Mashirika ya ndege yaukimbia uwanja wa ndege Chato. Hakuna ndege yoyote inayotua tena uwanjani hapo!

Mashirika ya ndege yaukimbia uwanja wa ndege Chato. Hakuna ndege yoyote inayotua tena uwanjani hapo!

Siyo kweli jamani mbona Jana nimeona kunguru, njiwa, pugi, madudumizi, nguya, visirimilo, utongwa, visonzi, vikucha, ninga, kware, n.k wametua na kujivinjari kwenye uwanja wa ndege ulojengwa level ya Bitumen au mna wivu? Au Sijawaelewa?
Kwa kuongeza kidogo ndege za abiria zimesitishwa kupisha ikolojia inayoendelea pale ikiwamo viumbe kujamiiana na kuongezeka Ili kujaza pori la chato na pia viumbe kuwindana nadhani nasema kweli ndugu zangu
🤣🤣🤣🔊
 
Uwanja wa Chato ulijengwa kwa haraka kama sehemu ya mkakati wa Bahima Empire …….ndugu yake hana sehemu ya kuweka ndege zake za kijeshi na ameziombea Ethiopia …ambako nako kutokana na Migogoro ni tabu , kikubwa siku moja mkoa wa Chato ungejimega ni kuwa sehemu Yao ..huo uwanja ni sehemu ya mkakati Mpana ndio maaana uliharakishwa sana
Kama Hakuna wateja basi TPDF watapeeleka kituo cha jeshi la anga cha mwanza Kiwe kinautumia
 
Hahahahaaah Kitombile hamna alternative? Ikibidi muanika pamba zenu au mchunge ng'ombe pembezoni
Figisu hizo japo hizo pesa za kujenga li uanja chato ni bora kiwanja chetu cha Mwanza kingejengwa nahuo uwanja utaendelea kufanyiwa figisu na hawamu hii mpka waanikie dagaa wa ziwani, hii nchi ngumu sana.
 
Bora mchunga ngombe alijitaidi kuhakikisha umeme unapatikana muda wote, wa sasa yeye ni mchunga nini au mchunga ngedere?
😄 🤣 😂 😆 😄 naona unasaka ugomvi na wavaa makobazi sasa
 
Hata kampuni moja ya ndege iliyokuwa inakwenda Chato, mara moja kwa wiki, sasa imesimamisha safari zake.

Ofisa Uhusiano wa Shirika la Ndege Tanzania (ATCL), Sarah Reuben akijibu swali la Mwananchi “kwa nini safari za Chato zimefutwa,” anasema “hazijafutwa” isipokuwa kuna mabadiliko katika mpangilio wa safari kwenye viwanja kadhaa.

“Kutokana na baadhi ya ndege zetu kupaki (kuwa katika matengenezo), tumepunguza safari katika baadhi ya viwanja (njia) na sio kwamba tumesitisha,” anasema Reuben alipoulizwa na Mwananchi Juni 21.

Anafafanua kuwa hatua hiyo inatokana na mahitaji ambapo baadhi ya viwanja vimeongezewa safari.
Kwa mujibu wa tovuti ya ATCL, kwenye ukurasa wa kununua tiketi, hakuna ndege kwa abiria wanaosafiri kutoka au kwenda Chato hadi Agosti 3, 2023.

Wakati ATCL inaanza kutua katika uwanja huo, Januari 2021 ilikuwa inafanya safari tatu kwa wiki yaani Jumatatu, Alhamisi na Jumamosi.

Lakini sasa safari zimebaki mbili (Alhamis na Jumamosi) ambazo nazo kiuhalisia hazipo kwani katika tovuti ya shirika hilo ukitaka kununua tiketi kwa ajili ya safari za kutoka au kuelekea Chato unaambiwa hakuna nafasi au hakuna ndege.

