Utendaji wa sasa wa wafanyakazi wa Tanesco katika kushughulikia dharura za umeme zinapotokea, kwa kweli zinatufurahisha wateja kwani ni za haraka na za ufanisi mno.Sijajaua nani aliyeleta mwamko huu katika shirika hili la umma amblo mwanzoni zilikuwa haziridhishi. Ila kama ni ujio wa mtendaji mkuu,basi Mwenyezi Mungu amzidishie na ikiwezekana akishaiweka vizuri Tanesco, apelekwe na kwenye mashirika mengine ya umma kama Dawasa,TTCL n.k akarekebishe mambo huko.
Mimi nipo Dar, linapotokea tatazo ,unapopiga ile simu ya dharura au hata ukiandika kaka group la Whatsapp katika magroup waliyoyaanzisha katika maeneo, basi baada ya muda mfupi tu, team itaingia na kuanza kazi .Haitoshia hapo ,kwani wakishamaliza na huduma kurudi,baada ya muda utapigiwa simu kama tatizo lako limetatuliwa. Isitoshe,taarifa za kuaktika umeme zinatolewa mapema katika magroup ya whatsapp,na kisha huduma itakaporudi wanaomba radhi kwa yaliyotokea.Katika magroup hayo kwenye maeneo wanaweka mpaka afisa wa zamu na muda na mawasiliano yake.
Tanesco sasa hivi wana operate kwenye level nyingine ,yaani katka viwango vya nje na siyo vya hapa kwetu kama tulivyozoea.
Tunaomba mashirika ya umma mengine kama TTCL, dawasa n.k. nao waige mfano wa utendaji huu wa Tanesco, kwani wananchi watapunguza manung'uniko kwa serikali yao.