Mashine za NIDA zote wilaya ya Arusha zaibwa

Mashine za NIDA zote wilaya ya Arusha zaibwa

Hayo yamethibitishwa na Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Jerry Muro ambapo amesema hakuna mlango uliovunjwa wala mahali popote palipohifadhiwa mashine hizo. Mkuu wa Wilaya amesema huo ni wizi wa kimkakati na polisi mkoani Arusha wameanza msako mara moja kwa ajili ya kufuatilia suala hilo.

Wana bodi hii habari inashangaza, hao wezi wameiba kwa sababu gani hizo mashine, ili zoezi liongezwe muda? au hawakujua ni mashine za kitu gani? na ni wezi wanaojielewa kwasababu wamezichomoa mashine peke yake bila kuathiri kitu kingine chochote!.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Najiuliza mashine kama hizo mtu anaenda kuzitumia kwa shughuli gani
 
Hivi zile PC za DPP zilizokombwa zilipatikana?
 
kamateni wafanyakazi wote wa NIDA wikaya mkuu wa wilaya mkuu wa mkoa hata ikiwezekana mkurugenzi wote wawekwe ndani kwa uzembe.
Ukishasema hivyo tu!! hawawezi kushikwa kwa madai ya kuwa hawapangiwi!! iiiiii in someones voice
 
Najiuliza mashine kama hizo mtu anaenda kuzitumia kwa shughuli gani
Vifaa vilivyoibwa bila shaka itakuwa ni kompyuta, printers za kawaida, labda vifaa vya kusoma alama za vidole, kamera n.k, vifaa ambavyo kibaka yoyote mwenye njaa anaweza kuiba...

Sidhani kama mtambo wa kuchapa au kudurufu vitambulisho utakuwepo kwenye ofisi ndogo...
 
Vifaa vimeibiwa NI vya wilaya ya ARUSHA nahuyo anaetoa maelezo ya kuibiwa n mkuu wa wilaya ya ARUMERU Kama mm ningekuwa RPC ARUSHA ningeanza na huyu mkuu wa wilaya ya ARUMERU angenisaidia kwenye uchunguzi wa wizi huo.
Yaani hapo watoto pendwa wanamuundia zengwe mwenzao! Jamani??!!1
 
Hizi camera tatu hawawezi kununua zingine? Hizo laptop si wanunue tu zingine..
 
Back
Top Bottom