Hii ina maana kwamba ndoto za Rais John Pombe Magufuli mwasisi wa wazo na mipango ya kujenga uwanja wa ndege wa Chato kama bado zipo basi zimetatizwa. Dk Magufuli aliingia madarakani Novemba 5, 2015 na miezi tisa tu baadaye, Agosti 31, 2016, Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroads) ilisaini mkataba na Kampuni ya Mayanga Contractors Co. Ltd kujenga uwanja huo unaotajwa kuwa ni wa tatu kwa ukubwa baada ya wa Juliua Nyerere na (JNIA) na wa Kilimanjaro (KIA).

Katika bajeti ya Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi ya mwaka wa fedha 2023/2024, zimetengwa Sh1 bilioni kwa ajili ya kuendeleza uwanja huo.

Kabla ya bajeti kulikuwa na tetesi miongoni mwa wafuatiliaji wa maendeleo ya ujenzi wa uwanja huo, kuwa wizara ingekuja na bajeti maalumu ya kukamilisha moja kwa moja uwanja huo wa ndege ambao mpaka hapo ulipofikia unakadiriwa kugharimu zaidi ya Sh 50 bilioni.

Akiwasilisha bajeti hiyo bungeni, Mei 22, 2023, Waziri wa Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa alisema Serikali inaendelea kutafuta fedha kwa ajili ya ujenzi wa jengo la abiria na mnara wa kuongozea ndege.

Hayo yanajiri wakati Meneja wa Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroads) Mkoa wa Geita, Japherson Nnko anasema kukamilisha awamu zote za ujenzi wa uwanja kutategemea uwezo wa Serikali kifedha na umuhimu wa kugharimia mradi husika.

Nnko alikuwa akihojiwa na Mwananchi, miezi mitatu iliyopita aliposema ujenzi wa uwanja wa Chato ni endelevu na kwamba “mchakato unaoendelea sasa ni ujenzi wa uzio ambao ni muhimu kwani ndiyo unavutia kampuni za ndege kuja kwa kuwa wanakuwa na uhakika wa usalama,” anasema Nnko.

Mtumishi mwandamizi wa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi ambaye hakutaka jina lake litajwe gazetini anasema, kuna “umuhimu mdogo” wa kuendelea kuwekeza katika uwanja huo. “Baada ya ujenzi wa uzio itakuwa imetosha. Uwanja wenyewe hautumiwi ilivyotakiwa na hata safari za ATCL hivi sasa zimesimamishwa. Hakuna haja ya kuendelea kufanya uwekezaji pale,” amesema.

Mtumishi huyu asiye na matumaini anahoji, “Uwanja ujengewe jengo la abiria? Kwa ndege zipi? Ngapi? Hili jengo la watu mashuhuri lililopo ambalo sasa linatumiwa na watu wote ni kubwa kuliko mahitaji ya sasa. Jingine la nini?” Kwa upande wa Mkurugenzi wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege nchini (TAA), anayehusika na usimamizi wa viwanja vya mikoa, Hamis Amiri aliliambia gazeti hili Februari mwaka huu, kuwa mamlaka yake haina mpango wa hivi karibuni wa kuuongezea uwezo zaidi uwanja wa ndege wa Chato.

Amesema hiyo ni kutokana na a uwezo wake wa sasa ni mkubwa kuliko huduma inayotolewa. “Wakati huo uwanja ulikuwa unatumiwa na shirika moja tu la ATCL kwa safari zilizoko kwenye ratiba na rubani aliongozwa kwa msaada kutoka Uwanja wa Ndege wa Mwanza uliopo kilomita 235 kutoka Chato. Ndege kubwa kama Dreamliner (Boeing 787-8, zenye kubeba abiria 248 zinaweza kutua hapa.

