine yako binafsi ili unapoenda kunyolewa saluni utumie mashine yako mwenyewe, hii itasaidia kuepuka kupata hata magonjwa mengine kama vile ya ngozi.
 
Uwezekano utakuwepo kama chombo kitakuwa contaminated na maji maji au damu kutoka kwa mtu mwenye VVU na kutumika kwa mtu asiye na maambukizi ya VVU lakini na yeye awe na vidonda au open cut wounds au mikwaruzo.

Risk ya maambukizi itapungua kama chombo kikipata sterilization ipasavyo.

Risk ya maambukizi itapungua ikiwa kuna muda wa kutosha kutoka chombo kinachotumika kwa mtu mmoja hadi mwingine, umuhimu wa kuwa na mashine zaidi ya moja, yaani mashine ilkishatumika isafishwe vizuri ifanyiwe sterilization.
Mzee ukianzisha sterilization ya machine si saloon za vichochoroni itakuwa ni 20k
Au unaongelea disinfection ya kutumia split
 
kuna daktari keshawahi kumuona kirusi wa HIV kwenye darubini???mana kuna dhana zinasema ukimwi kama ukimwi ulikuwepo tangu zamani shida ni huyo virus anayejukikana kama HIV inasemekana hayupo.Picha tunazoona kwenye vitabu ni za kuchora.....anyway kina Deception wana majibu zaidi
 
Back
Top Bottom