Mashirika ya umma kuunganishwa, manne kufutwa

Mashirika ya umma kuunganishwa, manne kufutwa

Mbona bado kuna taasisi za Umma nyingi tu ambazo zimeachwa bila ya kuunganishwa pamoja na kuunda taasisi moja??
Zipo taasisi au mashirika mengi sana ya Serikali ambayo yanapaswa kuunganishwa pamoja kwa sababu yanafanya kazi zinazofanana au kuingiliana ktk majukumu.
Hawa watu waliofanya kazi hii ya kuunganisha hizi taasisi hawajafanya Uchunguzi na Utafiti wa kina kuhusu suala hili.
Kwa maoni yangu ni kwamba, walipaswa kuualika umma wa Watanzania ili watoe maoni yao (Public Opinion) katika mchakato huu wa kuunganisha mashirika na taasisi za umma kabla ya kufikia hitimisho hili walilofanya. Sijui ni kwa nini Serikali huwa haitaki kuwashirikisha wananchi kwenye masuala nyeti kama haya ya ujenzi wa Taifa lao?? Sijui Serikali inaogopa kitu gani kuwashirikisha wananchi kwenye masuala kama haya??
Endapo kama Wananchi wangeshirikishwa kwenye suala hili, naamini kwa dhati kabisa kwamba wangeweza kuja na maamuzi au hitimisho ambalo ni bora zaidi kabisa kwa mustakabali mwema wa nchi yetu.
Hivi tunakwama wapi Watanzania ?????????????
Kwa kulalama tu hamjambo

Hujataja hata taasisi moja
 
Kwa kulalama tu hamjambo

Hujataja hata taasisi moja
Ninazifahamu taasisi nyingi tu ambazo zinafaa kuunganishwa, sikuzitaja hapa kwa makusudi kabisa wala siyo kwa bahati mbaya, ukizingatia kwamba uamuzi na hitimisho kuhusu suala hili tayari umeshafanywa na Serikali. Aidha, sijajua sababu hasa za Serikali za kutokutaka kupata Public Opinion juu ya jambo hili.
 
Hivi ni lini serikali itaanzisha bodi ya pombe?

Halafu pia serikali ifute cheo cha naibu waziri mkuu haraka!

Mawaziri katika ofisi za waziri mkuu na makamu wa rais wanafanya nini huko ofisini?

Makamu wawili wa rais na waziri mkuu kiongozi Zanzibar yenye idadi ya watu sawa na wilaya ya Sengerema ni ubadhirifu vyeo hivyo vifutwe mara moja!
Suluhisho pekee kwa yote haya uliyotaja ni upatikanaji wa Katiba Mpya itakayotokana na Fikra, Maoni na Mawazo ya wananchi wote ktk nchi hii.
 
ccm mambo ya uchaguzi yakikaribia huwa wanawehuka...kila mahala, akili huwa zinajaribu kurudi kidogo ila mwisho wa uchaguzi upumbavu huwarudia, yaani sawa na mlokole anapoamua kuokoka shetani huwa haendi mbali anakaa pembeni anamsubiria mizuka imuishe airudie dhambi shetani ajinufaishe tena...ajitaifishie mali. Naona copy yao wanayo ccm....😡
 
Wakimaliza hilo waanze na kufuta/kuvunja na kuunganisha wizara. Hii nchi yetu haihitaji kuwa na mawaziri zaidi ya 10.

Kuna wizara ya maji...
Kuna wizara ya uvuvi...
Kuna wizara ya kilimo
Kuna ya wizara ya maliasili....
Kuna wizara ya mifugo (sijui na uvuvi?)
Kuna wizara ya mazingira...
Kuna wizara ya ardhi...

Ukichunguza kwa makini ni vitu vinavyoshahabiana, kuhusiana na kuingiliana kwa 100%. Kwanini vyote visiwe ni wizara moja tu?
Sio kweli mkuu
 
Ninazifahamu taasisi nyingi tu ambazo zinafaa kuunganishwa, sikuzitaja hapa kwa makusudi kabisa wala siyo kwa bahati mbaya, ukizingatia kwamba uamuzi na hitimisho kuhusu suala hili tayari umeshafanywa na Serikali. Aidha, sijajua sababu hasa za Serikali za kutokutaka kupata Public Opinion juu ya jambo hili.
Hii ni awamu ya kwanza !!! Mchakato bado unaendelea !!
 
Back
Top Bottom