Mashirika ya umma kuunganishwa, manne kufutwa

Mashirika ya umma kuunganishwa, manne kufutwa

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
TAARIFA - MASHIRIKA 16 YALIYOUNGANISHWA N 4 KUFUTWA_page-0001.jpg

TAARIFA - MASHIRIKA 16 YALIYOUNGANISHWA N 4 KUFUTWA_page-0002.jpg

TAARIFA - MASHIRIKA 16 YALIYOUNGANISHWA N 4 KUFUTWA_page-0003.jpg

TAARIFA - MASHIRIKA 16 YALIYOUNGANISHWA N 4 KUFUTWA_page-0004.jpg
 
Wakimaliza hilo waanze na kufuta/kuvunja na kuunganisha wizara. Hii nchi yetu haihitaji kuwa na mawaziri zaidi ya 10.

Kuna wizara ya maji...
Kuna wizara ya uvuvi...
Kuna wizara ya kilimo
Kuna ya wizara ya maliasili....
Kuna wizara ya mifugo (sijui na uvuvi?)
Kuna wizara ya mazingira...
Kuna wizara ya ardhi...

Ukichunguza kwa makini ni vitu vinavyoshahabiana, kuhusiana na kuingiliana kwa 100%. Kwanini vyote visiwe ni wizara moja tu?
 
Mbona bado kuna taasisi za Umma nyingi tu ambazo zimeachwa bila ya kuunganishwa pamoja na kuunda taasisi moja??
Zipo taasisi au mashirika mengi sana ya Serikali ambayo yanapaswa kuunganishwa pamoja kwa sababu yanafanya kazi zinazofanana au kuingiliana ktk majukumu.
Hawa watu waliofanya kazi hii ya kuunganisha hizi taasisi hawajafanya Uchunguzi na Utafiti wa kina kuhusu suala hili.
Kwa maoni yangu ni kwamba, walipaswa kuualika umma wa Watanzania ili watoe maoni yao (Public Opinion) katika mchakato huu wa kuunganisha mashirika na taasisi za umma kabla ya kufikia hitimisho hili walilofanya. Sijui ni kwa nini Serikali huwa haitaki kuwashirikisha wananchi kwenye masuala nyeti kama haya ya ujenzi wa Taifa lao?? Sijui Serikali inaogopa kitu gani kuwashirikisha wananchi kwenye masuala kama haya??
Endapo kama Wananchi wangeshirikishwa kwenye suala hili, naamini kwa dhati kabisa kwamba wangeweza kuja na maamuzi au hitimisho ambalo ni bora zaidi kabisa kwa mustakabali mwema wa nchi yetu.
Hivi tunakwama wapi Watanzania ?????????????
 
TCAA na TAA iwe shirika moja.

PURA ,EWURA na PBPA iwe ni shirika moja ila pawe na vitengo.

TPA na TASAC iwe shirika moja .

GEPG na GPSA liwe shirika moja wawe wanafanya procurement na kudili plus kuratibu miamala yote inayokwenda serikalini.
 
Back
Top Bottom