Takwimu za TAA zinaonyesha kuwa katika kipindi cha miezi sita (kuanzia Julai 2022 hadi Desemba 2022), idadi ya ndege zilizotua na kupaa katika uwanja huo zilikuwa 112 zikiwa na abiria 2,111. Pia hakuna mzigo wowote uliosafirishwa kupitia uwanja huo katika kipindi hicho. Mzigo ni kifurushi chochote kinachoanzia uzito wa gramu 500 ambacho husafirishwa kibiashara katika eneo la mizigo (sio sehemu ya uzito ambao abiria anapewa kwenye tiketi yake).

Mmoja wa maofisa wa uwanja wa Chato aliyekutwa uwanjani Februari 2, 2023 aliiambia Mwananchi kuwa tangu kuanza kutumika kwa uwanja huo Januari 9, 2021, ni ATCL pekee inaoutumia na idadi ya nafasi zilizotengwa kwa abiria zilikuwa 30.

Amesema mara ya mwisho uwanja huo kuhudumia ndege nyingi ni wakati wa msiba wa Rais John Magufuli. “Siku moja kabla na siku ya mazishi tulipokea ndege kubwa zaidi ya 20 na ndogo zilizokuwa zimebeba waombolezaji. Kuna muda ndege nane zilikuwa zinaegesha kwa wakati mmoja,” alisema ofisa huyo.

“Watu waelewe kwamba Uwanja wa Chato tunautumia kama mmbadala uwanja wa Mwanza ukipata shida. Chato kuna ndege zinatua kupitia Mwanza kuna ndege ya Air Tanzania inatua Chato kupitia Mwanza,” amesema.
Hata zile Ndege za Mseveni haziendi tena
 
All in all kujenga international Airport Chato ilikuwa wazo na kijinga from economic perspective. Kwanin uwanja wa Mwanza usingepanuliwa uwe international?!! Mwanza mji mkubwa unahitaji international Airport ambao kwa namna flani pia uko centre ya east African countries na pia ni viable economically. Tatizo la nchi hii vipaumbele ni hiisia na mapenzi binafsi ya rais badala ya kuwa priorities ziwe determined na economic benefits.
 
Maskini Chato. Imegeuka Gbadolite hata kabla mwili wa mwendazake haujazoea ardhi! Ngoja tuone kama taifa tutakubali kuzamisha fedha yote hii na kuacha iteketee. Nimeona sababu ni kwanini viongozi wengi kama Jakaya Kikwete waliamua kuwa mafisadi wa wazi wazi kwa ajili ya familia na marafiki zao. Hili ni tatizo la Afrika.
Hata kwa Matendo jiwe alimsadifu mobutu kwa roho mbaya na ubinafsi, ukanda na ukabila na kuanzisha miradi ya hovyoo
 
All in all kujenga international Airport Chato ilikuwa wazo na kijinga from economic perspective. Kwanin uwanja wa Mwanza usingepanuliwa uwe international?!! Mwanza mji mkubwa unahitaji international Airport ambao kwa namna flani pia uko centre ya east African countries na pia ni viable economically. Tatizo la nchi hii vipaumbele ni hiisia na mapenzi binafsi ya rais badala ya kuwa priorities ziwe determined na economic benefits.
What happens wanasiasa wanapofanya maamuzi based on siasa na sio professionalism , au kusikiliza ushauri wa wataalam, matokeo yake project hewa zinazoleta hasara
 
What happens wanasiasa wanapofanya maamuzi based on siasa na sio professionalism , au kusikiliza ushauri wa wataalam, matokeo yake project hewa zinazoleta hasara
Exactly rais anaamini ana akili kuliko watu wengine na anajua kila kila kitu mwisho wake anasababishia nchi hasara kwa maamuzi ya hovyoo
 
Kama ulitumika wakati wa mazishi pia ilitosha.

Huo ilikuwa sadaka yetu kwa Magufuli. Alitumikia taifa kwa uaminifu na sasa tunayaona.

Kuna mabilioni ya kodi yanapotea na wala hayajulikani yanapotelea wapi.
Kabisa
 
Back
Top Bottom