Mashirika gani yanasaidia wanafunzi wanaotokea mazingira magumu , kidato cha 1 - 4

Mashirika gani yanasaidia wanafunzi wanaotokea mazingira magumu , kidato cha 1 - 4

Joined
Dec 13, 2023
Posts
67
Reaction score
238
Ndugu wana jamiiforum ni matumaini yangu nyote mnaendelea vyema.

Nina mdogo wangu anaenda kidato cha pili sasa , lakini kutokana na chanagomoto za kiuchumi nina wasiwasi huenda si ndoto yangu tu hata yake huenda ikafa.

Amesoma shule ya msingi na kufanikiwa kuwa na ufaulu wa juu hatimaye akapata nafasi ya kwenda shule ya Ilboru,
Wakati huo mzee alikuwa anapambana anapata pesa anampa ya nauli, na mambo mengine.

Sasa hivi karibuni mzee wetu amepoteza kila kitu hadi nyumba ameuza kiufupi hakuna pa kuishi tena.
Pesa ya nauli kuja likizo na kurudi shule na mahitaji mengine nilikuwa najibana namsaidia lakini hivi sasa hata mimi ninapata changomoto hata kulipa ada, makazi na mambo mengine nikiwa chuo maana bumu halitoshi najikuta nashindwa kumsaidia mdogo wangu hata pesa ya kurudi shule.

Kufanya umahisho kurudi shule ya kata hapo kusoma inakuwa ngumu kwasababu ya makazi , hakuna msaada wa ndugu wala mtu yeyote.

Wakuu kama kuna mtu anafahamu mashirika au scholarship zozote zinaweza kusaidia naomba anifamishe .
Natanguliza shukrani
 
Back
Top Bottom