Mashirika na Taasisi za Umma zinazostahili kufutwa na zile zinazostahili kuunganishwa

Naomba tuwe serious, Kama unapenda utani nenda jukwaa la jokes .

Viongozi wa serikali wapo hum Na zipo shuhuda kadhaa zinazoonyesha huwa wanapitiapitia hum kupata ABC sasa sio busara kuleta utani kwenye nyuzi Kama hizi.
Kweli kabisa..watu wanaleta dhihaka kwenye vitu vya msingi
 
Kipindi inaitwa TFDA nafikiri ndo ilikuwa inaendana sana na TBS.

Nimeonelea hii TMDA na NIMRI ziwekwe pamoja maana zote zinabase kwenye madawa.
NIMR imejikita kwenye tafiti za magonjwa ya binadamu.

TMDA imejikita kwenye udhibiti wa madawa ya binadamu na mifugo.

Ebu fikiria tena namna ya kuziunganisha
 
Serikali imesema imetumia jopo la wataalam kubaini mashirika ya kuunganishwa na Yale ya kufutwa.
Nashangaa serikali haiwezi kutumia wataalam Hawa wenye elimu, busara, maono, hekima, akili kuendesha bandari zetu au mbuga zetu au viwanja vya ndege.
Akili ya Hawa wataalam kilele chake Ni kugundua kwamba shirika la polisi uzalishaji Mali lifutwe.
 
Mamlaka ya kupambana na dawa za kulevya ipelekwe polisi,REA iunganishwe na TANESCO VETA na NACTE
 
πŸ‘πŸ‘πŸ™πŸ†’
 
Mashirika ambayo kwangu naona bora yaunganishwe..
  • TARURA Na TANROADS
  • LATRA na TASAC (bora zote zirudi kuwa SUMATRA)
  • REA na TANESCO
  • TCU na NACTE
  • Tungekuwa Na wizara moja yenye Jina la Wizara ya Usalama Wa Raia,Ulinzi wa mali,Rasilimali,Utu na Haki ya Raia.. (JESHI LIKABAKI MOJA TU)
    • Halafu tukawa na idara kama zamani au kama wenzetu nchi za nje.. Kwenye hii wizara kama POLISI,UHAMIAJI,TAKUKURU,ASKARI WA TANAPA,MGAMBO,Na kukaanzishwa Idara ya uchunguzi ambayo ingekuwa tofauti na POLISI,USALAMA WA TAIFA TISS,MAGEREZA,FIELD FORCE,USALAMA BARABARANI , MAPAMBANO MADAWA YA KULEVYA etc zikawa ni idara zinazojitegemea
  • COASCO na CAG (Hawa naona waunge nguvu liwe shirika moja hatuwezi kuwa na Mamlaka mbili za ukaguzi katika nchi moja)
  • Shirika la POSTA , TCRA na TTCL hizi zilipaswa kuwa kitu kimoja huku vikiongoza sector binafsi
  • SIONI KAMA KUNA HAJA YA WIZARA YA TAMISEMI wakati kazi zake nyingi zipo kwenye Wizara nyingine..kwa mfano kusimamia Afya kazi ya Wizara ya afya, Kusimamia Elimu kazi ya wizara ya Elimu, Kusimamia utumishi wa Sekretarieti za mikoa na mitaa Lipo Chini ya Wizara ya Utumishi na Utawala Bora
  • TMDA ingepelekwa ikawa kitengo Ndani ya MSD cha ukaguzi
  • Sioni sababu kuwepo na Mkuu wa wilaya kma kuna Mkurugenzi wa wilaya hii ndo hupelekea migongano ya kimajukumu Aidha ifutwe Mkuu wa wilaya au iondolewe post moja kati ya hizo
 
Hapo umebugi
 
πŸ™πŸ†’πŸ‘
 
We ndio bure kabisa
 
Mamlaka ya kupambana na dawa za kulevya ipelekwe polisi,REA iunganishwe na TANESCO VETA na NACTE
Mamlaka ya madawa ya kulevya kuwa chini ya polisi siungi mkono..
Polisi ni enforcement ila mamlaka ya madawa inajaribu kurecover society
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…