Tanzania hakuna Shirika la Kijasusi kuna Idara ya Ujasusi inayofanya kazi chini ya Taasisi ambayo ni Ofisi ya Raisi.
Kivitendo hiyo Idara ya Usalama wa Taifa inawajibika kwa Raisi ambaye ni Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Hivyo CCM na Raisi Magufuli wakiamua kufutilia mbali hao Usalama wa Taifa wanaweza na hakuna atakayewazuia Kisheria. Sema kiuhalisia CCM hawezi kufanya hivyo kwasababu huo ndiyo utakuwa mwisho wao pamoja na familia zao.
Hili hata Nyerere aliliweka bayana: "The Government is an Instrument of the Party" hapa alizungumzia Bunge, Mahakama na hata Jeshi. Tena mshukuru siku hizi mambo yamebadilika sanaa, miaka ya nyuma unaweza kukuta mwana-CCM kama Mangula au Makamba anawaamrisha na kuwatumia hawa TISS hovyo kabisa.
Kuna miaka ya nyuma huyu Mzee Kingunge na Marehemu Mzee Siyovelwa pamoja na TISS walitendaga madhambi kule Iringa sitaki hata kukumbuka. Yaani mfumo huu uliopo ni mbaya na unachangia kurudisha taifa nyuma. Wamechukua mifumo ya:
- Communist Party of the Soviet Union (CPSU) na The KGB.
- Communist Party of China (CPC) na Ministry of State Security.
- Communist Party of Cuba na Direccion General de Inteligencia.
Sasa kwenye hii mifumo Chama kikivamiwa na mamluki basi Intelijensia ya nchi lazima iharibike tu.
Mfano Mzuri kabisa kuwahi kutokea:
Urusi ya Kisovyeti na Ujanja wake wote ule walikuja Wanachama wa hovyo hovyo wa CPSU wakina Mikhail Gorbachev na Boris Yeltsin wakaharibu kila kitu mle ndani. KGB iliparanganyika vibaya sana kisa tu ilikuwa inaripoti kwenye Politburo ya Chama cha Kikomunisti cha Urusi.