Kaka mwisho
JF-Expert Member
- Dec 19, 2011
- 407
- 178
Unaweza kuweka specifications zake na picha tujue ni aina gani na pia kwanini unauza incubator hiyo imetengenezwa wapi? pia weka contact zako hasa e-mail.
kuna incubator iko sokoni.. ni automatic ila mayai unageuza manually. iko very effecient na utotoleshaji ni zaidi ya asilimia 85.
inatumia umeme mdogo sana. hata solar yenye uwezo wa kuwasha taa mbili inauwezo wa kuiendesha.
capacity yake ni mayai 400. inauzwa kwa sh laki saba. kama uko interested ni pm mawasiliano yako.
Ni automatic ila mayai inageuza manualy? Kwan maana ya automatic ni nini?
Mkuu mashine za kutumia mafuta ya taa kwa kweli hazifai ni 100% manual unatakiwa uishi pembeni ya mashine, hivyo mashine nzuri ni za automatic ambazo unaweza ukawa hata unaenda kazini na kurudi jioni kuchungulia labda umeme ukatike, Mahine ukiwa na uhakika wa umeme unaweza hata maliza 10 days hujaifungua au hata kuingalia inaendela vipi, make ziko ambazo hata maji yanajiongeza yenyewe pale ynapo pungua.
So tafuta mashine automatic, kuhusu umeme nyingi hazili umeme kiasi kwamba unaweza ukawa na sola tu ya kawaida na bado ukapiga kazi, na hata generea bado ni zuri mashine ya mayai 150 -200 inaendeshwa na jenereta ndogo sana.
Nina mashine ya mayai 176 na hapa nyumbani ninatumia solar maana umeme bado haujafika. Jenereta yenye ukubwa gani inaweza nisaidia kufanya shughuli ya utotoresjaji? Cc.Chasha poultry farm na yeyote mwenye ufahamu katika hili.
Jamani mimi naulizia mayai ya kienyeji tu maana leo incubator yangu imetema mzigo, wajinga waliniuzia mayai mabovu tray nzima